Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Wakati tunavaa viraka na kukosa mahitaji muhimu ilikuwa kipindi Cha ubepari?
Siku zote unapoanza safari ya maisha kuanzia chini usitegemee utafanikiwa katika kila jambo. Kumbuka pia tulikuwa na vita, labda kwa kuwa unadhani vita tunaisoma na kuona kwenye tv pekee tunaona ni kitu cha kawaida. Vita iliturudisha nyuma sana kiuchumi. Je, viraka na kukosa mahitaji muhimu yanahalalisha wizi na ufisadi?
 
Saa nyingine ni ego au kiburi tu, mtu anajua kabisa amekosea ila akijirekebisha hataki maana anaona atakuwa amejishusha mbele ya wakosoaji wake
Enzi zake ukimkosoa kidogo ilikuwa unapotezwa, msome Ludovick Mwijage alifanywa nini akaimbia nchi, kaandika vitabu viwili kuhusu hilo, kuna mtu aliweka hapa JF:

 
Serikali ni taasisi, Uraisi ni taasisi inayoongoza Serikali hivyo kupatikana kwa majawabu ni rahisi tu. Mambo yote ambayo Raisi Nyerere aliwahi kuyafanya yalianza katika ngazi ya kisera na baadaye kutekelezwa kupitia sheria. Hivyo kwasababu wengi walikuwepo kipindi hicho ni rahisi kufahamu nini kilikuwa kinaendelea hadi kupelekea serikali kutengeneza sera za namna ile na baadaye kuzitungia sheria kandamizi vile.

Mfano, mwaka 1967 wakati tunatanzanga Azimio la Arusha, sababu zilizotolewa ni kwamba jamii ya Tanzania ilikuwa haina usawa kutokana miaka ya ukoloni. Hivyo kujenga usawa na kuondoa matabaka ni lazima nyezo zote za uzalishaji (Major Means of Production) zitaifishwe ili serikali iweze kutoa huduma kwa kila mwananchi. Atleast this is understandable. Ila kwanini serikali ilitumia dola na sheria kandamizi kuhakikisha watanzania tunalala njaa na kukosa hata mavazi mwilini, kwa miaka mitano mfululizo sijapata majawabu yake.

Lengo lake haswa kutuona tukiishi kimasikini vile ilhali ilikuwa inawezekana kutuachia kutafuta mahitaji yetu ilikuwa inawezekana. Somethings defy ordinary human comprehension.
Nafikiri pengine ni uchanga wa kuendesha nchi ambapo kwa namna moja ama nyengine kiongozi atakuwa tu too idealistic. Kwa mfano uliyotoa kwa nchi tuliyochukua sera zao za kiujamaa wenzetu civilisation yao ni kubwa kwa maana imejengeka kwa miaka mingi. Hivyo kutakuwa na namna kwa wao kuwa rahisi kubadilika.

Nimejaribu tu kuwaza.
 
Nami nimepata mshangao wa kulitumia neno MTAKATIFU sijui anafanya dhihaka au nini. Kwa namna alivyo humu ndani jf na hiyo lugha anayotumia ndo hayo tunayosema madhaifu ya kibinadamu.
Wavaa kobazi wameungana kupinga Utakatifu wa Nyerere, Sasa wanaanza kumuita Mtakatifu kwa kejeli kabla ya Muda

Bila Nyerere Hawa wavaa kobazi hata hiyo Elimu wasingekuwa nayo ,

Wanatakiwa wamuheshimu sana
 
Kiongozi lazima awe na principles zake, kusimamia kile anachokiamini mpaka mwisho, kiongozi asiye na msimamo ndie chanzo cha kuyumba kwa taifa lolote hapa duniani, leo atashika hiki atakiacha, kesho atashika kile nacho atakiacha...

Kulalamika miaka yote ya Nyerere kuwepo madarakani halafu bado hali ya maisha ya mtanzania ikaendelea kuwa mbaya, kwangu sioni kama kuna mantiki yoyote, kwasababu siku zote mabadiliko hayaji kwa usiku mmoja, ni mchakato.

