Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Hulka ya Baba wa taifa ilikuwa ya ujuaji zaidi, ndio maana walimuita "Bwana haambiliki"hii ililetwa na tabia yake ya kuto sikiliza ushauri wa mtu,bali maono yake tu,kinyume na hapo ni tatizo kubwa sana.Mpaka kufikia hatua ya watu kuwekwa vizuizini na wengine kukimbia taifa hali ilikuwa mbaya sana.
 
Kule kwnye history

Point zilikuwa kama ifuatavyo

Poor science and technology in simplifying the process of renewals

ideological from other leaders


imitate without being sure in the revolution so that we destroy the confusion

Nyerere's knowledge in everything...here he saw himself as knowing everything in the country, even his advisors were considered fools

Wazee wa history mnirekebishe



Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Sawa kabisa ila hii ni history lazima ipewe hakiyake watu wajue nini kilikuwa kinaendelea ilikuwa kama Misukule watanzania suruali viraka viatu matairi ya gari. Hakika inasikitisha..
Ukiwaambia watu hili, wengi wanaweza wasiamini. Nguo za viraka, makobaz, kupanga mstari kununua sukari, halafu hapo bado bwana Moringe hajakusweka ndani kisa tuhuma za uhujumu uchumi. Kuna baadhi ya mambo tulikosewa na kunyanyaswa mno sisi watanzania. Hivi hadi chakula uende ukaombe kwa Mwenyekiti kweli ?​
 
Ndio maana tuko hapa tulipo.....Nyerere alijali san Tanu kuliko Tanzania
 
Nyerere aliondoka madarakani mwaka 1985 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 24 wakati wa vita baridi. Leo hii ni miaka zaidi ya 38 tangu aondoke madarakani, na vita baridi ilikufa takriban miaka 32 iliyopita. Dunia imebadilika sana baada ya vita baridi kuisha na ukuaji wa information technology. Kwa nini una interest na revisionisim ya mambo ambayo siyo relevant ten katika dunia ya leo?
 
Mkuu wanaokumbuka adha hiyo ni wachache, na hao ni wale walioishi na kukulia mijini na hasa jiji la Dar es salaam.
Wengi wenye umri kama wako wakati huo walikuwa shule vijijini, ambako vyakula walikuwa wanalima wenyewe.
Na vitu kama dawa ya meno, siagi, sabuni, sukari, kandambili nk kwenye maeneo ya vijijini vilikuwa ni anasa tu. Hawakuhisi adha ya kukosekana kwake.
Vinginevyo wangekuelewa unasema nini.

Binafsi sijasahau mateso niliyopitia nikiwa mvulana mdogo kufuatilia gari ya ugawaji kwenye mitaa niliyoishi.
Kwenye foleni ya kupata bidhaa adimu na muhimu tulikuwa tunapanga mawe kusubiri gari.
Haya yalisababishwa na sera mbaya za ujamaa na utekelezaji wake kupitia Azimio la Arusha.
 
Nyerere alikuwa ni mtu mwenye utu,kipindi cha msiba wake Maalim Seif alinukuliwa akisema Mwl alikuwa ni mkweli.Sasa jiulize yule mliyekuwa mnamuona alionewa na mwl anasema alikua mkweli which means ni kama ali-REGRET kuhusu ugomvi wao.Kushindwa kwa ujamaa dhidi ya ubepari ni sawa na kushindwa kwa utu dhidi ya unyama na kuonesha kwamba hakukubaliana na ubepari aling'atuka ili asiingize nchi matatizoni kwa shinikizo la wenye makucha(aliipenda nchi yake)kipi cha ajabu cha sasa hivi ukiachana teknolojia ambayo ni lazima tucheze nayo?
 
Sikuwepo duniani kipindi cha Nyerere,lakini kupitia maandiko mbalimbali unaweza kuona utawala ule ulikua na ahueni kwa wananchi licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza.waliokuwepo enzi hizo wanasema hakukua na mgao wa umeme,elimu ilikua bora zaidi,huduma mbalimbali za kijamii pamoja na kwamba zilikua chache lakini zilitolewa kwa wakati na bila upendeleo wowote na tena kwa kiwango cha juu, utu wa Mtanzania ulikua ni kipaumbele cha serikali, serikali iliwajibika kisawasawa.je tujiulize miaka 38 sasa tangu Nyerere atoke madarakani zaidi ya kuongezeka majengo marefu kwenye miji mikubwa kama Dar nini cha maana serikali zilizopita zimefanya ambacho hakikufanywa na serikali ile ya Nyerere?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…