Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Nyerere alikuwa na propaganda zilizosoma shule.
Akikupiga dongo moja nchi nzima inakuchukia.

Sitasahau tulivyoimbishwa mabaya ya Idd amini tukiwa kwenye michakamichaka ya shule
Watanzania wengi tunapenda sana mambo marahisi lakini ukweli Mzee Nyerere alitukosea sana. Matatizo mengi yanayoendelea hapa nchini Tanzania yanaratibiwa na kizazi cha makada, majasusi na wasomi wenye mlengon wa kijamaa ambao walitengenezwa na MTAKATIFU RAISI NYERERE. Mambo mengi tu ni dhahiri ambayo ni lazima tuulize:

1. Katiba ya mwaka 1977,
2. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
3. Sera ya Ujamaa na Kujitegemea.
4. Kupigania uhuru wa nchi za Afrika (Nyerere ndiyo aliwaweka Kagame, Mugabe na Museveni madarakani)

Hizi ndiyo LEGACIES kubwa ambazo MTAKATIFU RAISI NYERERE, alituachia Tanzania. Sasa tujiulize kwenye lipi hapa alifanikiwa labda na kwa kiwango kipi, maana mengi hapa ni Propaganda zaidi ya uhalisia ambao ulikuwepo.​
 
Unasema kina nani walikuwa na uwezo wa kuagiza vitu nje ? Kwan Mwinyi aliporuhusu ni nani walikuwa wanaagiza ?
Tangu mmeanza kuagiza, mnajitosheleza na nini?
Aliminya maoni, gazeti la serikali tu, Redio moja nch nzima hakuna nyingine, Huruhusiwi kumiliki TV au Radio, ukikutwa na computer 💻 ni kosa kubwa wanaweza kukutoa pumbu bila ganzi kisha wakupe ule na pilipili
Wewe brainwashed wa mwaka 2000. Miaka ya 1960s sito jana Wala juzi.

Hujui nchi na dunia ilikuwa katika nyakati gani?

Siyo nyakati za shisha .
Hivyo viwanda Nyerere kaviacha vina hali mbaya balaa, mitambo ilikuwa ipo very outdated, productions cost zikiwa juu unrealistically, mauzo yakiwa chini sanaaa, (mana aliua uchumi wa mtu mmoja mmoja yeye mwenyewe) ,
Sema tu aliacha magofu ya viwanda,
Haya, zilikuwa outdated kulingana na wakati huo.

Ninyi Sasa hivi wenye advanced technology mmefanya nini?
Kifupi tu Nyerere ni raisi wa ovyo sana hii nchi kupata
Nyerere ni ovyo nakubaliana na wewe. Ila mliobaki ni MAVI kabisa, ya nguruwe.
 
Sera ya ujamaa na kujitegemea haikuwa mbaya kwa kiwango hicho.

Leo una sehemu ya kuishi, umesoma unatukana Nyerere.

Of course, wenye mali kwa wakati huo, wenginwakiwa wahindi ambao kiuhalisia walipewa upendeleo.wakati wa ukoloni ndio walikuwa na mali ndio waliumia
Leo nchi hii bado Ina ardhi, una kisehemu cha kuishi unabweka bweka tu.

Nenda Kenya kwa Mabepari ukajionee.

Wakati wa uhuru,umoja ulihitajika kuliko chochote.

Cooperative zilikuwa chini ya Nani kabla ya kuwekwa chini ya TANU?

Watu binafsi kina ani waliokuwa na uwezo huo?

Huu ni uwongo.

Uhuru wa mawazo, kivipi wakati hakukuwa na magazeti Wala social network.

Sana sana waliokuwa na vita na Nyerere zilikuwa za madaraka hasa kutokana na kutofautiana itikadi.

Kuna watu walitaka , wakitoka wakoloni wao ndio wawe wakoloni.

Wengine walitaka nchi iwe na dini.

