Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Kiongozi lazima awe na principles zake, kusimamia kile anachokiamini mpaka mwisho, kiongozi asiye na msimamo ndie chanzo cha kuyumba kwa taifa lolote hapa duniani, leo atashika hiki atakiacha, kesho atashika kile nacho atakiacha...

Kulalamika miaka yote ya Nyerere kuwepo madarakani halafu bado hali ya maisha ya mtanzania ikaendelea kuwa mbaya, kwangu sioni kama kuna mantiki yoyote, kwasababu siku zote mabadiliko hayaji kwa usiku mmoja, ni mchakato.

Sasa ndani ya kipindi hicho cha mchakato ndicho kinamfanya kiongozi aendelee kusimamia kile anachokiamini, akiamini atafikia malengo, kama kikija kuwa na matokeo tofauti hayo ni mambo ya kibinadamu, kwamba alikosea, na ndio maana akawapisha wengine.

- Lakini unaposema Nyerere hakuwa na huruma na watu wake unakosea, alikuwa na huruma kupitiliza.

1. Hakujilimbikizia mali yoyote, licha ya madini na kila aina ya rasilimali tulizonazo.

2. Aliwahi kukaririwa akisema; "kiongozi unapita barabarani, unaona hali ya mtanzania ilivyo mbaya, unajua hili ni jukumu langu kumuondoa hapo alipo".

3. Hakuna hata mtoto wake mmoja tunayesikia amewahi kuhusishwa na wizi/ufisadi wa aina yoyote.

Mpaka hapo naamini utapata picha Nyerere alikuwa kiongozi wa aina gani, kwamba licha ya sera yake ya ujamaa kufeli, lakini dhamira ya dhati ya kumkomboa mtanzania toka kwenye lindi la umasikini alikuwa nayo tofauti na ulivyoandika.

Above all, hivi umewahi kujiuliza baada ya Nyerere kuondoka madarakani nini kilifuatia?

Kilichofuatia ndicho kile ambacho Nyerere alikipiga vita na wewe unaonekana kukifurahia, binafsi nchi hii naamini hakuna mabadiliko yoyote ya maana kiuchumi zaidi ya kuwepo pengo kubwa kati ya walio nacho na wasio nacho, hili Nyerere na Sokoine ndio walikuwa wakilipinga.

- Hii kwangu ni sawa na kusema, licha ya kumuona Nyerere alifeli, lakini hata hao waliofuatia baada yake nao wamefeli pia, hatuna cha maana cha kujivunia, mgao wa umeme, ukosefu wa maji safi na salama, wanafunzi kukosa matundu ya vyoo shuleni na madawati, mambo ni mengi...

Labda uniambie tu kwa sasa unafurahia uwepo wa unga, sabuni, mchele na mahitaji mengineyo mitaani, lakini ukweli wa mambo ni kwamba, licha ya uwepo wa vitu hivyo, bado hali ya mtanzania kiuchumi ni mbaya na ndio maana mpaka leo bado wapo ndugu zetu vijijini wakisubiri kampeni zianze, ili wagaiwe t-shirts na kofia za CCM ziwastiri.

Hivyo kwangu, kumlaumu Nyerere kwa kufeli bila ya kunionesha yule aliyefaulu hapa ndani kwetu sikuelewi, na kutumia mifano ya nje kumhukumu Nyerere bila kunionesha nani aliyefuatia wa hapa ndani akafaulu, umemuonea, that's unfair comparison.

Unless uniambie mahitaji yetu siku zote yangebaki yale yale ya unga, mchele na sabuni kupatikana madukani, jambo ambalo kwangu halina mantiki, naamini mahitaji hubadilika kulingana na wakati, na pale unaposhindwa kuwapa watu wako kile wanachohitaji kwa wakati husika, basi umefeli, there is no way out.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hata wakimtangaza kuwa ni mungu hilo halinihusu hata kidogo, ila ntakachouliza ni kwanini huyu mnayemuita mungu wenu alikuwa na moyo mgumu, wa jiwe kama Firahuni ? Alikuwa anapata faida gani kutuona sisi tunaishi vile ?
Sasa hivi tunaishi vizuri sana kwenye mahekalu yetu na tunatembelea mavieite yetu makubwa makubwa huku tumepiga tinted !
Huku tunawazoom wale mamilioni kwa mamilioni wanaokimbizana na maisha ili mkono uende kinywani !
Maisha kweli yamebadilika sana !

Nyerere alituchelewesha !!
RIP Mwalimu Nyerere 🙏🙏
 
Sasa mzee wangu, majibu utayapataje wakati muhusika ameshafariki? Ilipaswa awe hai kisha umuulize mwenyewe uso kwa macho
 
Kilichoongezeka kwa sasa ni watu wachache kuwatambia watu wengi ambao ni hohehahe !
 
Kwamba ubepari ni unyama na ujamaa ni utu ?

Chagua kuishi USA au North Korea, kisha jibu lako litakuambia wapi kuna utu wapi kuna unyama
 
Nyerere pia ndiye aliyetuepusha na udini, ukabila na ukanda mambo ambayo yalilitafuna sana bara la Africa kipindi hicho.
 
Wamesahau vita vya kagera vilivyo turudisha nyuma.
 
Kwamba ubepari ni unyama na ujamaa ni utu ?

