Waislamu Mnafeli wapi?

Waislamu Mnafeli wapi?

Lengo
Lengo ni kupata viumbe watiifu ambao wamefuata amri za Mola wao walipwe Kwa matendo Yao mema

Na

Wabaya walipwe Kwa matendo Yao,kwenda motoni
Sasa niambie aliyeruhusu uwepo wa hayo matendo mabaya(Vishawishi) ni nani?
 
Umekuwa unaikumbatia Sana hoja ya Uhuru WA kuchagua kuzaliwa,naona hii ndo inakubeba Sana

Naomba unijibu swali hili!

Je unakuwa hai Kwanza kabla ya kuzaliwa?
Naona hili swali ameshindwa kujibu
Hata mimi nimemuuliza pia naonayupo na uhuru wake tu
 
Kwa kusema hivyo ni kwamba umekubali hoja muhimu ya Kiranga kwamba mwanadamu hana uhuru wa kuchagua kitu chochote ambacho kiko nje ya kile mungu alichopanga si ndio?
Na kwani ulikuwa hai kabla ya kuzaliwa??

Ukilijibu hili swali nami nitajibu la kwako

Au ulipokuwa mtoto mdogo ulikuwa unachagua kula ugali badala ya kunyonyeshwa?
 
Na kwani ulikuwa hai kabla ya kuzaliwa??

Ukilijibu hili swali nami nitajibu la kwako

Au ulipokuwa mtoto mdogo ulikuwa unachagua kula ugali badala ya kunyonyeshwa?
Mkuu umeniuliza swali ambalo mimi halinihusu...hakuna pahala nimeongea mambo ya kuzaliwa au kutokuzaliwa.
swali langu ni kwamba kwa mujibu wa post yako hapo juu, unakubali kwamba binadamu hawezi kufanya kitu ambacho ni nje ya mipango ya mungu? nakuomba Usichanganye swali langu na la kiranga.
 
Mithali 19:21 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

Hivyo it's true kwamba
Binadamu hawezi kufanya kitu ambacho ni nje ya mipango ya Mungu
 
Mungu hatupi nafasi hiyo kwa sababu
Yeye ndio mpangaji wa kila kitu na ndio muamuzi wa kila kitu katika dunia hii
Kuwa mpangajibwa kila kitu si sababu.

Kwa sababu, kuwa mpangaji wa kila kitu hakumzuii kutupa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe.

Sasa, kwa sababu unasema Mungu ndiye mpqngaji wa kila kitu, kwa nini kaamua tuzaliwe bila kuchagua?

Kwa nini hajatupa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe? Hususannkwa sababu tunaambiwa Mungu katupa uhuru wa kuchagua mambo, sasa kqma Mungu hatupi uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, hapi tunabuhuru gani wa kuchagua?

Ukisema Mungu ndiye mpangaji hujajibu swali, umekubali kwamba huna jibu.

Mimi sijasema Mungu si mpangaji, ninekuuliza kwa nini kapanga hivi na si vile, hususan kwa sababu hivi alivyopanga kuna contradict habari nzima ya uhuru wetu kuchagua?

Hujajibu swali. Umekubali huna jibu.
 
Umekuwa unaikumbatia Sana hoja ya Uhuru WA kuchagua kuzaliwa,naona hii ndo inakubeba Sana

Naomba unijibu swali hili!

Je unakuwa hai Kwanza kabla ya kuzaliwa?
Siwi hai kabla ya kuzaliwa.

Na mimi nakuuliza swali.

Mungu wako muweza yote alishindwa kutupa uchaguzi kuhusu kuzaliwa, kabla hatujazaliwa na kuwa hai?

Alishindwa kutuonesha "haya maisha, ukikubali kuzaliwa utakutana na hili na lile, kuna kufa, kuna magonjwa, kuna njaa na kushiba, kuna vita na raha, nataka uishi hivi, usiishi vile, unakubali kuzaliwa?" au hukubali?"

Kwa nini hakutupa nafasi hiyo?
 
Kuwa mpangajibwa kila kitu si sababu.

Kwa sababu, kuwa mpangaji wa kila kitu hakumzuii kutupa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe.

Sasa, kwa sababu unasema Mungu ndiye mpqngaji wa kila kitu, kwa nini kaamua tuzaliwe bila kuchagua?

Kwa nini hajatupa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe? Hususannkwa sababu tunaambiwa Mungu katupa uhuru wa kuchagua mambo, sasa kqma Mungu hatupi uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, hapi tunabuhuru gani wa kuchagua?

Ukisema Mungu ndiye mpangaji hujajibu swali, umekubali kwamba huna jibu.