Wengine walitaka makabila yao yawe TOP Kwasababu wamesoma kuliko wengine. Ulitakaje?

Ujamaa umefeli miaka ya 1980's haya tangu wakati huo mmeshafanya nini nje ya mawazo ya Nyerere.

  • Kaacha mashirika ya umma zaidi ya 400
  • Kaacha viwanda vya kutosha Kama General
Nimeshakwambia Nyerere aliondoka madarakani miaka 38 iliyopita, kwani aliondoka na akili zetu mpaka tuendelee kumlaumu mpaka leo? hapa sio suala la msingi wala paa!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Kam Unafikiri Nyerere kaondoka kwenye hii nchi bado unasafari ndefu kwenye kujua mambo ya siasa ya nchi hii.
 
Kam Unafikiri Nyerere kaondoka kwenye hii nchi bado unasafari ndefu kwenye kujua mambo ya siasa ya nchi hii.
Kama bado unaendeshwa na mtu aliyoko kaburini Basi wewe ni NGURUWE KIBUDU.

Wameua misingi mingi mizuri ya Nyerere, hayo mabaya kubadilisha mnashindwa nini:
  • Miiko ya uongozi
  • Azimio la Arusha
  • Mambo ya muungano.

Siasa nchi unaendeshwa KITAPELI TAPELI Kama MAZUZU
 
Kama bado unaendeshwa na mtu aliyoko kaburini Basi wewe ni NGURUWE KIBUDU.

Wameua misingi mingi mizuri ya Nyerere, hayo mbaya kubadilisha mnashindwa nini:
  • Miiko ya uongozi
  • Azimio la Arusha
  • Mambo ya muungano.

Siasa nchi unaendeshwa KITAPELI TAPELI Kama MAZUZU
Hao viumbe sijui wana mindset ya aina gani, kusema Nyerere bado anaishi huku wameharibu kila kizuri alichofanya kama viwanda, naona wana na matatizo ya akili.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nyerere alikuwa binadamu kama sisi! Licha ya kwamba alikuwa na nia njema ya kuleta usawa ni kweli alikosea!
Hata hivyo ni makosa yaliyosahihishika!
Changamoto tunayopata ni kutuachia Katiba iliyolinda Mamlaka yake, ya kutohoji Serikali hata kama imekosea, na ambayo ilirithiwa toka awamu moja mpaka nyingine!
Lakini hata baada ya yeye kuondoka nchi imeendelea kuwa Masikini tu.
Kwa yanayoendelea sasa hivi yapo ambayo tunaweza kusema ni afadhari enzi za Mwalimu kuliko za sasa hivi!
Changamoto ya Tanzania siyo umasikini. Katika ngazi ya kitaasisi Tanzania imekuwa sana kiuchumi na inaendelea kukua kwa kasi. Nchi ina uwekezaji kutoka nje (FDI), inafanya biashara za kimataifa (International Trade) na ina nguvu kazi iliyoelimika (Skilled Manpower). Changamoto kubwa ya Tanzania ni mgawanyo wa keki ya taifa (Redistribution of National Wealth), kwasababu sehemu kubwa ya uchumi wa nchi inamilikiwa na matajiri wachache ambao mifumo inawalinda. Hili ni tatizo ambalo linaikumba dunia yote kwasasa, kwamba watu wanafanya kazi lakini utajiri wao unanyonywa kupitia mifumo ya kiutawala.

Hata Marekani kuna hii shida, Uingereza kuna hii shida, Nigeria ambako ndiyo wakubwa hapa barani kuna hii shida. Ndiyo maana unakuta taifa linatangazwa kweli linakua kiuchumi, lakini huo uchumi wewe raia wa kawaida hauoni, ni kwasababu mifumo inakupa wewe kitu kidogo ila inakunyonya sana. Hili ndiyo mwanauchumi nguli kabisa duniani aliyewahi kushinda tuzo ya Nobel, Prof Joseph Stiglitz anaelezea kwenye kitabu chake kiitwacho THE PRICE OF INEQUALITY. Hivyo Tanzania, chakula kipo, ardhi ipo, huduma zipo lakini kuzipata huduma hizo bila kuwa na pesa ndiyo changamoto.

