Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu usijifiche kwenye chaka la utu uzima, pinga hoja kwa kuweka facts za kiutu uzima. Tiririka ukweli wako hapa!Inaonekana kabisa enzi za Mwalimu ulikuwa mtoto mdogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu usijifiche kwenye chaka la utu uzima, pinga hoja kwa kuweka facts za kiutu uzima. Tiririka ukweli wako hapa!Inaonekana kabisa enzi za Mwalimu ulikuwa mtoto mdogo.
Mkuu kuhusu hoja namba 1 kamuulize ndugu Amir Jamal na ndugu Bernard Membe upate ukweli na kuweka rekodi yako sawa sawa!Mtoa mada nadhani unakosea kwa kusema Nyerere hakuwa na huruma hata kidogo. Umechambua upande wa udhaifu wake ndio maana unaona hakua na huruma hata kidogo.
Chambua na upande wa mazuri yake ndipo utaiona huruma ya Nyerere kwa wananchi wake.
1. Nyerere kwa kipindi alichoongoza alikua na nafasi ya kuiba mali za umma na kujilimbikizia kadri atakavyo na asingekuwepo wa kumpigia kelele lakini hakufanya hivyo.
2. Mwl. J.K. Nyerere angetaka kutoa madaraka makubwa kwa watoto wake angefanya hivyo lakini mpaka sasa nadhani Makongoro Nyerere ndio kakumbukwa juzi hapa kuwa Mkuu wa Mkoa angalia hao wengine wanavyowapaisha watoto wao.
Inakua rahisi kumchambua udhaifu wake kwa kuwa kimepita kipindi kirefu inakua rahisi kuona makosa yake.
Kumbuka:
3. Mwl. Nyerere alitoka madarakani Nchi ikiwa na viwanda vingi sana lakini kutokana na ubinafsi na Ubepari leo hii viwanda karibu vyote vimeuzwa na kutelekezwa matokeo yake ajira nyingi sana zimepotea.
4.Harakati za kuunganisha Nchi unaweza kuzichukulia rahisi kwa kuwa unaona matokeo tu lakini mchakato wake sio wa kubeza. Pale ilifanyika kazi kubwa sana kuwaungansha watanzania na kuondoa ukabila na udini.
5. Nadhani nia ya Mwl.ilikua nzuri sana ila matokeo ndio hayakua mazuri.
Kitu kingine matokeo ya vita ya Kagera kwa uchumi wetu ilileta athari kubwa sana.
Vile vile Mwl.alijihusisha sana na ukombozi wa Nchi nyingine za Afrika. Hivyo alikua na mambo mengi sana ya kupigania katika lindi la ufukara wa Taifa.
Tujiulize
Miaka 38 tangu Mwl. Nyerere atoke madarakani ni eneo gani kama Taifa tunalifanya kwa ufanisi ndani ya Ubepari.
Nadhani sekta ya uchawa tu ndio tuko njema zaidi.
Mwl.apewe heshima yake
Mkuu hali ilikuwa mbaya mno. Ukiona mikono inayobariki mashoga sasa hivi inatumika kumfanya Nyerere Mtakatifu, ujue kuna jambo la Kimaslahi zaidi ya kiimani!Ukiwaambia watu hili, wengi wanaweza wasiamini. Nguo za viraka, makobaz, kupanga mstari kununua sukari, halafu hapo bado bwana Moringe hajakusweka ndani kisa tuhuma za uhujumu uchumi. Kuna baadhi ya mambo tulikosewa na kunyanyaswa mno sisi watanzania. Hivi hadi chakula uende ukaombe kwa Mwenyekiti kweli ?
Mkuu huwezi ukawa na msingi wa mabua halafu ukategemea ghorofa imara! Chanzo cha haya yote ni Nyerere!Jibu langu ni moja tu tangu tumejitawala mpaka hivi leo ni wapi tulipofanikiwa. Licha ya Nyerere, tueleze mafanikio tuliyopata kutoka kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hivi sasa kwa SSH
🙏Si kwamba huna muda wa kubishana, kwenye mada hii huna unachojua.
Hukuwepo wala kuona athari za ujamaa.
Unachojua ni historia za vitabuni tu ambazo nyingi zimepotoshwa.
Utu uzima dawa😎Mkuu usijifiche kwenye chaka la utu uzima,..
Mkuu kweli unaweza kuhisi maumivu halisi na mabichi kama waliyopitia watu kipindi cha Azimio la Arusha la 1967, operation vijiji ya 1973, njaa ya 1974, vita ya Kagera ya 1979 na kadhalika kwa kusoma kitabu???Sikuwepo duniani kipindi cha Nyerere,lakini kupitia maandiko mbalimbali unaweza kuona utawala ule ulikua na ahueni kwa wananchi licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza.waliokuwepo enzi hizo wanasema hakukua na mgao wa umeme,elimu ilikua bora zaidi,huduma mbalimbali za kijamii pamoja na kwamba zilikua chache lakini zilitolewa kwa wakati na bila upendeleo wowote na tena kwa kiwango cha juu, utu wa Mtanzania ulikua ni kipaumbele cha serikali, serikali iliwajibika kisawasawa.je tujiulize miaka 38 sasa tangu Nyerere atoke madarakani zaidi ya kuongezeka majengo marefu kwenye miji mikubwa kama Dar nini cha maana serikali zilizopita zimefanya ambacho hakikufanywa na serikali ile ya Nyerere?
