Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

1. Sasa mbona unasema Watu siku hizi hawafuati Azimio la Arusha wakati muda huohuo unakubali kuwa sera na falsafa zilizokuwapo kwenye Azimio hilo zilipitwa na wakati duniani tangu miaka hiyo. Ikiwemo ideology ya ujamaa.
Nyerere alikuwa na dira na maono yake.

Na aliyapambania hata Kama mengine yalikwama.

Tena amefariki dira yenu Sasa hivi ni ipi zaidi ya kuuza kila kitu na kuvimba MITUMBO.

Nyerere hakuiba kitu, kaacha nchi Bikra kabisa. Hata Kama alifeli, mmeshindwa nini kupiga hatua miaka 35 Sasa??
2. Kutokuwa na huruma rejea alichoandika mtoa post ndio anataka majibu. Kumjibu kama mnatofautiana hayo majibu.
Mtoa maoni kaweka rejea yoyote?

Nyerere ambaye alikuwa anasamehe kina Bibi titi, Kambona na Abdul Jumbe??

Mtu asiye na utu ni Kama Kikwete kung'oa meno Ulimboka au Kutandika risasi Kama unaua chatu alikofanya Magu.
3. Kinachoshinda Watu kubadili hiyo mifumo ni kwa sababu bado nchi ipo mikononi mwa Wafuasi wa Nyerere.
Wapi hapaeleweki
Wafuasi wa Nyerere ni Nani Sasa hivi kwenye mfumo?

Maana kina Madaraka, Butiku, WARIOBA hawana usemi kwa Sasa?

Acheni visingizio mavi ya bata.
 
Kwenye hili Nyerere alikuwa ndiye bingwa. Alikuwa kila anayemkosoa anahama nchi. Ni vile tu ukweli hausemwi na bahati mbaya Nyerere katawala ktk kipindi ambacho media outlets zilikuwa hakuna.

Redio ya taifa ilikuwa inaandikiwa nn cha kusema kuhusu rais kwenye taarifa ya habari.

¶ Nyerere ndiye aliyefanya Kambona kuishi ukimbizini maisha yake yote.
¶ Nyerere ndiye aliyechana vyeti vya Tuntemeke Sanga.
¶ Nyerere ndiye aliyemfunga kifungo cha nyumbani (alimuweka kizuini) Kasangatumbo
¶ Nyerere ndiye alimuondoa kwenye urais Abdul Jumbe halafu akamuweka kizuizini hapo Kigamboni mpk umauti.
¶> Nyerere ndiye aliyetunga hili katiba bovu lililomfanya yeye kujipa umungu wa Tanzania.

Nyerere ni dikteta asiyesemwa.
Kwani sasa hivi ndiyo Mtanzania ana maisha mazuri?mbona bado kundi la watawala na watu wao wa karibu ndiyo wananeemeka na keki ya taifa!
Kwaiyo shida siyo itikadi bali ni kuwa viongozi wa Afrika ni majangili!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
NChi iharibiwe na mwinyi akishauriwa na lipumba.vu leo mnalaumu mzee wa watu aliepigania hii nchi kwa kila pumzi yake
Je benki alizoziancha mzee bado zipo?
Shirika la Usafirishaji?
National milling bado ipo?
Shirika la ndege na ndege zake bado zipo?
Shirika la reli?
Viwanda vya nguo, saruji,chuma, matairi?
Gesi?
Mafuta?
Madini?
Bandari?
Halafu umejishibia maharage huko unakuja kujamba na kumdhihaki mzee wa watu
 
Kwanza sijui kwanini unatumia jina MTAKATIFU ikiwa bado Kanisa Katoliki halijamuidhisha kuitwa hivyo, sijui una malengo gani, muhimu ukumbuke tu, chakula huliwa kikiwa na chumvi ya wastani, ikizidi au kupungua huondoa ladha kwa walaji.

- Hilo suala la huruma unalozungumzia sijui hata unataka huruma ya aina gani? kwani ni kiongozi gani wa hili taifa amewahi kuwa na huruma na watanzania? tena kwangu afadhali ya Nyerere kuliko hawa waliomfuatia, ni walafi na mafisadi wa kutisha, tuliza mihemko utafakari kwa makini.

- Unaposema kuwashtaki waliokuwa wakilisha familia zao una maana gani? hao waliolisha familia zao walifuata sheria za wakati huo au walikiuka? kama walikiuka kwanini sheria isichukue mkondo wake? nakuona upo upande wa kutetea wahalifu bila sababu ya msingi.

Sitaki kuamini kama Nyerere na Sokoine walikuwa wakikamata watu hovyo barabarani na kuwabambikia kesi kama unavyotaka kuonesha hapa, hao waliokamatwa palikuwepo na vyombo vya usalama wakati huo vikajiridhisha, kama hawakuwa na maelezo ya kutosha kuelezea walipopata hizo mali sioni tatizo kwao kukamatwa.

