Magonjwa Mtambuka
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 32,246
- 31,176
Hata ukiandika kwa kizungu haitobadilisha kitu; unanisikia wewe kijana?😎Very kiddish.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata ukiandika kwa kizungu haitobadilisha kitu; unanisikia wewe kijana?😎Very kiddish.
Nyerere alikataa kuingia mikataba na makampuni ya kuchimba madini kwa sababu walikuwa wanatoa asilimia ndogo sana kwa Serikali !
Hapo ni kweli Nyerere squandered the opportunity !
Then wakaja wanaojua how to use apportunities wakaingia mikataba ya madini kwa spidi ya 5G kwa kusaidiwa kupewa 3% kama mgao wa faida kwa Serikali !!
Kweli Nyerere squandered apportunities !
Na Gesi nayo wenye kujua how to do with apportunities wakaingia mikataba chapchap !
Mwamba akaja akatuambia TUMEPIGWA 😱😱 !!
Kweli Nyerere alituchelewesha sana !!
Na ndivyo tulivyokuwa tukifanya kwa miaka yote ya utawala wa Nyerere hakukuwa na madini wala Gesi Bali KILIMO tu ndicho kilichokua chanzo cha mapato ya wananchi na Serikali pia!Kiasili Tanzania ni nchi ya kilimo, uvuvi na ufugaji. Hata bila madini hii nchi badi ingepiga hatua nzuri. Wajamaa waliharibu shughuli za kilimo kwa kuleta siasa. Hakuna zao la biashara serikali iweke mkono halafu lisiharibike. Hizo siasa za madini unazozileta hapa sizifahamu, hivyo endelea kukaa nazo.
Hao ndio mabingwa wa ujingaWee chalii akili huna sasa uongozi na masuala ya dini yana uhusiano gani ? Pumbavu
So kenya ni Benchmark?Kusafiri kwenda majuu miaka fulani kukata ticket mpaka kibali kutoka kwa governor wa BOT.
Huwa nikipita page ya uhamiaji ya Kenya naona wenzetu walivyo mbali kwa exposure.
Mimi kwa nchi nilizotembelea hadi leo niseme ukweli tusidanganyane uzalendo ni kubaki nyumbani mtu aliyesafiri sana sehemu tofauti anacho kitu cha tofauti kuliko yule aliyekaa sehemu moja tu.
Wanaoitwa wazalendo kwa kubaki nyumbani ndio wanaiba mabilioni huku wakitembelea gari za milioni 400 na full kiyoyozi ndani mmewapa walinzi na mnawaita waheshimiwa.
Ninaamini bila uwepo wa diaspora kwa wingi Kenya wasingepata katiba mpya 2010 ambayo ilikuja na mabadiliko mengi ikiwemo uraia pacha na hata hata diaspora kwa kuruhusiwa kupiga kura.
Hadi leo ninauchukia ujamaa maana ni umasikini , masikini ni wengi na ndio mtaji wa CCM maana ukishakuwa masikini utahitaji tu uhakikishiwe chakula na kesho ila sio miaka 10 ijayo hawa ndio mtaji wa chama chakavu.
My point ni kuingiza mambo ya utakatifu wa Nyerere ktk andiko lako. Nafkiri ilitosha ku criticise bila kuingiza mambo ya utakatifu wake. Nyerere ni binadamu mwenye sifa ya kukosea, ingawa ktk Marais tulionao namuona yeye kakosea less kuliko wenzake. Kitu ambacho huwa naanza nacho ktk kujadili utendaji wa mtu ni dhamiri. Yeye Nyerere alikosea sana na amekiri mara kadhaa kukosea, na wote tunakua jinsi ubepari ulivyo tukalia kooni na masharti mengi magumu ya kidunia kwa wakati ule lakini ukweli usemwe dhamiri yake ilikuwa safi ktk uongozi na ktk kujiletea maendeleo.Objectivity/Upembuzi yakinifu ni kuweza kuchambua sifa za kitu na kuziangalia, kuzitaja na kuzielezea kama zilivyo bila kuingiza misimamo binafsi (Personal Inclination/Ideology). Mzee Nyerere alikuwa na mazuri yake ambayo yanaimbwa, lakini alikuwa na mabaya yake ambayo yalifichwa na wengi hawapendi kuyaongelea kwasababu wanalinda heshima yake. Ukweli mchungu ni kwamba watanzania wengi hawawezi kufanya upembuzi yakinifu ndiyo maana ni ngumu kubadilika na kujifunza kutokana na makosa.