Sasa ndani ya kipindi hicho cha mchakato ndicho kinamfanya kiongozi aendelee kusimamia kile anachokiamini, akiamini atafikia malengo, kama kikija kuwa na matokeo tofauti hayo ni mambo ya kibinadamu, kwamba alikosea, na ndio maana akawapisha wengine.

- Lakini unaposema Nyerere hakuwa na huruma na watu wake unakosea, alikuwa na huruma kupitiliza.

1. Hakujilimbikizia mali yoyote, licha ya madini na kila aina ya rasilimali tulizonazo.

2. Aliwahi kukaririwa akisema; "kiongozi unapita barabarani, unaona hali ya mtanzania ilivyo mbaya, unajua hili ni jukumu langu kumuondoa hapo alipo".

3. Hakuna hata mtoto wake mmoja tunayesikia amewahi kuhusishwa na wizi/ufisadi wa aina yoyote.

Mpaka hapo naamini utapata picha Nyerere alikuwa kiongozi wa aina gani, kwamba licha ya sera yake ya ujamaa kufeli, lakini dhamira ya dhati ya kumkomboa mtanzania toka kwenye lindi la umasikini alikuwa nayo tofauti na ulivyoandika.

Above all, hivi umewahi kujiuliza baada ya Nyerere kuondoka madarakani nini kilifuatia?

Kilichofuatia ndicho kile ambacho Nyerere alikipiga vita na wewe unaonekana kukifurahia, binafsi nchi hii naamini hakuna mabadiliko yoyote ya maana kiuchumi zaidi ya kuwepo pengo kubwa kati ya walio nacho na wasio nacho, hili Nyerere na Sokoine ndio walikuwa wakilipinga.

- Hii kwangu ni sawa na kusema, licha ya kumuona Nyerere alifeli, lakini hata hao waliofuatia baada yake nao wamefeli pia, hatuna cha maana cha kujivunia, mgao wa umeme, ukosefu wa maji safi na salama, wanafunzi kukosa matundu ya vyoo shuleni na madawati, mambo ni mengi...

Labda uniambie tu kwa sasa unafurahia uwepo wa unga, sabuni, mchele na mahitaji mengineyo mitaani, lakini ukweli wa mambo ni kwamba, licha ya uwepo wa vitu hivyo, bado hali ya mtanzania kiuchumi ni mbaya na ndio maana mpaka leo bado wapo ndugu zetu vijijini wakisubiri kampeni zianze, ili wagaiwe t-shirts na kofia za CCM ziwastiri.

Hivyo kwangu, kumlaumu Nyerere kwa kufeli bila ya kunionesha yule aliyefaulu hapa ndani kwetu sikuelewi, na kutumia mifano ya nje kumhukumu Nyerere bila kunionesha nani aliyefuatia wa hapa ndani akafaulu, umemuonea, that's unfair comparison.

Unless uniambie mahitaji yetu siku zote yangebaki yale yale ya unga, mchele na sabuni kupatikana madukani, jambo ambalo kwangu halina mantiki, naamini mahitaji hubadilika kulingana na wakati, na pale unaposhindwa kuwapa watu wako kile wanachohitaji kwa wakati husika, basi umefeli, there is no way out.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
to
Mimi kinachonishangaza ni huyu wa sasa ambaye hana uwezo lakini bado tu anangangania.
Tunazungumza ya zamani wakati ya Sasa yanatushinda.👩‍⚖️
 
Nyerere alikuwa na dira na maono yake.

Na aliyapambania hata Kama mengine yalikwama.

Tena amefariki dira yenu Sasa hivi ni ipi zaidi ya kuuza kila kitu na kuvimba MITUMBO.

Nyerere hakuiba kitu, kaacha nchi Bikra kabisa. Hata Kama alifeli, mmeshindwa nini kupiga hatua miaka 35 Sasa??

Mtoa maoni kaweka rejea yoyote?

Nyerere ambaye alikuwa anasamehe kina Bibi titi, Kambona na Abdul Jumbe??

Mtu asiye na utu ni Kama Kikwete kung'oa meno Ulimboka au Kutandika risasi Kama unaua chatu alikofanya Magu.

Wafuasi wa Nyerere ni Nani Sasa hivi kwenye mfumo?