😃😃😃😃 hatari sana[emoji419][emoji419][emoji375]View attachment 2852061View attachment 2852062
Kumbe wabongo mnapenda kupigwa!Kwa io unaamini kwenye ujamaa, Mkuu wa mkoa anaishi sawa na mkulima wa nanjilinji?
Au unahisi Nyerere familia yake nayo ilipanga folen kwenye maduka ya ushirika? Au unadhani na Nyerere aliishi kama wakulima wa Namtumbo?
Duniani hakuna usawa, ila ni bora kwenye ubepari mana the door are opened ila kwenye ujamaa the doors are closed
Nyerere aliondoka madarakani mwaka 1985 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 24 wakati wa vita baridi. Leo hii ni miaka zaidi ya 38 tangu aondoke madarakani, na vita baridi ilikufa takriban miaka 32 iliyopita. Dunia imebadilika sana baada ya vita baridi kuisha na ukuaji wa information technology. Kwa nini una interest na revisionisim ya mambo ambayo siyo relevant ten katika dunia ya leo
Asante kwa kumbukumbu hizi. Acha na mm nizipakue na kuzihifadhi
🙏Kwa sababu msingi tayari ni mbovu nyumba haiwezi kusimama
Sikuwepo duniani kipindi cha Nyerere,lakini kupitia maandiko mbalimbali unaweza kuona utawala ule ulikua na ahueni kwa wananchi licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza.waliokuwepo enzi hizo wanasema hakukua na mgao wa umeme,elimu ilikua bora zaidi,huduma mbalimbali za kijamii pamoja na kwamba zilikua chache lakini zilitolewa kwa wakati na bila upendeleo wowote na tena kwa kiwango cha juu, utu wa Mtanzania ulikua ni kipaumbele cha serikali, serikali iliwajibika kisawasawa.je tujiulize miaka 38 sasa tangu Nyerere atoke madarakani zaidi ya kuongezeka majengo marefu kwenye miji mikubwa kama Dar nini cha maana serikali zilizopita zimefanya ambacho hakikufanywa na serikali ile ya Nyerere?
👍👏🆒Sio hapakuwa na mgao wa umeme.
Sema nchi haikuwa na umeme vijiji vingi.
Sasa kama hakuna umeme kutakuwaje na mgao wa umeme.
Ni sawa useme elimu ilikuwa bure na bora alafu wakati huo huo waliozaliwa miaka ya 60-80 wengi tupo nao na hawana elimu yoyôte.
Propaganda mbaya sana
Sera ya ujamaa na kujitegemea haikuwa mbaya kwa kiwango hicho.. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
Wakati wa uhuru,umoja ulihitajika kuliko chochote.2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
Watu binafsi kina ani waliokuwa na uwezo huo?3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
Huu ni uwongo.4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
Uhuru wa mawazo, kivipi wakati hakukuwa na magazeti Wala social network.5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.
Ujamaa umefeli miaka ya 1980's haya tangu wakati huo mmeshafanya nini nje ya mawazo ya Nyerere.
Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.
Nyerere ameachiwa Madaraka mwenyewe kwa hiari miaka 1985 huku nchi ikiwa mbichi.
Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirud
Alikuwa na vitabu vyake.Ndio maana tuko hapa tulipo.....Nyerere alijali san Tanu kuliko Tanzania
Msingi gani mbovu unazungumzia ikiwa Nyerere baada ya kuondoka madarakani, kila kitu walikipindua upside down?!Kwa sababu msingi tayari ni mbovu nyumba haiwezi kusimama
Walidanganya sana vijana wakati wanasoma kumuimba kama shujaa wakati ni kinyume chake.Kwenye hili Nyerere alikuwa ndiye bingwa. Alikuwa kila anayemkosoa anahama nchi. Ni vile tu ukweli hausemwi na bahati mbaya Nyerere katawala ktk kipindi ambacho media outlets zilikuwa hakuna.
Redio ya taifa ilikuwa inaandikiwa nn cha kusema kuhusu rais kwenye taarifa ya habari.
¶ Nyerere ndiye aliyefanya Kambona kuishi ukimbizini maisha yake yote.
¶ Nyerere ndiye aliyechana vyeti vya Tuntemeke Sanga.
¶ Nyerere ndiye aliyemfunga kifungo cha nyumbani (alimuweka kizuini) Kasangatumbo
¶ Nyerere ndiye alimuondoa kwenye urais Abdul Jumbe halafu akamuweka kizuizini hapo Kigamboni mpk umauti.
¶> Nyerere ndiye aliyetunga hili katiba bovu lililomfanya yeye kujipa umungu wa Tanzania.
Nyerere ni dikteta asiyesemwa.