Mzee Nyerere alikuwa na nafasi ya kufanya makubwa kuliko Raisi yoyote hapa Afrika, lakini sera zake za uchumi ambazo ndizo zinaendesha kila kitu zilifeli vibaya mno kwasababu hakupenda kusikiliza ushauri na hakusoma vizuri majira na nyakati. Ujamaa ni sera ambayo tuliige Uchina na Urusi. Ujamaa ulifeli na kusababisha madhara huko Uchina na Urusi tulikouiga japo walau wenzetu walifanikiwa kwenye baadhi ya mambo. Mataifa mengi ya kijamaa yalianza kudidimia miaka ya 70's baada ya mtikisiko wa uchumi wa dunia. (Hapa sipo objective kivipi ?)
Uchina sera za Mao kama The Great Leap Forward na The Cultural Revolution zilisababisha madhara makubwa, na kuacha mamilioni ya wachina wakiwa wamekufa. Baada ya Mao kufariki wachina wakiongozwa na Deng Xiaoping wakaanza kufanya mabadiliko kwenye mfumo mzima ili kusaidia watu. Ikumbukwe kwamba mabadiliko ambayo Uchina iliyafanya miaka ya 70's chini ya Dend Xiaoping yalipendekezwa kufanywa miaka ya 60's lakini Mao na wenzake wakawafunga gerezani wakina Deng Xiaoping na kumuua Liu Shaoqi ambaye aliratibu maendeleo hayo.
Alichokifanya Mao nchini Uchina hakina tofauti na alichokifanya Mzee Nyerere nchini Tanzania. Wote walishauriwa kwamba wafanya mabadiliko miaka ya 60's lakini wakakataa. Mao aliwafunga waliomshauri afanya mabadiliko na kuwaita mabeberu hata wengine kuuawawa. Mzee Nyerere naye ndiyo aliyefanya hivyo hivyo, wakina Mtei na kina Rweyemamu hawakusikilizwa na wakaonekana kama ni vibaraka fulani hivi. Uchina bahati nzuri Mao aliondoka mapema na wakaanza kufanya mabadiliko kwa kasi na kuruhusu mfumo wa masoko.
Tanzania watu walikuwa wanahangaika lakini Mzee Nyerere aliendelea kukomaa. Hili nalo nikilesema mnashindwa kulimeza halafu mnaanza kunifundisha kuhusu OBJECTIVITY. Mzee Nyerere hakuwa na ufahamu mzuri kwenye uchumi wa masoko huu ndiyo ukweli. Hata Deng Xiaoping wa Uchina alikuwa hana huo ufahamu, hivyo akaamua kwenda Singapore kufundishwa na Waziri Mkuu Deng Xiaoping. Wasomi wa Uchina walifundishwa na wasomi wa Singapore kuendesha nchi. Huu ndiyo ukweli. Sasa mkiendelea kulazimisha kwamba Mzee Nyerere alikuwa ni malaika anayejua kila kitu ilhali wenzake kama Deng Xiaoping walikubali kufundishika, napata ukakasi mno na namna mnaitizama hii dunia.
USSR nako ilikuwa hivyo-hivyo, Andropov aliona kabisa Ujamaa unahitaji mabadiliko na akakiri mwaka 1982 mbele ya mkutano mkuu wa chama kwamba kama Urusi inataka kufanikiwa ni lazima ibadilike. Bahati mbaya alikaa madarakani miaka miwili tu, na hakufanikiwa kutekeleza aliyotaka kuyafanya. Sasa watu ambao Ujamaa mmeiga kwao wanakubali kubadilika kwasababu mfumo wa Ujamaa was not sustainable, nyie ambao mmeletewa mlikuwa mnakataa nini ?
Tunauliza Mzee Nyerere alifahamu kabisa kwamba nchi haina fedha za kigeni, lakini kwanini aliendelea kukomaa ?
Hivi unadhani Mao Zedong mbali na kukosea kwenye Uchumi, unadhani sehemu nyingine muhimu hakupatia?
===============================================================================
Mwisho kabisa, UCHUMI ndiyo moyo wa taifa lolote lile. Ukikosea UCHUMI hata uwe na jeshi imara na taifa lenye wazalendo mambo lazima yaharibike tu. Urusi alipatia mengine, alipokosea Uchumi tu ikala kwake. Uchina anakosea mengi sana, kisiasa bado lile ni taifa la kidikteta lakini wamepatia sana UCHUMI. Watu wanahitaji sana maendeleo kuliko porojo za kisiasa za demokrasia au utawala bora. Ndiyo maana mataifa kama Saudi Arabia, UAE na Qatar hayahangaiki kabisa na hizo porojo kwasababu wanafahamu fika ukishawapa watu maendeleo maneno hupungua.