Maana kina Madaraka, Butiku, WARIOBA hawana usemi kwa Sasa?

Acheni visingizio mavi ya bata.

Biashara yangu ya bata inahusiana nini na uzi juu
 
Wavaa kobazi wameungana kupinga Utakatifu wa Nyerere, Sasa wanaanza kumuita Mtakatifu kwa kejeli kabla ya Muda

Bila Nyerere Hawa wavaa kobazi hata hiyo Elimu wasingekuwa nayo ,

Wanatakiwa wamuheshimu sana
Hao wavaa kobazi ndio waliompokea na kumlea Nyerere.

Nyerere hazungumzwi kwa sababu ya ukatoliki wake. Kichwa unacho kazi yake ni kufikiri sio kujaza kinyesi
 
Huwa najiuliza sana lakini sipati majawabu, lakini naomba wasomi wa humu ndani mnisaidie.

Hivi Mzee Nyerere alikuwa ana roho ya namna gani kuona mambo kama haya yakitokea kwa wananchi lakini bado hataki kubadilika na akaendelea kutumia mkono wa chuma kuhakikisha anasigina kabisa uwezo binafsi wa mtanzania kuweza kujikwamua kiuchumi. Ujamaa wa Tanzania hakuleta matokeo yoyote makubwa na ya kuchangaza ukilinganisha na kule Asia na Ulaya ambako walau walifanya mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Uchina walifanikiwa sana baada ya Raisi Deng Xiaping kuanza kuwaonea huruma raia wake akifahamu kabisa kwamba njia waliyokuwa wanaenda ilikuwa siyo sahihi. Aliruhusu watu waanze kumiliki mali zao binafsi na kufanya biashara. Najiuliza sana, miaka yote 18 ya Ujamaa, yalifanyika na kutokea mambo mengi mno kwa watanzania, kiasi kwamba kiongozi yoyote mwenye huruma na wananchi ni lazima angekaa chini na kujifanyia tathmini, lakini Raisi Nyerere hakufanya hivyo, aliendelea kuwa na moyo mgumu kama Farao. Hebu tuzingatie haya:

1. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.

Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.

Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirudi.

Hivi kwanini MTAKATIFU na MWENYEHERI, Raisi Nyerere hakuwa na chembe ya huruma moyoni ?
Kuna mambo nikikumbuka huwa naumia sana na nakosa majawabu. Hivi alikuwa anapenda kutuona sisi vile ?​
Wapigania uhuru wa Afrika hawakuwa viongozi wazuri wa nchi zao baada ya uhuru kupatikana, na sababu ni nyingi miongoni mwa hizo ni :-
1-Azma yao kubwa ni kujitawala, lakini utaalamu wa kujitawala walikuwa hawana.
2-Uendelezaji wa uchumi kutoka katika nidhamu ya kikoloni kwenda katika mfumo wa kitaifa uliaathirika.
3-Ukosefu wa wataalamu wazalendo katika fani mbalimbali.
4-Kutofautiana wenyewe kwa wenyewe katika njia gani ya kendesha nchi (ujamaa au ubepari).
5-Tofauti za kikabila, kiimani na hata kichama ziliweza kuwagawa baadhi ya viongozi.
6-Vita vya wenyewe kwa wenyewe.
7-Wakoloni kuwacha vibaraka wao kwa maslahi yao.
8-Elimu duni kwa wananchi.
9-Kuwasaidia wengine ambao waliyokuwa wakiishi chini ya ukandamizwaji ilhali uwezo wa kusaidia ni mdogo.
 
Ila Nyerere naye kwa maigizo alikuwa hajambo. Anapanga mstari kuwa anachagua kiongozi, lakini tayari alikuwa na matokeo mfukoni! Ogopa kiongozi aliyekuwa anaamini kiongozi wa kweli atatoka ccm, yaani Hawa watoto wa kina Mwigulu ndio Nyerere alimaanisha hao!
Kawarithisha na wengineo.
20230616_214620.jpg
 
Nadhani swali kubwa zaidi kujiuliza ni kwa nini pamoja na mateso yote waliyopitia watanzania, bado aliendelea kuwa na ushawishi mkubwa hata baada ya kutoka madarakani na pia kifo chake kilitia simanzi watu wengi haswa maskini waliokuwa wanateseka zaidi.