Hivyo wananchi wengi na watumishi wa ummah, wanafanya kazi sana huku nguvu zao zikinyonywa na wanaoshikilia mfumo. Wanakata kodi kubwa (Levying Heavy Taxes), hawadhibiti mfumuko wa bei (They can't curb inflation) jambo ambalo linaharibu akiba za watu, hawayatozi mashirika makubwa kodi inayotakiwa(Tax Holidays to the Rich), matumizi yasiyo na msingi (Excessive Government Spending) na rushwa (Corruption). Hizi ndizo changamoto zetu kipindi hiki, Raisi Mzee Mkapa alijitahidi kupambana nazo japo hilo la rushwa lilimshinda kabisa.​
 
Haya mengine ya kisiasa ntayazungumzia siku ingine panapo majaaliwa. Ila kilichonileta hapa ni kuuliza kwanini bado aliendelea kutumia mabavu na kulazimisha sera zake hata pale ambapo mamilioni ya watanzania walikuwa wanapitia kipindi kigumu mno kimaisha. Najiuliza kwanini hakuwa hata na chembe ya huruma pale ambapo watanzania wengine walikosa chakula hadi kuchemsha pumba na huku wengine wakilala njaa ? Najiuliza sana, lengo lake haswa lilikuwa ni nini, lakini sipati majibu?​

Nadhani swali kubwa zaidi kujiuliza ni kwa nini pamoja na mateso yote waliyopitia watanzania, bado aliendelea kuwa na ushawishi mkubwa hata baada ya kutoka madarakani na pia kifo chake kilitia simanzi watu wengi haswa maskini waliokuwa wanateseka zaidi.

Kingine cha kujiuliza ni kwa nini baada ya kifo chake, kulitokea mabadiliko makubwa haswa kuleta mfumo wa soko huria lakini bado viongozi waliopo hawajapata imani ya wananchi tofauti na enzi hizo za mateso na wala nchi haijapiga hatua kama nchi ulizozitolea mfano.

Binafsi yangu naamini Nyerere alifanya makosa mengi lakini dhamira yake haikuwa mbaya maana hakunufaika financially kwa yote aliyoyafanya hivyo, alijaribu kujenga misingi ya Tanzania ya ndoto yake tofauti na sasa nchi inavyojiendea bila kuwa na direction.

Naamini pia yeye kuona ugumu na kuuvumilia si kwamba alikuwa haumii ila aliichukulia kama gharama ya kutimiza malengo kama yeye na watu wengine walivyoumia kama gharama ya kuleta uhuru 🙏🏽
 
Kama bado unaendeshwa na mtu aliyoko kaburini Basi wewe ni NGURUWE KIBUDU.

Wameua misingi mingi mizuri ya Nyerere, hayo mbaya kubadilisha mnashindwa nini:
  • Miiko ya uongozi
  • Azimio la Arusha
  • Mambo ya muungano.

Siasa nchi unaendeshwa KITAPELI TAPELI Kama MAZUZU

Unajua Azimio la Arusha tangu kuanzishwa 1967 mpaka 1985 wakati Nyerere anaachia kijiti ni zaidi ya miaka 17. Unafikiri ni kwa nini Azimia la Arusha halikufanikiwa licha yakuwa muasisi wake ndiye aliyekuwa incharge?

Kwenye miiko ya uongozi, ndio hapo Mtoa mada anauliza. Hiyo miaka ya 1980 - 1985 (Sikuwepo)nini kilimfanya Nyerere asiwe na huruma?

Unasema huongozwi na Mtu akiyekaburini alafu wakati huohuo unatumia Katiba yake. Hii ni akili gani?
 