Sasa nikuombe unisaidie labda kuna kitu ambacho wewe unakifahamu, mimi sikifahamu naweza kujifunza:
1. Unadhani Mzee Nyerere alifanikiwa kwenye Uchumi? (Kama jibu ni NDIYO nieleze alifanikiwa kivipi ?)
2. Nini kilipelekea matatizo ya uchumi nchini Tanzania kuanzia miaka ya 1975-1985 ?
3. Unadhani Tanzania ingeendelea kufanikiwa kwa kukomaa na mfumo wa Kijamaa?
4. Kwanini miaka ya 1980-1985 ilikuwa imejaa changamoto kubwa za kiusalama kuliko wakati wowote ule ?
5. Kwanini sera alizozikataa miaka ya 1970's alikuja kuzikubali miaka ya 1984 wakati anaondoka madarakani?
Hapa Africa mashariki na kati huwa naona nchi Bora kijamii ni Tanzania tu. Wengi wanaisifia Kenya na Rwanda lakini huwa nazionaga hizo nchi ni kama house of cards...any time zinaporomoka kwa kuwa jamii yake iko na high grievances and disparitiesSo kenya ni Benchmark?
Ni maswali mazuri sana na ningehitaji nafasi kubwa kukujibu. Maono ya Mtei kama Gavana wa BOT peke yake hayangeweza kuikomboa Tanzania kiuchumi. Ili Uchumi ukue haihitaji pesa peke yake. Kama ingekuwa hivyo, nchi ambazo zilifuata masharti ya Benki ya Dunia hapa Afrika mbona hazina tofauti na Tanzania kimaendeleo. Ndiyo maana nilikupa mfano wa Malawi au Kenya.Nakuelewa lakini wewe ambaye ni Mkubwa naomba unisaidie kutoa haya majawabu.
Mosi, Mzee Nyerere na Mzee Mtei walipishani kwasababu gani. Je, mambo aliyoshauri Mtei yalikuwa mabaya hadi Nyerere kuamua kumfanyia vile? Hivi Unadhani Mzee Nyerere angekubali kufanya mabadiliko miaka ya 70's unadhani nchi ingepitia kipindi kigumu kama kile cha miaka ya 80's?
Pili, nchi ilianza kudorora uchumi tokea mwaka 1980, kwanini Mzee Nyerere hakutaka kuchukua hatua zozote zile kusaidia wananchi waliokuwa kwenye lindi kubwa la umasikini, mpaka kusubiri mwaka 1984 baada ya Mzee Dr Salim kufanya ziara kule Lindi na kumwambia Mzee Nyerere kwamba hali ilikuwa ni mbaya. Kwanini miaka yote hii alikuwa hawaonei huruma watanzania?
Tatu, kwanini Mzee Nyerere alikuja kuzikubali sera zote alizozikataa (Japo siyo vigezo vyote vya SAP vilikuwa vinatekelezeka), alizisaini mwaka 1984 na zikaanza kutekelezwa na Mzee Mwinyi. Kama sera zilikuwa ni mbaya kihivyo kwanini alizikubali baadaye ?
Nne, mbona Uchina alikioga mfumo wa Ujamaa walifanya mabadiliko mapema miaka ya 70's na hawakupata matatizo yoyote, zaidi zaidi walifanikiwa mno. Tanzania tulikuwa na uziada upi wa kuchelewesha mabadiliko kwa muda mrefu ilhali wananchi wakiwa wanapitia mateso?
Lengo lake haswa lilikuwa ni nini ?
Pia hiyo suluhu ya Waziri Mkuu Ahmed Salim ya kuruhusu mitumba ndiyo ambayo leo inatufanya tushindwe kufufua viwanda vyetu vya nguo hapa Tanzania ingawa ni wakulima wa pamba!Nakuelewa lakini wewe ambaye ni Mkubwa naomba unisaidie kutoa haya majawabu.
Mosi, Mzee Nyerere na Mzee Mtei walipishani kwasababu gani. Je, mambo aliyoshauri Mtei yalikuwa mabaya hadi Nyerere kuamua kumfanyia vile? Hivi Unadhani Mzee Nyerere angekubali kufanya mabadiliko miaka ya 70's unadhani nchi ingepitia kipindi kigumu kama kile cha miaka ya 80's?
