Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Mkuu kuhusu hoja namba 1 kamuulize ndugu Amir Jamal na ndugu Bernard Membe upate ukweli na kuweka rekodi yako sawa sawa!

Kuhusu hoja 2 - 5 yalikuwa ni mambo ya kawaida ambayo Marais wengi katika nchi za Afrika na Eshia kwa wakati huo walifanya, hata zaidi yake.

Mkuu kipindi cha Nyerere ndio Tanzania ilijikuta ikiwa nchi masikini zaidi duniani.
 
Mkuu hali ilikuwa mbaya mno. Ukiona mikono inayobariki mashoga sasa hivi inatumika kumfanya Nyerere Mtakatifu, ujue kuna jambo la Kimaslahi zaidi ya kiimani!
 
Mkuu kweli unaweza kuhisi maumivu halisi na mabichi kama waliyopitia watu kipindi cha Azimio la Arusha la 1967, operation vijiji ya 1973, njaa ya 1974, vita ya Kagera ya 1979 na kadhalika kwa kusoma kitabu???

Mkuu watanzania walipitia wakati mgumu mno mikononi mwa Nyerere, Acha kabisa!
 
Kumbe wabongo mnapenda kupigwa!
 

Kwa sababu msingi tayari ni mbovu nyumba haiwezi kusimama
 

Sio hapakuwa na mgao wa umeme.
Sema nchi haikuwa na umeme vijiji vingi.
Sasa kama hakuna umeme kutakuwaje na mgao wa umeme.

Ni sawa useme elimu ilikuwa bure na bora alafu wakati huo huo waliozaliwa miaka ya 60-80 wengi tupo nao na hawana elimu yoyôte.

Propaganda mbaya sana
 
👍👏🆒
 
. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.​
Sera ya ujamaa na kujitegemea haikuwa mbaya kwa kiwango hicho.

Leo una sehemu ya kuishi, umesoma unatukana Nyerere.

Of course, wenye mali kwa wakati huo, wenginwakiwa wahindi ambao kiuhalisia walipewa upendeleo.wakati wa ukoloni ndio walikuwa na mali ndio waliumia
Leo nchi hii bado Ina ardhi, una kisehemu cha kuishi unabweka bweka tu.

Nenda Kenya kwa Mabepari ukajionee.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.​
Wakati wa uhuru,umoja ulihitajika kuliko chochote.

Cooperative zilikuwa chini ya Nani kabla ya kuwekwa chini ya TANU?
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.​
Watu binafsi kina ani waliokuwa na uwezo huo?
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.​
Huu ni uwongo.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.​
Uhuru wa mawazo, kivipi wakati hakukuwa na magazeti Wala social network.

Sana sana waliokuwa na vita na Nyerere zilikuwa za madaraka hasa kutokana na kutofautiana itikadi.

Kuna watu walitaka , wakitoka wakoloni wao ndio wawe wakoloni.

Wengine walitaka nchi iwe na dini.

Wengine walitaka makabila yao yawe TOP Kwasababu wamesoma kuliko wengine. Ulitakaje?
Ujamaa umefeli miaka ya 1980's haya tangu wakati huo mmeshafanya nini nje ya mawazo ya Nyerere.

  • Kaacha mashirika ya umma zaidi ya 400
  • Kaacha viwanda vya kutosha Kama General Tyre, Musoma Textile, Mwamza Textile etc leo mmefika wapi?
Nyerere ameachiwa Madaraka mwenyewe kwa hiari miaka 1985 huku nchi ikiwa mbichi.
  • Hakuchimba madini
  • Hakuuza bandari, Ngorongoro Wala Loliondo

Aliemdesha nchi hivyo kigumu kwa kutumia mazao ya wakulima.

Haya nyie Sasa hivi baada ya miaka karibu 40 mko wapi, zaidi ya kunywa makonyagi na kufirwa tu ndio mmegundua.
 
Kwa sababu msingi tayari ni mbovu nyumba haiwezi kusimama
Msingi gani mbovu unazungumzia ikiwa Nyerere baada ya kuondoka madarakani, kila kitu walikipindua upside down?!

Ulichokiandika hapa hakina maana, kujenga taifa sio sawa na kujenga nyumba, taifa halijengwi kwa matofali kwamba ukikosea msingi uwe umeharibu, taifa linajengwa kwa akili zilizochangamka, hivyo kama tumeshindwa kujisogeza mbele hilo haliwezi kuwa kosa la Nyerere, kwasababu hakuondoka na akili zetu, labda aliondoka na zako!.

- Leo tuna wasomi wengi.

- Tuna kila aina ya maarifa.

- Vyuo vikuu vingi.

Kuendelea kumlaumu Nyerere, miaka 38 baada ya kuondoka madarakani ni udumavu wa kifikra, binafsi sioni kingine zaidi ya hicho. Ndio maana hata Nyerere mwenyewe kwa kutambua watu wake ni wajinga, aliwahi kunukuliwa akisema; "ajabu wanaacha yale mazuri yangu, wanachukua mabaya"!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Walidanganya sana vijana wakati wanasoma kumuimba kama shujaa wakati ni kinyume chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…