Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Kiasili Tanzania ni nchi ya kilimo, uvuvi na ufugaji. Hata bila madini hii nchi badi ingepiga hatua nzuri. Wajamaa waliharibu shughuli za kilimo kwa kuleta siasa. Hakuna zao la biashara serikali iweke mkono halafu lisiharibike. Hizo siasa za madini unazozileta hapa sizifahamu, hivyo endelea kukaa nazo.​
 
Na ndivyo tulivyokuwa tukifanya kwa miaka yote ya utawala wa Nyerere hakukuwa na madini wala Gesi Bali KILIMO tu ndicho kilichokua chanzo cha mapato ya wananchi na Serikali pia!
Kuanzia mapato ya fedha za kigeni mpaka chakula na mambo mengine yote !!
Wakaja wajuaji na Azimio lao la Zanzibar wakatupilia mbali slogan yetu tuliyokuwa tukiitumia enzi hizo -:
KILIMO NDIO UTI WA MGONGO WA NCHI YETU !!
N.B sisi tulikuwepo wengine wahakuwepo bali wanaendelea kulishwa matango pori ! 😅🙏🙏
 
So kenya ni Benchmark?
 
My point ni kuingiza mambo ya utakatifu wa Nyerere ktk andiko lako. Nafkiri ilitosha ku criticise bila kuingiza mambo ya utakatifu wake. Nyerere ni binadamu mwenye sifa ya kukosea, ingawa ktk Marais tulionao namuona yeye kakosea less kuliko wenzake. Kitu ambacho huwa naanza nacho ktk kujadili utendaji wa mtu ni dhamiri. Yeye Nyerere alikosea sana na amekiri mara kadhaa kukosea, na wote tunakua jinsi ubepari ulivyo tukalia kooni na masharti mengi magumu ya kidunia kwa wakati ule lakini ukweli usemwe dhamiri yake ilikuwa safi ktk uongozi na ktk kujiletea maendeleo.
 
So kenya ni Benchmark?
Hapa Africa mashariki na kati huwa naona nchi Bora kijamii ni Tanzania tu. Wengi wanaisifia Kenya na Rwanda lakini huwa nazionaga hizo nchi ni kama house of cards...any time zinaporomoka kwa kuwa jamii yake iko na high grievances and disparities
 
Ni maswali mazuri sana na ningehitaji nafasi kubwa kukujibu. Maono ya Mtei kama Gavana wa BOT peke yake hayangeweza kuikomboa Tanzania kiuchumi. Ili Uchumi ukue haihitaji pesa peke yake. Kama ingekuwa hivyo, nchi ambazo zilifuata masharti ya Benki ya Dunia hapa Afrika mbona hazina tofauti na Tanzania kimaendeleo. Ndiyo maana nilikupa mfano wa Malawi au Kenya.
Muundo na utawala wa China ni wa karne nyingi huwezi kulinganisha na Tanzania. Tekn olojia na Uongozi wa China una uzoefu wa karne nyingi ambao hata Wamerikani wanaofikiri sasa ndiyo wanatambua na wanauhofia. China hata baada ya Nyerere kuondoka walikuja kuishauri Tanzania namna ya kubinafsisha mashirika ya umma kwa faida lakini uongozi wa Tanzania katika ujumla wake hawakuwa na upeo hata kumwekewa Mchina anachoshauri!
Huyo Nyerere ndiye alitushangaa kuwa hata Marekani inajua umuhimu wa China kwa uchumi wa miaka ijayo lakini Tanzania ambayo ina urafiki wa jadi na China imezubaa!
Ningependa kurudia ushauri wangu kuwa usimhukumu Nyerere kuhusu Tanzania kwa vigezo vya sasa. Ungemsikiliza Kissinger,akiwa US Secretary of State, alichosema baada ya kukutana na Nyerere Kilimanjaro Hotel miaka hiyo, ungekuwa na heshina kidogo ya uwezo wa Nyerere kujua dunia inavyoendeshwa na nchi zetu zinatakiwa zifanye nini. Nyerere alikuwa kama Socrates alikuwa mbele mno kimawazo lakini Watanzania tulikuwa hatujaiva ingawa alijitahidi kutuelimisha tuweze kufikiri. Sasa tumerudi nyuma hata kufikiri imekuwa shidaa! Soma hotuba za viongozi wa leo na maono yao ya maendeleo ndipo utagundua toafauti!
 