Pili, nchi ilianza kudorora uchumi tokea mwaka 1980, kwanini Mzee Nyerere hakutaka kuchukua hatua zozote zile kusaidia wananchi waliokuwa kwenye lindi kubwa la umasikini, mpaka kusubiri mwaka 1984 baada ya Mzee Dr Salim kufanya ziara kule Lindi na kumwambia Mzee Nyerere kwamba hali ilikuwa ni mbaya. Kwanini miaka yote hii alikuwa hawaonei huruma watanzania?
Tatu, kwanini Mzee Nyerere alikuja kuzikubali sera zote alizozikataa (Japo siyo vigezo vyote vya SAP vilikuwa vinatekelezeka), alizisaini mwaka 1984 na zikaanza kutekelezwa na Mzee Mwinyi. Kama sera zilikuwa ni mbaya kihivyo kwanini alizikubali baadaye ?
Nne, mbona Uchina alikioga mfumo wa Ujamaa walifanya mabadiliko mapema miaka ya 70's na hawakupata matatizo yoyote, zaidi zaidi walifanikiwa mno. Tanzania tulikuwa na uziada upi wa kuchelewesha mabadiliko kwa muda mrefu ilhali wananchi wakiwa wanapitia mateso?
Lengo lake haswa lilikuwa ni nini ?
Kabisa. !My point ni kuingiza mambo ya utakatifu wa Nyerere ktk andiko lako. Nafkiri ilitosha ku criticise bila kuingiza mambo ya utakatifu wake. Nyerere ni binadamu mwenye sifa ya kukosea, ingawa ktk Marais tulionao namuona yeye kakosea less kuliko wenzake. Kitu ambacho huwa naanza nacho ktk kujadili utendaji wa mtu ni dhamiri. Yeye Nyerere alikosea sana na amekiri mara kadhaa kukosea, na wote tunakua jinsi ubepari ulivyo tukalia kooni na masharti mengi magumu ya kidunia kwa wakati ule lakini ukweli usemwe dhamiri yake ilikuwa safi ktk uongozi na ktk kujiletea maendeleo.
Kabisa ,Pia hiyo suluhu ya Waziri Mkuu Ahmed Salim ya kuruhusu mitumba ndiyo ambayo leo inatufanya tushindwe kufufua viwanda vyetu vya nguo hapa Tanzania ingawa ni wakulima wa pamba!
Masharti ya SAP ndiyo Nyerere alikataa kwa hoja na yalipobadilishwa Tanzania ilikubali SAP. Kulikuwa na majadiliano. Zamani ukitaka ajira World Bank ilikuwa huwezi kupita kwenye usaili bila kujifunza hoja na mtazamo wa Nyerere kwenye maendeleo ya nchi chnga! Mpaka kesho Mataifa ya Magharibi hayamtaki kiingozi ye yote anayezungumzia hoja za kujitegemea kwenye uchumi.
Tulia ww wanaume wanapojadili mambo muhimuMbona uongo mwingi?🙂
Binuka nikubamize.Tulia ww wanaume wanapojadili mambo muhimu
Hiv unajadili na huyu mwehu!!!!!!ucpoteze muda wako bure jitu lenyew ni magonjwa!!!!hajawahi na hatowahi kuwa na akili.Ndugu yangu, niwe mdogo kiasi cha kutoelewa kwamba leo nyumbani hakuna chakula ?
Au kuambiwa na wazazi tufiche kila kitu kwenye zizi la ng'ombe na tusiwaambie majirani chochote hata wakituuliza.
Hakika ujinga wa uzeeni lazima utakufa nao tu pole sanaUtu uzima dawa[emoji41]
Kuliko yule aliyeng'ang'ania zaid ya miaka 20???Mimi kinachonishangaza ni huyu wa sasa ambaye hana uwezo lakini bado tu anangangania.
Nan huyo????Ndiye Rais pekee aliyejitambua na kuthamini kila binadamu na kumpa thamani yake
View attachment 2852299
Tatizo la mtoa mada, anapresent hoja ya Sera za SAP kana kwamba zilikuwa ni sera zenye lengo la kutokomboa na kufanya tuwe nchi ya maziwa na asali ilihali zilikuwa ni sera za kutufanya tuingie kwenye mfumo wa ukoloni wa uchumi wa Marekani.Mpaka kesho Mataifa ya Magharibi hayamtaki kiingozi ye yote anayezungumzia hoja za kujitegemea kwenye uchumi.
Binuka nikubamize.Hakika ujinga wa uzeeni lazima utakufa nao tu pole sana