Mimi sijasema Mungu si mpangaji, ninekuuliza kwa nini kapanga hivi na si vile, hususan kwa sababu hivi alivyopanga kuna contradict habari nzima ya uhuru wetu kuchagua?

Hujajibu swali. Umekubali huna jibu.

Naomba nikuulize tena

Kama huwi hai kabla ya kuzaliwa, na unahitaji kupewa nafasi ya kuchagua yale utakayo sasa utachaguaje kama hauko hai??

#jibu unalifahamu lakini hutaki kulielewa
 
Kwa kusema hivyo ni kwamba umekubali hoja muhimu ya Kiranga kwamba mwanadamu hana uhuru wa kuchagua kitu chochote ambacho kiko nje ya kile mungu alichopanga si ndio?
Yani unaambiwa Mungu ndiye mpangaji wa kila kitu, halafu mtu akikosea, dhambi ni ya mtu.

Hivi hili linaingia akilini?
 
Naomba nikuulize tena

Kama huwi hai kabla ya kuzaliwa, na unahitaji kupewa nafasi ya kuchagua yale utakayo sasa utachaguaje kama hauko hai??

#jibu unalifahamu lakini hutaki kulielewa
Unataka kuniambia Mungu wako muweza yote alishindwa kutupa uchaguzi wa kuamua tuzaliwe au tusizaliwe kabla hatujazaliwa?

Kama hakushindwa, kwa nini hakutupa nafasi hiyo?

Kama alishindwa, je, huyo Mungu kweli ni muweza yote?
 
Mithali 19:21 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

Hivyo it's true kwamba
Binadamu hawezi kufanya kitu ambacho ni nje ya mipango ya Mungu
vyema..kwa kutokana na jibu lako nikisema kwamba fate ya mwanadamu anayei-determine ni mungu unakubaliana nami?
 
Kwa hivyo sheria ya nchi mtu akiikiuka ni nchi ndio imefanya makosa??
Sheria ya Mungu wako muweza yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni sawa na sheria ya nchi inayowekwa na watu wasio na uwezo wote, ujuzi wote wala upendo wote?
 
Unataka kuniambia Mungu wako muweza yote alishindwa kutupa uchaguzi wa kuamua tuzaliwe au tusizaliwe kabla hatujazaliwa?

Kama hakushindwa, kwa nini hakutupa nafasi hiyo?

Kama alishindwa, je, huyo Mungu kweli ni muweza yote?

Naendelea kusema kwamba
Mungu wetu ni pendo
Mwingi wa rehema alitupenda tangu mwanzo
Japo tulitanga mbali nae ila anatuonyesha upendo,
Ni wangapi wanaozaliwa na kufa?? Papo hapo Na wengine mimba zao zinatoka kabla hawajazaliwa?
Ila mungu katupenda sisi na ndio maana mpaka leo tupo hai
 
Sheria ya Mungu wako muweza yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni sawa na sheria ya nchi inayowekwa na watu wasio na uwezo wote, ujuzi wote wala upendo wote?
Ni mfano nimechukulia
Ila tambua ya kuwa Mungu aliweka sheria zake na alitukabithi hata kama huijui dini tayari alikwishaziweka katika moyo wakila mwanadamu

Au we hujui ya kuwa kuua ni kosa?
Kusema uongo je?

Sasa kama Mungu alitupa taratibu zake iweje tuzivunje sisi na liwe kosa lake??
 
hayo masuala ya majini na ushirikina ni mambo ya kimilia ya kiswahili na kiafrika. Hayana mahusiano kabisa na uislamu.

Uislamu ulishaeka wazi kuwa uchawi na ushirikina unamtoa mtu ndani ya uislamu, ni dhambi kubwa yao kuliko zote.
Mimi nikajua ili uwe uko lazima uwe na majini maana naona wengi wao wana majini na kujisifu na kupiga watu biti mtaani kabisa.
Okay naendelea kujifunza maana toka utoto kule dsm tuko karibu na msikiti na mjirani 50% waislamu
 
Vyema. kwa kutokana na jibu lako,nikikwambia watu wa kuingia motoni na mbinguni mungu anakua kashawapanga tayari tunakubaliana katika hilo?

Sio kashawapanga ila anawafahamu wale wa kuingia katika lile ziwa la moto

Basi kwa kuwa kila mmoja ana uhuru wa kufanya kila anachokipenda
Na ndivyo hivyo ya kuwa Mungu anawajua walio wake
Na siku ya mwisho atatenga wanakondoo mkono wa kuume na Mbuzi mkono wa kushoto,
Pia hata kama M/Mungu amekuandika katika wale watakaoingia motoni ila ukaamua kuacha dhambi na matendo maovi basi anakurehemu na kusamehe dhambi zako.

#Nawafahamu walio wangu
 
Back
Top Bottom