Ninachokiona hapa ni chuki dhidi ya Nyerere na ujamaa wake...

Malcom ningekushangaa kama ungemsifia Nyerere na ujamaa wake ili hali wewe ni bepari

Haiwezi tokea ...

Ninachokijua ni kuwa Nyerere hakua malaika, alikua binadamu mwenye mazuri na mabaya...

Kwa msingi huo sidhani kama ni sawa kumweleza Nyerere kwa mabaya huku mazuri tukiyafumbia macho...

Kwa kutumia itikadi ya ujamaa Nyerere aliweza kutufanya watanzania tujione ni ndugu licha ya tofauti za makabila...

Ujamaa uliwafanya watanzania kusoma bure na kutibiwa bure kama nakosea naruhusu kukosolewa...

Ujamaa kama tusingeruhusu vita ya kagera nchi yetu ingekua mbele ya nchi zote za Afrika mashariki na kenya ikiwemo....

Huo ubepari unaoupigia kampeni sijawahi ona faida zake kwa nchi za Afrika, kama zipo zitaje.
 
Hao viumbe sijui wana mindset ya aina gani, kusema Nyerere bado anaishi huku wameharibu kila kizuri alichofanya kama viwanda, naona wana na matatizo ya akili.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Anayeharibu ni Nani kama sio Watu walewale walioandaliwa n Nyerere?
Chama kilekile
Mfumo uleule
Katiba ileile
Falsafa zilezile.

Nafikiri humjui vizuri Nyerere.
N Kwa Sisi tusiomjua tutatumi Katiba yake kumjua, falsafa zake, Watu aliowaandaa kuongoza nchi, chama chake. Hivyo yaani
 
Uzombie ndani ya nchi hii ulipandikizwa na Nyerere. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio itakuwa ubatizo wa nchi hii.
Ukitembea nchi nyingi za Afrika utafahamu kwamba mbali na changamoto zilizopo, Tanzania yetu ni nchi ambayo ina upekee wa aina yake. Usipotembea na kuona huko nje kuna matatizo gani huwezi kukosa kuwa na shukrani. After knowing what's going on in some African states, I can't be grateful enough a Tanzanian. Tatizo letu kubwa hapa nchini ni genge la WAJAMAA au MIZEE YA COLD-WAR ambayo imeshikilia mifumo, imejimilikisha mali na inaitafuna nchi kwelikweli pamoja watoto na wajukuu zao.

Wengi wao ni wale makada, viongozi waandamizi wa dini, wasomi na majasusi waliongizwa kwenye mfumo na MTAKATIFU RAISI NYERERE wakiwa vijana wadogo na wakakulia kwenye mfumo na sasa wanaamini nchi ni mali yao binafsi. Hawa ndiyo inabidi tuwafulumushe bila huruma. Ila watanzia wengi, hawana matatizo, wengi ni watu waungwana mno, ambapo uungwana wao umetumiwa kama silaha na hii jamii ya wanyonyaji.​
 
Changamoto ya Tanzania siyo umasikini. Katika ngazi ya kitaasisi Tanzania imekuwa sana kiuchumi na inaendelea kukua kwa kasi. Nchi ina uwekezaji kutoka nje (FDI), inafanya biashara za kimataifa (International Trade) na ina nguvu kazi iliyoelimika (Skilled Manpower). Changamoto kubwa ya Tanzania ni mgawanyo wa keki ya taifa (Redistribution of National Wealth), kwasababu sehemu kubwa ya uchumi wa nchi inamilikiwa na matajiri wachache ambao mifumo inawalinda. Hili ni tatizo ambalo linaikumba dunia yote kwasasa, kwamba watu wanafanya kazi lakini utajiri wao unanyonywa kupitia mifumo ya kiutawala.