- Ajabu kwako wahujumu uchumi unawaona wajanja kwa kuwaita walikuwa na akili za haraka, mindset yako na Nyerere ziko tofauti kabisa, hivyo sishangai ukimuona mkosefu. Jiulize; hao wenye akili za haraka leo wako wapi na wengine kule vijijini/mijini nao wako wapi kiuchumi? Jibu unalo.

Suala la mahakama kuwa ya aina gani hilo kwangu siwezi kuingilia, wao ndio walioona pawepo na mahakama ya aina gani kwa wakati husika ili kupeleka mambo kwa haraka, kama mambo yaliharibika mbeleni nimeshakwambia Nyerere nae hakuwa malaika, alikosea kama hawa wanaokosea wakati huu, sijui kwanini unalazimisha makosa ya Nyerere yaonekane ndio makubwa kupita ya wote waliomfuatia.

NB.
Matumizi ya neno MTAKATIFU kwenye majibu yako kwangu naona unavuka mipaka, ni either uache kutumia hilo neno, niendelee kuwepo hapa, au uendelee kulitumia hilo neno niondoke hapa. Hayo mambo kwa sasa yapo chini ya Kanisa Katoliki kimchakato, hivyo naamini huna sababu yoyote ya maana ya kutumia jina hilo zaidi ya ujuaji ulionao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nami nimepata mshangao wa kulitumia neno MTAKATIFU sijui anafanya dhihaka au nini. Kwa namna alivyo humu ndani jf na hiyo lugha anayotumia ndo hayo tunayosema madhaifu ya kibinadamu.
 
TATIZO SIO NYERERE BALI UDINI,,,KISA BABU ALIKUA MGALATIA
Kama ulikuwa hufahamu, Benjamini William Mkapa alikuwa ni Mgalatia wa Wagalatia. Lakini kwenye uchumi tunamsifia kwasababu alikuwa PRAGMATIC. Mambo mengi ambayo Tanzania inatambaa nayo yalianzishwa na Mzee Mkapa ambaye aliikuta nchi imeishiwa kila kitu. Alifanya kazi sana yule Mzee, tatizo lake likawa ni rushwa kwa watu wachache ambayo imakithiri. Katika hili hata yeye alikiri makosa kwamba aliingizwa mkenge na alisema wazi kabisa kwamba anajutia.

Upande mwingine hata lile la Zanzibari alisema ni doa kwenye uongozi wake, japo tunasema mkubwa haombi msamaha wa moja kwa moja, sisi waungwana tulimuelewa. Waliomshauri na kumchochea Mzee Mkapa kuhusu Mwembechai tunawafahamu ni wakina nani, pamoja na malengo yao. Ila katika yote Mzee Mkapa alikuwa ni muungwana na alijitahidi kufuata ushauri wa kitaalamu hata kutoka kwa wapinzani wake kama Mzee Prof Lipumba. Binafsi hili kwangu linatosha kuonesha nia njema ya marehemu Mzee Mkapa.

Turudi sasa kwa MTAKATIFU MZEE NYERERE. Kuna siku baada ya kustaafu alisema kabisa hadharani anaatembea na Biblia na Azimio la Arusha, na kuendelea kusema kwamba anaamini Ujamaa ndiyo njia pekee sahihi kwa Tanzania. Najiuliza tu, njia sahihi hata baada ya kusababisha nchi ipigwe na MAPOOZA nA UKAUFU miaka ya 80's. Mzee Nyerere alikuwa hakili makosa kama yeye binafsi, alikuwa ni lazima aongee kwa ujumla na atafute mtu au sababu ya kumrushia furushi. Kipindi cha uongozi wake Mzee Raishid Mfaume Kawawa, took a lot of bullets for Nyerere. Ana he took them proudly like a trooper. Kawawa alimpenda sana Nyerere.

Huo ugalatia ambao wewe unataka kuulazimisha hapa, it's not watertight....​
 
Huwa najiuliza sana lakini sipati majawabu, lakini naomba wasomi wa humu ndani mnisaidie.