Chagua kuishi USA au North Korea, kisha jibu lako litakuambia wapi kuna utu wapi kuna unyama
Ubepari ni ushetani. Wewe una njaa lakini mwenzako anasaza bila huruma ndivyo tunaishi hivyo kwa sasa. Ujamaa unataka wote muende pamoja hata mtu wa mwisho kabisa naye awezeshwe ndio maana tunaita ujamaa ni utu. Hamuoni licha ya matatizo tuliyonayo lakini mtu yupo radhi awe na fedha ambazo hatomaliza milele? Watu wanamiliki magari na majumba ya kifahari na ni viongozi wa serikali na kulipwa fedha nyingi ukiachia mbali kuiba lakini watu wanakosa huduma muhimu?
 
Wamesahau vita vya kagera vilivyo turudisha nyuma.
Hii nayo ni mojawapo na setbacks kwenye uongozi wa Nyerere, mleta mada badala ya kutumia muda mwingi kuhukumu tena kwa kutumia mifano nje, nadhani angejielekeza pia kwenye changamoto za kila awamu ili tupime awamu ipi ilikuwa na changamoto nzito zaidi ya nyingine, kisha tuone yupi alikuwa mzembe zaidi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Watu ni wajinga sana kama umegundua viongozi wengi wenye maono na mtazamo mwema kwa wananchi na ambao wamekuwa tayari kujitoa kwa ajili ya wananchi huishia kuitwa madikteta alafu wale wanao ruhusu ufisadi na wizi serikalini wanapewa sifa za kijinga.

Hata Yesu alikuwa mwema lakini akaishia kuuliwa bila kosa lolote. Binadamu ni wajinga na wapuuzi sana. Badala ya kumlinda mtu anayejali, sisi tunampiga mawe.
 
Wewe,you are quite mistaken. Unadhabi Ujamaa umekufa.
Ujamaa haujakuja.
By God! Tunazitamani sana hizo video zenu,na tutakuja kuwapora hizo video ili na sisi tuzitazame.
 
Kosa lilianzia kwenye mifumo ya kuabudu, MUNGU WETU HARISI, keshatukataa, hatuchagulii viongozi wa kutuvusha, hatufumbui kuhusu raslimali alizotuwekea ardhin kwetu, ametufanya kuwa watumwa wa kudum
 
Mtoa mada nadhani unakosea kwa kusema Nyerere hakuwa na huruma hata kidogo. Umechambua upande wa udhaifu wake ndio maana unaona hakua na huruma hata kidogo.
Chambua na upande wa mazuri yake ndipo utaiona huruma ya Nyerere kwa wananchi wake.
1. Nyerere kwa kipindi alichoongoza alikua na nafasi ya kuiba mali za umma na kujilimbikizia kadri atakavyo na asingekuwepo wa kumpigia kelele lakini hakufanya hivyo.
2. Mwl. J.K. Nyerere angetaka kutoa madaraka makubwa kwa watoto wake angefanya hivyo lakini mpaka sasa nadhani Makongoro Nyerere ndio kakumbukwa juzi hapa kuwa Mkuu wa Mkoa angalia hao wengine wanavyowapaisha watoto wao.
Inakua rahisi kumchambua udhaifu wake kwa kuwa kimepita kipindi kirefu inakua rahisi kuona makosa yake.
Kumbuka:
3. Mwl. Nyerere alitoka madarakani Nchi ikiwa na viwanda vingi sana lakini kutokana na ubinafsi na Ubepari leo hii viwanda karibu vyote vimeuzwa na kutelekezwa matokeo yake ajira nyingi sana zimepotea.
4.Harakati za kuunganisha Nchi unaweza kuzichukulia rahisi kwa kuwa unaona matokeo tu lakini mchakato wake sio wa kubeza. Pale ilifanyika kazi kubwa sana kuwaungansha watanzania na kuondoa ukabila na udini.
5. Nadhani nia ya Mwl.ilikua nzuri sana ila matokeo ndio hayakua mazuri.
Kitu kingine matokeo ya vita ya Kagera kwa uchumi wetu ilileta athari kubwa sana.
Vile vile Mwl.alijihusisha sana na ukombozi wa Nchi nyingine za Afrika. Hivyo alikua na mambo mengi sana ya kupigania katika lindi la ufukara wa Taifa.
Tujiulize
Miaka 38 tangu Mwl. Nyerere atoke madarakani ni eneo gani kama Taifa tunalifanya kwa ufanisi ndani ya Ubepari.
Nadhani sekta ya uchawa tu ndio tuko njema zaidi.
Mwl.apewe heshima yake
 
Kwamba ubepari ni unyama na ujamaa ni utu ?

Chagua kuishi USA au North Korea, kisha jibu lako litakuambia wapi kuna utu wapi kuna unyama
Namba 9 ina maajabu !
Upande moja inonekana ni 6 lakini upande mwingine ni 9.
Maisha yenye furaha ni mindset ya kila mtu alivyojitengenezea !!
Wapo watu wanayafurahia maisha huko Korea na wapo watu wanayachukia maisha huko USA !
 
Huo umeme ambao haukuwa kwenye mgao ulikuwa kwenye miji mingapi,

Unakumbuka maduka ya ushirika,?
 
Kwa io unaamini kwenye ujamaa, Mkuu wa mkoa anaishi sawa na mkulima wa nanjilinji?

Au unahisi Nyerere familia yake nayo ilipanga folen kwenye maduka ya ushirika? Au unadhani na Nyerere aliishi kama wakulima wa Namtumbo?

Duniani hakuna usawa, ila ni bora kwenye ubepari mana doors are open ila kwenye ujamaa doors are closed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…