Kingine cha kujiuliza ni kwa nini baada ya kifo chake, kulitokea mabadiliko makubwa haswa kuleta mfumo wa soko huria lakini bado viongozi waliopo hawajapata imani ya wananchi tofauti na enzi hizo za mateso na wala nchi haijapiga hatua kama nchi ulizozitolea mfano.

Binafsi yangu naamini Nyerere alifanya makosa mengi lakini dhamira yake haikuwa mbaya maana hakunufaika financially kwa yote aliyoyafanya hivyo, alijaribu kujenga misingi ya Tanzania ya ndoto yake tofauti na sasa nchi inavyojiendea bila kuwa na direction.

Naamini pia yeye kuona ugumu na kuuvumilia si kwamba alikuwa haumii ila aliichukulia kama gharama ya kutimiza malengo kama yeye na watu wengine walivyoumia kama gharama ya kuleta uhuru 🙏🏽
Mkuu Eyce, Merry Christmas to you Brother,

Mzee Nyerere is a controversial, enigmatic, mysterious and polarizing figures. Wengi wanamkubali na wengine hawamkubali, hasahasa kizazi ambacho kiliyaishi makosa ambayo aliyafanya Mzee Nyerere. Huu ndiyo ukweli mchungu. Kukosea kila mtu anakosea hapa duniani, jambo ambalo linanitatiza ni kwamba hata baada ya kuiingiza Tanzania vitani dhidi ya Uganda na kuifilisi Tanzania, Raisi Nyerere hakukubali makosa na akaendelea kutumia mkono wa chuma kudhibiti watanzania ambao walionekana kutoridhika na ile hali. Kwanini hakutaka kubadilika hata baada ya kuona watanzania wako kwenye lindi kubwa la umasikini ambao ulisababishwa na sera zake?

Miaka mitano ya mwisho ya Mzee Nyerere ilijaa taharuki mambo ya kuogopesha kuwahi kutokea Tanzania. Wengi hawafundishwi lakini Tanzania ilipitia changamoto nyingi za kiusalama, na ziliondoka punde tu baada Mzee Nyerere kung'atuka madarakani. Hebu tupitishane kwa harakaharaka.

1. Utekaji wa ndege uliofanya na vijana waliotaka Raisi Nyerere ajiuzulu.
2. Mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na maafisa wa jeshi waliotaka Raisi Nyerere auawawe.
3. Uasi kanda ya ziwa, maafisa wa kijeshi huko mkoa wa Mara walianzisha nchi yao iitwayo Jamhuri ya Chui.
4.Mzee Nyerere anamrudisha Waziri Mkuu Sokoine madarakani huku akilalamika kwa Samora kwamba wanapishana.
5. Kuna minong'ono kwamba kuna chama cha kisiasa kinataka kuanzishwa na kina mahusiano na taifa la Ujerumani Mashariki.
6. Harakati za kusaka wahujumu uchumi zinaanza ambapo chama kiligawanyika na Sokoine katishia hadi maaskofu.
7. Waziri Mkuu anauwawa kwa ajali, jambo ambalo siyo kawaida kwenye msafara wake. Postmertem haikufanywa.
8. Nyerere anazungukwa na wajanja kina Thabiti Kombo ambao wanamwambia Mwinyi akubali kuwa Raisi.
9. Aboud Jumbe ameshinikizwa kwamba Zanzibar ijitoe kwenye muungano na anawekwa kizuizini.

Watanzania ni watu wenye utulivu mno, ukiona hadi wamefikia hatua ya kutumia jeshi, vurugu na kukuzunguka kisiasa, suala zima la kukubalika kwa Mzee Nyerere linatutia wengi ukakasi. Mwishoni Mzee alishindwa kuidhibiti dola na chama, watu wakawa wanamfanyia hujuma waziwazi. Nini kilipelekea hili kutokea ?​
 
Kwenye hili Nyerere alikuwa ndiye bingwa. Alikuwa kila anayemkosoa anahama nchi. Ni vile tu ukweli hausemwi na bahati mbaya Nyerere katawala ktk kipindi ambacho media outlets zilikuwa hakuna.