Hivi Mzee Nyerere alikuwa ana roho ya namna gani kuona mambo kama haya yakitokea kwa wananchi lakini bado hataki kubadilika na akaendelea kutumia mkono wa chuma kuhakikisha anasigina kabisa uwezo binafsi wa mtanzania kuweza kujikwamua kiuchumi. Ujamaa wa Tanzania hakuleta matokeo yoyote makubwa na ya kuchangaza ukilinganisha na kule Asia na Ulaya ambako walau walifanya mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Uchina walifanikiwa sana baada ya Raisi Deng Xiaping kuanza kuwaonea huruma raia wake akifahamu kabisa kwamba njia waliyokuwa wanaenda ilikuwa siyo sahihi. Aliruhusu watu waanze kumiliki mali zao binafsi na kufanya biashara. Najiuliza sana, miaka yote 18 ya Ujamaa, yalifanyika na kutokea mambo mengi mno kwa watanzania, kiasi kwamba kiongozi yoyote mwenye huruma na wananchi ni lazima angekaa chini na kujifanyia tathmini, lakini Raisi Nyerere hakufanya hivyo, aliendelea kuwa na moyo mgumu kama Farao. Hebu tuzingatie haya:

1. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.

Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.

Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirudi.

Hivi kwanini MTAKATIFU na MWENYEHERI, Raisi Nyerere hakuwa na chembe ya huruma moyoni ?
Kuna mambo nikikumbuka huwa naumia sana na nakosa majawabu. Hivi alikuwa anapenda kutuona sisi vile ?​
Nyerere kwa asilimia kubwa alifata maagizo ya kanisa katoliki. Alikuwa mjanja wa maneno tu lakini kwenye uchumi alikuwa sifuri kabisa.
 
Ila Nyerere naye kwa maigizo alikuwa hajambo. Anapanga mstari kuwa anachagua kiongozi, lakini tayari alikuwa na matokeo mfukoni! Ogopa kiongozi aliyekuwa anaamini kiongozi wa kweli atatoka ccm, yaani Hawa watoto wa kina Mwigulu ndio Nyerere alimaanisha hao!
Nyerere na Jakaya utadhani ni mtu na baba yake. They both were nefariously cunning with a mesmerizing charm. Always pointing left while moving right. Kiukweli, siasa waliifahamu vizuri.
 
Huwa najiuliza sana lakini sipati majawabu, lakini naomba wasomi wa humu ndani mnisaidie.

Hivi Mzee Nyerere alikuwa ana roho ya namna gani kuona mambo kama haya yakitokea kwa wananchi lakini bado hataki kubadilika na akaendelea kutumia mkono wa chuma kuhakikisha anasigina kabisa uwezo binafsi wa mtanzania kuweza kujikwamua kiuchumi. Ujamaa wa Tanzania hakuleta matokeo yoyote makubwa na ya kuchangaza ukilinganisha na kule Asia na Ulaya ambako walau walifanya mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Uchina walifanikiwa sana baada ya Raisi Deng Xiaping kuanza kuwaonea huruma raia wake akifahamu kabisa kwamba njia waliyokuwa wanaenda ilikuwa siyo sahihi. Aliruhusu watu waanze kumiliki mali zao binafsi na kufanya biashara. Najiuliza sana, miaka yote 18 ya Ujamaa, yalifanyika na kutokea mambo mengi mno kwa watanzania, kiasi kwamba kiongozi yoyote mwenye huruma na wananchi ni lazima angekaa chini na kujifanyia tathmini, lakini Raisi Nyerere hakufanya hivyo, aliendelea kuwa na moyo mgumu kama Farao. Hebu tuzingatie haya:

1. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.

Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.

Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirudi.

Hivi kwanini MTAKATIFU na MWENYEHERI, Raisi Nyerere hakuwa na chembe ya huruma moyoni ?
Kuna mambo nikikumbuka huwa naumia sana na nakosa majawabu. Hivi alikuwa anapenda kutuona sisi vile ?​
Huu ndio upumbavu Magufuli alikuwa anaturidisha huko, halafu kuna watu wanamshangilia
 
Nyerere kwa asilimia kubwa alifata maagizo ya kanisa katoliki. Alikuwa mjanja wa maneno tu lakini kwenye uchumi alikuwa sifuri kabisa.
Uko sahihi kuwa Nyerere kwenye uchumi alikuwa empty set. Nyerere angetaka kuwa kiongozi mzuri angekaa madarakani miaka 10 tu. Lakini kitendo cha kukaaa madarakani Hadi aibu ilipomkuta ndio alipochemkia.
 
NChi iharibiwe na mwinyi akishauriwa na lipumba.vu leo mnalaumu mzee wa watu aliepigania hii nchi kwa kila pumzi yake
Je benki alizoziancha mzee bado zipo?
Shirika la Usafirishaji?
National milling bado ipo?
Shirika la ndege na ndege zake bado zipo?
Shirika la reli?
Viwanda vya nguo, saruji,chuma, matairi?
Gesi?
Mafuta?
Madini?
Bandari?
Halafu umejishibia maharage huko unakuja kujamba na kumdhihaki mzee wa watu
Pamoja na kuacha vyote hivyo, anyerere alikuwa anaendesha nchi kwa mazao ya kilimo.

Leo yanauza kila kitu, bandari, madini, hewa (carbon credit) mpaka twiga na vyura yanauza, lakini hakuna kitu.
 