Pia hiyo suluhu ya Waziri Mkuu Ahmed Salim ya kuruhusu mitumba ndiyo ambayo leo inatufanya tushindwe kufufua viwanda vyetu vya nguo hapa Tanzania ingawa ni wakulima wa pamba!
Masharti ya SAP ndiyo Nyerere alikataa kwa hoja na yalipobadilishwa Tanzania ilikubali SAP. Kulikuwa na majadiliano. Zamani ukitaka ajira World Bank ilikuwa huwezi kupita kwenye usaili bila kujifunza hoja na mtazamo wa Nyerere kwenye maendeleo ya nchi chnga! Mpaka kesho Mataifa ya Magharibi hayamtaki kiingozi ye yote anayezungumzia hoja za kujitegemea kwenye uchumi.
 
Kabisa. !
 
Kabisa ,
 
Ndugu yangu, niwe mdogo kiasi cha kutoelewa kwamba leo nyumbani hakuna chakula ?
Au kuambiwa na wazazi tufiche kila kitu kwenye zizi la ng'ombe na tusiwaambie majirani chochote hata wakituuliza.
Hiv unajadili na huyu mwehu!!!!!!ucpoteze muda wako bure jitu lenyew ni magonjwa!!!!hajawahi na hatowahi kuwa na akili.
 
Napata tabu sana kuelewa kwa vipi unahitimisha kuwa Nyerere hakua na huruma kwa kigezo tu cha mapungufu ya mfumo wa kiuchumi wa enzi zake.

Ni kweli usio na shaka kuwa kulikuwa na matokeo hasi ya mfumo wa ujamaa kwa falsafa za Nyerere—Nyerereism, kama ambavyo pia kulikuwa na matokeo chanya. Changamoto kubwa sana ya nchi huru ni migawanyiko ya kikabila, kikanda na kimbari(race); sioni namna gani uchumi wa kibepari na Demokrasia ya vyama vingi ingejenga Taifa moja kama lilivyo leo—Rejea visa vya kina Christopher Kassangatumbo na kuundwa kwa Preventive Detention Act; Vuguvugu la Afrikanaizesheni; Rejea kura tatu 1958; Rejea Vuguvugu la waislam dhidi ya Nyerere enzi za TAA/TANU n.k! Bila Nyerereism; leo ni wachagga, Wahaya na Wanyakyusa ndio wangekuwa makabila hodhi ya kila kitu nchi hii; Ni wakristo ndio wangekuwa tabaka tawala nchi hii.

Nyerere huyu ametoka madarakani akiwa 'lofa' kabisa, contrary to watu kama Mobutu, Dos Santos n.k. Unawezaje muita Katili? Huo ukatili ameufanya kwa manufaa yapi? Tuseme kuwa sera zake zilipata zilifeli, lakini kumuita asiye na huruma ni kutotazama mambo kwa picha pana.

Sijui kwanini Liberalist mnapenda sana kumpoint kuwa Mao ameua mamilioni ya watu as if aliwaweka kwenye concentration camps na kuwaua. Hebu, mtoa mada nijibu haya; Dunia hii kuna mfumo umeua watu mamilioni kuliko ubepari?—Vita zote mbili za dunia ni ubepari, zimeua watu milioni ngapi? 50+ Milion. Ukoloni ni matokeo ya Ubepari, Ukoloni wa mzungu umeua waafrika wangapi? 10+Mil, Ubepari huu uliotumia watumwa uliua watu Milioni ngapi kwenda kujenga ubepari? About 60 Mil. Uchafuzi wa Mazingira kutokana na viwanda vya kibepari vimeua watu Mil ngapi? 7 Mil kila mwaka. Ubepari huu umechochea migogoro iliyoua watu Milioni ngapi? Leo huo ubepari unaua watu wangapi huko Mashariki ya kati? Karibu 5 Mil. Ukizungumzia Sera za kiuaji, hakuna sera UAJI kuliko za KILIBERALI/UBEPARI.
 
Mpaka kesho Mataifa ya Magharibi hayamtaki kiingozi ye yote anayezungumzia hoja za kujitegemea kwenye uchumi.
Tatizo la mtoa mada, anapresent hoja ya Sera za SAP kana kwamba zilikuwa ni sera zenye lengo la kutokomboa na kufanya tuwe nchi ya maziwa na asali ilihali zilikuwa ni sera za kutufanya tuingie kwenye mfumo wa ukoloni wa uchumi wa Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…