Hata Marekani kuna hii shida, Uingereza kuna hii shida, Nigeria ambako ndiyo wakubwa hapa barani kuna hii shida. Ndiyo maana unakuta taifa linatangazwa kweli linakua kiuchumi, lakini huo uchumi wewe raia wa kawaida hauoni, ni kwasababu mifumo inakupa wewe kitu kidogo ila inakunyonya sana. Hili ndiyo mwanauchumi nguli kabisa duniani aliyewahi kushinda tuzo ya Nobel, Prof Joseph Stiglitz anaelezea kwenye kitabu chake kiitwacho THE PRICE OF INEQUALITY. Hivyo Tanzania, chakula kipo, ardhi ipo, huduma zipo lakini kuzipata huduma hizo bila kuwa na pesa ndiyo changamoto.

Hivyo wananchi wengi na watumishi wa ummah, wanafanya kazi sana huku nguvu zao zikinyonywa na wanaoshikilia mfumo. Wanakata kodi kubwa (Levying Heavy Taxes), hawadhibiti mfumuko wa bei (They can't curb inflation) jambo ambalo linaharibu akiba za watu, hawayatozi mashirika makubwa kodi inayotakiwa(Tax Holidays to the Rich), matumizi yasiyo na msingi (Excessive Government Spending) na rushwa (Corruption). Hizi ndizo changamoto zetu kipindi hiki, Raisi Mzee Mkapa alijitahidi kupambana nazo japo hilo la rushwa lilimshinda kabisa.​

Tanzania dependency ratio bado ni kubwa brother na hata ukiangalia kiwango kikubwa cha ajira na biashara kinategemea sekta isiyo rasmi ambayo ni hand to mouth. Kiufupi Tanzania tuna unproductive population na hata graduates bado wengi hawawezi kupambana katika mfumo wa dunia

Hiyo FDI ni sawal lakini impact yake kwa common mwananchi ni nini zaidi ya Capital inflow and profit outflows ya kutosha

Huko kwenye international market tunyamaze tu maana ukifikiria balance of trade unaweza kulia japo haishangazi maana hata toothpick tunaagiza

Kiufupi vya kujivunia vichache
 
Unajua Azimio la Arusha tangu kuanzishwa 1967 mpaka 1985 wakati Nyerere anaachia kijiti ni zaidi ya miaka 17. Unafikiri ni kwa nini Azimia la Arusha halikufanikiwa licha yakuwa muasisi wake ndiye aliyekuwa incharge?
Azimio la Arusha halikufanikiwa kutokana na sera za ujamaa kufikia mwisho, hasa duniani kote.
Kwenye miiko ya uongozi, ndio hapo Mtoa mada anauliza. Hiyo miaka ya 1980 - 1985 (Sikuwepo)nini kilimfanya Nyerere asiwe na huruma?
Kutokuwa na huruma kivipi?

Kuwa specific?
Unasema huongozwi na Mtu akiyekaburini alafu wakati huohuo unatumia Katiba yake. Hii ni akili gani?
Kinachokushinda kubadilisha hiyo katiba kwa Sasa hayupo ni nini?
 
Ujamaa ni mzuri kwa nje au mtu akikusimulia. Lakini haufanyi kazi. Huwezi kuwafanya watu wawe sawa wakati kiasili tu watu hawako sawa. Equality is an abnormality.
Ukiwaambia watu kwamba Uchina wameanza kufanikiwa baada ya kuruhusu watu kumiliki uchumi hawakubali. Command Economy without Free Enterprise is destined to fail miserably. Ukweli ni kwamba, Tanzania yalifanywa makosa makubwa kwenye suala zila la kuruhusu watanzania kumiliki uchumi wao, na watanzania hawataki kuukubali huu ukweli, kwamba Raisi Nyerere angeruhusu baadhi ya mashirika yamilikiwe na watanzania asingekumbwa na kadhia ya miaka ya 1980's. Kilimo na uzalishaji vingekuwa juu, uwekezaji ungekuwa juu na watu wengi wangepata ajira.