Redio ya taifa ilikuwa inaandikiwa nn cha kusema kuhusu rais kwenye taarifa ya habari.

¶ Nyerere ndiye aliyefanya Kambona kuishi ukimbizini maisha yake yote.
¶ Nyerere ndiye aliyechana vyeti vya Tuntemeke Sanga.
¶ Nyerere ndiye aliyemfunga kifungo cha nyumbani (alimuweka kizuini) Kasangatumbo
¶ Nyerere ndiye alimuondoa kwenye urais Abdul Jumbe halafu akamuweka kizuizini hapo Kigamboni mpk umauti.
¶> Nyerere ndiye aliyetunga hili katiba bovu lililomfanya yeye kujipa umungu wa Tanzania.

Nyerere ni dikteta asiyesemwa.
Nyerere alikuwa tapeli na kibaraka kama alivyo sema Nkwame Nkrumah
Ndie aliye sababisha hatuna umoja wa Africa kama state badala yake akaleta regional blocks,
Ndie aliye asisi hili joka kuu Muungano na first born CCM,
Ndie aliye asisi mfumo wa chama kimoja kwa Tamaa zake mbaya(zidumu fikra za mwenyekiti),
Ali asisi ujamaa wa kitapeli wa kuua baadhi ya mahasimu wake kiuchumi.
Alikuwa sehemu ya mauaji ya Lumumba na Yule mawanaharakati wa msumbiji pale morogoro.
Japo hakuna ushaidi wa kuwa na Tamaa za pesa nyingi kama Mobutu, alikuwa na Tamaa
Za sifa entitlement kuwa ana akili.
Kwangu mimi huyu ndio anabeba lawama zote za mema na mbaya yaliyopo bongo
 
Na hakung'oka mwenyewe kama wengi tunavyodanganywa, maji yalimfika shingoni na aliambiwa ama ung'oke ama wananchi wako waendelee kuangamia, kanisa katoliki likamwabia pumzika urais uendelee kuwa mkuu wa chama staili ya Mao Tse Tung (Mao ze dong).

Mwenyewe akakiri kung'atuka maana alikuwa kang'ata.
Hilo liko wazi kuwa aling'oka kwa aibu.
 
Ubepari ni ushetani. Wewe una njaa lakini mwenzako anasaza bila huruma ndivyo tunaishi hivyo kwa sasa. Ujamaa unataka wote muende pamoja hata mtu wa mwisho kabisa naye awezeshwe ndio maana tunaita ujamaa ni utu. Hamuoni licha ya matatizo tuliyonayo lakini mtu yupo radhi awe na fedha ambazo hatomaliza milele? Watu wanamiliki magari na majumba ya kifahari na ni viongozi wa serikali na kulipwa fedha nyingi ukiachia mbali kuiba lakini watu wanakosa huduma muhimu?
Asiyefanya kazi na asile....ndio kanuni insyofanya watu wajitume na kupelekea uvumbuzi mbalimbali duniani wa kurahisisha kazi na kuleta uhuru kwa mtu binafsi.... binadamu hawawezi kuwa sawa kwa sababu sio mifugo
 
Hii nayo ni mojawapo na setbacks kwenye uongozi wa Nyerere, mleta mada badala ya kutumia muda mwingi kuhukumu tena kwa kutumia mifano nje, nadhani angejielekeza pia kwenye changamoto za kila awamu ili tupime awamu ipi ilikuwa na changamoto nzito zaidi ya nyingine, kisha tuone yupi alikuwa mzembe zaidi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Vita ya Kagera kisababishi ni Nyerere mwenyewe kwa uchokozi wake, akiingilia siasa za Uganda kwa kufadhili na kuwahifadhi waasi wa Obote ambao walikuwa wanaenda Uganda kujaribu kumuua Idd Amini
Ila History ya ki propaganda inasema Idd Amin aliibuka tu bila sababu yoyote kuja kuvamia Tanzania
 
Back
Top Bottom