Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Makamu kutokupatikana naona wanatengeneza pressure nyingine wakati pressure iliyopo tayari si nzuri. Wasicheze na picha inayojengwa kwa public! Ikianza kampeni ya kudai aonekane kwa public italeta image mbaya sana.
Image kwao si issue kabisa. Swali wanalohangaika nalo ni hili: Nchimbi anatolewaje na akaendelea kuwa huru.
 
Ukiukaji wa Katiba haina maana Katiba yenyewe ndio Mbovu. Nauliza:-
Kwa nini pale Viongozi wanapokiuka Katiba ya nchi, sisi husema sababu ni hii Katiba Mbovu? Tunahofia nini..
Ninakubaliana na wewe juu ya hili.

Katiba haiwezi kuwa mbadala wa kiongozi anayefuata taratibu na kutimiza wajibu wake wa uongozi kwa wote anaowaongoza.

Katiba ni maelekezo/mwongozo tu wa taratibu zinazosaidia viongozi kutimiza majukumu yao ndani ya taratibu hizo

Hizo taratibu, kiongozi mbaya anaweza kuzisigina wakati wowote, kama inavyofanyika sasa na wakati wa rafiki yako Magufuli..

Katiba Kuu kwa kiongozi yeyote ni kuipenda na kuitumikia nchi yake na wananchi wake kwa dhamira isiyotetereka.
 
EJN resigned at the proverbial gunpoint. Otherwise, no one resigns, goes into hiding and gets expelled by his political party at the same time!
 
Hajajiuzulu, kafukuzwa
 
Wakati wa rafiki yangu, mimi naamini hakuyafanya yeye bali waliyawanya wao, yeye akawa Bangusilo na hii ilifanyika ili watu kama nyie mumchukie yeye.

Chukulia utekwaji wa Mo Dewji! isitoshe. Ukimsikiliza kwa makini sana Polepole utanielewa, japo kuna watu wamesha aminishwa kuwa utekaji na mauaji ilikuwa kazi ya Magufuli. Kwa wanamojua Magufuli kwenye IMANI ya KIROHO watakwambia sii mtu anayeweza fanya mambo yale.

MAGUFULI alikuwa Gaddafi wa Tanzania (Magufulification) ukimkosea, ukimuudhi anakuchana mbele za watu hafichi kutumbua mtu yeyote hadharani na hili liliwachukiza wengi ati udhalilishaji kwa nini isiwe siri

Niishie hapa, maana kama Polepole aliweza kupotezwa hata Makamu wa rais anaweza kupotezwa! Mimi nani wa kusimama kidume mbele ya mfumo kandamizi.
 
Utamaduni wa serikali na CCM ya Samia ni kujitekenya na kucheka wenyewe. Wakishafanya maamuzi yao ya hovyo na kutoa justification zao za hovyo wanadhani watu wote duniani wa akili za hovyo kama wao.

Ukisha dogosha document muhimu katika nchi ni kakitabu tu, ina maana uelewi hata rationale ya kuandika hiko kijikitabu.

Katiba ina rationale nyingi behind every section. Kwa swala Nchimbi ni ‘power relation’ na hizo aspects uandikwa kwa ku-balance protection ya taasisi/kiongozi kuingiliwa majukumu yake au kuwa overruled kirahisi. Lengo ni serikali kuwa predictable and ordered, sio taahira mmoja tu ajiamkie asubuhi na kusema tutumie madaraka ya taasisi yetu kumtoa kiongozi fulani it doesn’t work that way.

In a codified institution kama kuna maelezo ya kumtoa kiongozi kwa njia zilizo orodheshwa uwezi kwenda kutunga upuuzi wako kumuondoa.

Makamu wa raisi hawezi ondolewa kwa kufukuzwa chama kama hilo halipo kwenye katiba, Maana yake he is protected, ukitaka kumtoa mpate na hatia (mahakamani), peleka hoja bungeni (inaweza hata kuwa kuvunjika kwa maelewano na raisi) bunge likiridhia he is out.

Yes katiba ya Tanzania inaruhusu raisi kukutimua kupitia bunge kama hakutaki, baada ya kumtoa V.P kwa njia halali ndio unaweza mfukuza chama. Lakini uwezi mwondoa kwa taratibu ambazo hazipo kikatiba.
 
Mkandara..binafsi naamini lilitokea jaribio la kwanza la kumuondoa JPM kule Mtwara. Wakaona inawezekana, ilipotokea mara ya pili hawakulazia dame.
 
Umeona sasa...yaani kama wanaamini "uzuri wa Katiba" wangeonesha kweli wanaiamini!!
Anajisifiaje uzuri wa katiba wakati anashindwa kitu cha msingi kabisa kama uwazi?

Nchimbi mpaka sasa hajaonekana, alitakiwa kufanya mkutano na waandishi na kujieleza kwa wananchi.

Yule Asha-Rose Migiro kafanya mkutano na waandishi, ukimuangalia unaona kabisa huyu anaona aibu.

Kafanya mkutano wa dakika tatu kama anakimbizwa, kashindwa hata kusema "Kidumu Chama Cha Mapinduzi". Kashindwa kuchukua swali hata moja la ngama.

Wao wenyewe wanajua wanafanya maigizo.
 
Unajua umesema kitu hapo nimecheka kidogo...kwao "katiba ni nzuri" wanapotaka kujificha..lakini ukiwaambia mbona inatambua haki ya kutoa maoni ya kuudhi wataanza kuikandia Katiba hiyohiyo. Ni nzuribkwa kujifichia, lakini si kwa kuweka uwazi. Kama wanaamini kweli swali la Nchimbi yuko wapi lisingekuwa na manikin.

Hata hivyo..wanatudokeza kwa ukimya wao Nchimbi akitokea hadharani atakuwa na msafara Maya wa kuelekea mahakamani na pingu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…