Tena kwa mtu mwenye hulka ya MTAKATIFU NYERERE, lazima kila mtu angelipa kodi nchi hii. Lakini akaamua kila kitu kifanywe na serikali yake (The Nanny Government) na mambo yalipofeli akagoma kukubali ukweli na kutuingiza wananchi wengi kwenye lindi la umasikini. For some people, this is a bitter pill to swallow!​
 
Azimio la Arusha halikufanikiwa kutokana na sera za ujamaa kufikia mwisho, hasa duniani kote.

Kutokuwa na huruma kivipi?

Kuwa specific?

Kinachokushinda kubadilisha hiyo katiba kwa Sasa hayupo ni nini?

1. Sasa mbona unasema Watu siku hizi hawafuati Azimio la Arusha wakati muda huohuo unakubali kuwa sera na falsafa zilizokuwapo kwenye Azimio hilo zilipitwa na wakati duniani tangu miaka hiyo. Ikiwemo ideology ya ujamaa.

2. Kutokuwa na huruma rejea alichoandika mtoa post ndio anataka majibu. Kumjibu kama mnatofautiana hayo majibu.

3. Kinachoshinda Watu kubadili hiyo mifumo ni kwa sababu bado nchi ipo mikononi mwa Wafuasi wa Nyerere.
Wapi hapaeleweki
 
Miaka 38 tangu ametoka madarakani, hiyo misingi imara mnasubiri mpaka afufuke aje kutengeneza?
Hii katiba inayomfanya Rais awe juu ya Sheria ni yeye aliiweka. Unatarajia Nini kama cheo Cha rais ndio kinapanga nani awe kiongozi? Au unadhani misingi mibovu ya hivyo inaondoka kirahisi huku afrika bila machafuko na mapinduzi ya kijeshi?
 
Badilisheni.

Nyerere katoka madarakani mwaka 1985.

Nyerere kafa mwaka 1999.

Mpo tu mnakunywa makonyagi na kuvaa vinjunga mnatamani kila kitu angekuwa amefanya na kumaliza Nyerere.

Stupid
 
Na Nyerere ndio muasisi wa wizi wa kura ndani ya nchi hii. Bila kuondoa maagano ya kishirikina aliyoweka Nyerere nchi hii, tutaendelea kutawaliwa kwa shuruti na chama chake. Ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi Ili tuanze upya kwenye mfumo wa kiutawala nchi hii.
Hili nalo ni ukweli ambao hauwezi kupingwa. Tume ya Jaji Nyalali ilileta mapendekezo kwamba asilimia 80% ya watanzania hawataki mfumo wa vyama vingi. MTAKATIFU RAISI NYERERE kama ilivyokuwa kawaida yake, akaamua kulazimisha mfumo wa vyama vingi ambao yeye na swahiba wake Kambona waliufuta punde baada ya kumshinda Bwana Zuberi Mtemvu wa ANC. Ambacho kinashangaza ni kwamba, hata baada ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi, MTAKATIFU RAISI NYERERE alianzisha mchakato wa kuhujumu demokrasia, kwanza ndani ya CCM, kisha kwenda nje ya vyama vya upinzani na kutengeneza kitu kiitwacho CONTROLLED OPPOSITION.

Wote tunafahamu kwamba, within party circles Mzee wetu Mkapa stood no chance against the likes of Kolimba, Malecela, Msuya even young blood Jakaya. Let alone outside, vying against the collosus of the time Lyatonga Mrema and his infamous acolytes like Prof Babu. Watu wengi mno walisulubishwa uchaguzi, kina General Kombe wangekuwepo hai wangesimulia. Baadaye tena wakapishana na Mzee Mkapa, akaanza hujuma za chinichini dhidi yake jambo ambalo halikufanikiwa. Mkapa aliyemuweka madarakani, akawa hamtaki. Sasa najiuliza, yule mzee alikuwa anataka nini haswaaa na sisi watanzania nakosa majibu.​
 
Back
Top Bottom