Uko sahihi kuwa Nyerere kwenye uchumi alikuwa empty set. Nyerere angetaka kuwa kiongozi mzuri angekaa madarakani miaka 10 tu. Lakini kitendo cha kukaaa madarakani Hadi aibu ilipomkuta ndio alipochemkia.
Na hakung'oka mwenyewe kama wengi tunavyodanganywa, maji yalimfika shingoni na aliambiwa ama ung'oke ama wananchi wako waendelee kuangamia, kanisa katoliki likamwabia pumzika urais uendelee kuwa mkuu wa chama staili ya Mao Tse Tung (Mao ze dong).

Mwenyewe akakiri kung'atuka maana alikuwa kang'ata.
 
Kawaida yao, ni makatili kupita kiasi, ila wanakujia na sura ya kuchekecheka ili kukuhadaa, take care, hata sasa wapo
Ukifanyika uchunguzi wa kina naamini hakuna mtu aliyeuwa raia wake kwa maamuzi ya kijinga zaidi ya nyerere.

Walikufa raia wengi sana wakati wa vijiji vya ujamaa yanafichwa tu. Natamani atokee mtu afanya utafiti wa kina wa athari za vijiji vya ujamaa wakati bado wapo waliobaki wa enzi hizo.

Binagfsi niliikimbia nchi enzi hizo, nikaona yanini tabu na raha ipo. nikasepa. Nashukuru kusepa, maana ile kukogea arita ilinishinda.

Nakumbuka kulikuwa na mti wa arita pale morogoro road, tukienda kuwahi kuziokota tuje kukogea ndiyo sabuni.
 
Ukifanyika uchunguzi wa kina naamini hakuna mtu aliyeuwa raia wake kwa maamuzi ya kijinga zaidi ya nyerere.

Walikufa raia wengi sana wakati wa vijiji vy aujamaa yanafichwa tu. Natamani atokee mtu afanya utafiti wa kina wakati bado wapo waliobaki wa enzi hizo.
Takbiiiiiiiiiiiiiiiir
 
- Ajabu kwako wahujumu uchumi unawaona wajanja kwa kuwaita walikuwa na akili za haraka, mindset yako na Nyerere ziko tofauti kabisa, hivyo sishangai ukimuona mkosefu. Jiulize; hao wenye akili za haraka leo wako wapi na wengine kule vijijini/mijini nao wako wapi kiuchumi? Jibu unalo.

hini ya Kanisa Katoliki kimchakato, hivyo naamini huna sababu yoyote ya maana ya kutumia jina hilo zaidi ya ujuaji ulionao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Umeongea mengi sana, lakini hebu tuzungumze kuhusu Uchumi wa Tanzania. Hivi wewe jamaa katika akili zako na kusoma kwako kote, kuna Raisi hapa nchini Tanzania aliyefanya kazi ya kufufua na kupaisha uchumi kama Mzee Mkapa?

Aliwezaje kufanya vile ndani ya muda mfupi ilhali alipookea nchi ikiwa haina mbele wala nyuma. Nini kilimfanya Mzee Mkapa kufufua uchumi hadi kuanza kukua kwa asilimia 7% kwa mwaka ? Mkapa alifanya jambo ambalo Mzee Nyerere hakuweza kulifanya kwa miaka yake yote aliyokuwa madarakani. Mbona mnataka kubishana na ukweli ambao uko wazi ? Mbaya zaidi, wakati Mzee Mkapa alikuwa anahangaika kufanya hivyo Mzee Nyerere na wajamaa wakaanza kumletea maneno.

Was Mkapa Right in his policy of privatization? Not totally, some things were excessively mishandled. Good thing is that President Mkapa made a public statement about this. The foolishness of believing that Juche could work in Tanzania in late 90's was really absurd and stupid. No country can ever succeed without free enterprise, you can bank on this.

Ukweli ni kwamba kama Mzee angeendelea kushikilia nadharia za kwamba lazima serikali ndiyo imiliki kila kitu ilhali tunafahamu taasisi nyingi za umma zilikuwa INSOLVENT asingefanikiwa hata kidogo. Mkapa alisaidia watanzania wengi mno kwenda hata shule kupata elimu. Wengi wenu mmeanza kusoma baada ya sera ya elimu ya mwaka 1997 kupitishwa ambayo ilipelekea ongezeko la wanafunzi mashuleni na vyuoni. Ni rahisi sana kusema, ila ukweli waliokuwepo walikiuona cha mtema kuni.

Kama unaamini kwamba kuna Raisi aliyefanikiwa kiuchumi nchini Tanzania zaidi ya Mzee Mkapa basi sitashangaa kwanini unachangia hivi unavyochangia.​
 
Back
Top Bottom