Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Kuna wengine na mie nikiwemo, tunaamini mzee Mwinyi ndie aliitengeneza tz baada nyerere kuiuwa

Wakati wa nyerere watu waliogea arita, sukari, mchele, unga na vinginevyo ilikuwa ni anasa, lakini Mwinyi alipoingia tu ruksaaaaa mambo yakanyooka
 
Nyumbu wanashida wamekomaa na Nyerere badala ya kujiuliza kwa nini uchumi wa chadema umedumaa miaka yote na ofisi ya chama kubaki na hadhi ya choo cha uswahilini
Mkiwa umerudi upyaa baada ya wasiojulikana kupata nguvu tena kupitia Waenezei😆😆
 

Mkuu una umri gani? Ulipigana vita vya kagera? Tanzania Ina umri wa miaka 62 sasa. Umri wa mtu bado anaishi. Na kama ni huku ulaya Basi ataitwa noch Jung. Je unadhani kuanza au mwanzo ni rahisi. Umaendika as if Kenya waliokuwa na ubepari watu wake wanaishi Kama wa Luxemburg [emoji1152]. Kama unataka kusaidia mada kwa nia ya kwenda mbele, jadili Sio kuhukumu.
 
Malawi walifuata siasa gani ? Au nao walikuwa wajamaa....tutajie nchi za africa ambazo azikufuata ujamaa tuona zilivyo na uchumi wa kitajiri kama nchi za asia ...ili tuone kama wewe unayo akili kichwani
 
Kweli mwandishi lazima atakuwa na umri mdogo lakini hili si kosa. Ukitaka kumhukumu Nyerere lazima umhukumu kwa vigezo vya wakati husika na siyo vigezo vya sasa. Wenzio tuliomfahamu Nyerere alikuwa ni mtu msomi, msikivu na mtafiti wa ukweli. Kama wewe unadhani hakukuwa na demokrasia wakati wa chama kimoja basi wewe hujasoma historia ya bunge la wakati huo ukalinganisha na Bunge la leo. Kuhusu maendeleo ya Tanzania pia unatakiwa ujue tulipopata uhuru maendeleo ya Tanganyika yalikuwa wapi na wasomi wangapi. Nyerere alimteua Prof Justian Rweyemamu, Mchumi nguli wa wakati huo lakini waliompiga vita hakuwa Nyerere ila establshment. Wengi walikuwa hawamwelewi. Akaletwa Prof Mbilinyi ambaye impact yake ilikuwa ndogo. Sasa kama una Tanzania iko nyuma unailinganisha na nchi ipi? Kenya? Uganda, DRC au Malawi? Wengi mnapenda kuona Kenya kama imeendelea lakini umewahi kaa Kenya ukaona maisha halisi yalivyo? Kwa wakati ule niliwahi kusikia comment moja ambayo pengine ina ukweli kwamba nchi ye yote ambayo ingefuata sera za Tanzania ikatumia uongozi wa Kenya wa wakati ule kutekeleza sera hiyo, ingeendelea vizuri hapa Afrika! Fikiri!
 
Umesahau kuwa elimu ilikuwa bure mpaka chuo kikuu, huduma za afya zilipatikana bure nchi nzima, viwanda vingi vilijengwa na ajira kwa wasomi zilikuwa za kutosha nk.
 
Na anakaribia kuwa mtakatifu, hakika kama mkatoliki nimekwazika sana tena mno.....dah.
 
Nchi Ina bahati mbaya kupata viongozi vichaa, type ya sokoine na magufuli, wameua biashara nyingi za wazawa,

Nyerere na sera zake ujamaa primitive alishindwa uchumi,
Zile sera zingewezekana nchi tajiri
Hii imepelekea kudidiza wazawa na kuwainua wageni- wahindi

Nyerere na kawawa sera yao ilikuwa kuua uchumi na ustawi wa mikoa ilivyokuwa mbele kwenye Early 60s Ili wote Wawa maskini watawalike kirahisi

Kambona alimshangaa sana nyerere na sera zake za kijima akaamua kusepa zake uhamishoni,
 
Mkuu unaandika facts tupu
Mtakatifu waingereza walimwachia Dola za kutosha, yeye akazitapanya na harakati zake za kusini mwa afrika

akashindwa kuelewa kuwa kwenye uchumi ukitumia Dola 1 nabidi uzalishe Dola 2 kufika 1975 Hela ikaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…