Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Mkuu, ni hatariii.....Ngoja nikupe kisa changu kilichonipata katika hizo pilika.

Kwanza nilivutiwa na jamaa fulani hivi tukiwa Mbeya huko wilaya XYZ,jamaa walifankkiwa kuopoa sanduku la dhahabu kwa Style hyhy ya kusaka Mali za wajerumani. Walikula bata sana na hadi muda huu ni malordilofa,yaani pesa bado wanayo.

Basi bhana,nikasafiri hadi wilaya kwa wajomba zangu baada ya kujifunza Code chache ambazo wajelumani walitumia kama alama na nikagundua hivi vitu nilivionaga kwa wajomba zangu nikiwa nachunga ng'ombe milimani.

Nilipofika kwa babu,nikanyoosha msituni kwenda kuhakiki kama zile alama kwenye miti,mawe na michoro kama ipo, bahati nzuri bhana nikavikuta kama vilivyo,wala havijaharibiwa sana na waharibifu wa mazingira. Nikashauriana na vijana wa pale tukaanza utaratbu wa kuchimba.

Huku tukiendelea kukutana na code na ninazisoma vizuri na kusonga mbele,baada ya siku 6 hatimaye tukalifikia sanduku bhana....!! Tulichokiona humo......mmamaye ,nikikumbuka huwa hata sijielewagi,maana ni hatari.

Tulikutana na marehemu mzungu humo.....ashamong'onyoka kawa unga tu,sijui walimtia nini hakuoza,kawa vumbi tu na mifupa, hilo vumbi likaingia vifuani, tulikohoa karibia ya kunya......!!!!

Aisee.....tulirudi nyumbani tukatengeezwa kienyehi ndio mambo yakawa sawa, lakini kuna mzee akasema mgetoa lile sanduku ndio mgekutana na mzigo wenyewe....!! Alinistua mbaya,lakini cha ajabu,nasema tena chaa ajabu niliporudi kule porini ile sehemu sijaikuta na wala sikuiona tena hadi leo, nilienda takribani mara 6 kwa siku tofauti lakini mpaka leo sipajui eti.....!!

Kuna sehemu tena nipo ugenini,nilikwenda kucheki shamba la kununua nimekutana na code tena za ajabu aisee.....!!! Sasa sijajua nini wameficha...!!

Kwanza nilikuta Mti mkubwa una mzizi upo nje,mzizi huo umetobolewa,nikaufuatilia kidogo nikakuta tobo la pili, nikaendelea kufukua nikakuta nikakuta tena mzizi umekunjwa kuelekea direction ya kusini,nikaendelea kuufuata, mbele ya huo mzizi kulikuwa na jiwe kubwa sana kama tani 30 hivi, nilipolizoom vizuri kabisa na kulichunguza,nikagundua kuwa huyo ni picha iliyojchongwa picha ya bundi...!!!! Nikafukuafukua kuzungua hilo hiwe nikakuta ramani aisee.....!!! Bahati mbaya sijui kijerumani .

Mzee nikaazimia kazi, tukaenda kwa mchawi wetu akasema kuna mzigo wa kufa jamaa....vizuri vyote ruby,gold na sapphire akasema zipo. Akatupa masharti tukaingia mzigoni...!!

Baba tumefungua ardhi huku tukifuata masharti makamanda tulikuwa 6, tuliikosea ramani kidogo tukajikuta kuna mwamba una ninginia juu yetu.

Tulichokifikia ni kwanza kuna vigae vya mawe vimefunika kitu tusichokijua hapo chini, pili kuna ukuta umejengwa kwa mawe ya kupondekezwa hapo chini shimoni...!!

Tuliogopa kupondwa na tulikuwa tumechoka sana,maana kazi ilikuwa ya ngumu na ilituchukua miezi 3,tukasema labda tusake katapila.


Sasa tumeliacha tu na tumeamua tulime tu kwanza lakini tukiwa na matumaini kwamba ipo siku.
Sasa najiuliza,au tutakuta marehemu mzungu tena au la ....nakaribisha wadau,kama unaweza kuleta Scaveta njoo tujaribu bahati.





Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ntakutafuta nje ya jf unipe habari Zaid,huwa napenda Sana hizi habari
 
Kuna jamaa alikuwa anawinda mbugani na baba yake wakapita sehemu wakakuta mawe mengi ya dhahabu yamerundikwa kwenye mti wa mwembe, hawakuyatilia maanani wakaendelea na uwindaji walipo rudi kijijini wakawasimulia watu. Watu walivyo sikia hivyo wakambembeleza kijana awapeleke. Kabla kijana hajawapeleka wakaenda kwa kwa mganga kupiga ramli.

Mganga akawambia waende ila anaona giza mbele ya huyo kijana anayewapeleka. Wakasisitiza japo kijana aliogopa. Basi mganga akawambia wakifika kuna kitu kitatokea ila wasiseme neno lolote.

Story ni ndefu ila nitaifupisha.

Walipokaribia kwenye ule mti kweli waliziona zile dhahabu ghafla kikatokea kimbunga kikali kikamyanyua mzee moja. Mkwe wa yule mzee kuona hivyo akasema "haiwezekani baba mkwe aende"

Ghafla walitokea nyani kusiko julikana wakawapa kichapo si cha nchi hii alafu ikanyesha mvua kubwa hawajawahi kuona. Ikaharibu chakula chote walicho kuwa nacho.

Ilikuwa ni safari ya siku nne kurudi bila msosi

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuu!!!
 
Wadau haya mambo nimeshiriki sana kweli vitu vipo nimefika ktk eneo husika sema kutoa mzigo ni shughuli na mpaka niliamua kuacha kwasababu unapoteza muda mwingi na pesa kufuatilia but kuna eneo najua kuna mzigo ila kuchukua sasa ni kugumu nimekutana na huo.ugumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikutana na mauza uza gani?
 
Wacha kudanganya watu, hakuna mdini yoyote kwenye hizo heller zaidi ya shaba. Hizo zinauzwa kwa "collectors" wa sarafu almaaruf "numismatics".

Thamani zake hizi hapa: German East Africa Heller KM 7 Prices & Values | NGC

Kuna utapeli wa siku nyingi toka miaka ya 70 kuhusu pesa za kizamani. Huu utapeli unakwenda na kurudi. Naona sasa mmeamua kuileta kwenye mtandao.

Yeyote atakae kufanya shughuli za sarafu za zamani azame eBay tu.

Umenikumbusha story ya yule jamaa alieanzisha uzushi huu, kijijini akampeleka Bibi aliekua anawauzia watu halafu wakija mjini wanaziuza kwa jamaa, kumbe jamaa alikua anazirudisha kule kijijini. Demand ilivyokua inaongezeka na bei inapanda, watu wakaenda kukopa wakanunua kwa yule bibi kwa gharama kubwa, walipofika town mnunuzi hayupo, waliporudi kijijini Bibi nae hayupo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Lupembe alikuja dada mmoja wa kizungu Kama volunteer akawapanga wanakijiji wachimbe shimo,walipofikia urefu flani akawaambia Basi inatosha,usiku akamalizia kuchimba akaamsha hajaonekana mpaka leo
Hiyo si Amini kbs!!! Jee viongozi na mweyekiti was Kijiji walipewa pombe wanted????
 
Ndugu zangu wanajamvi.
Nimekuwa katika utafiti wa mali kale na mambo ya asili kwa muda mrefu.
Katika utafiti wangu nimekuja kugundua wajerumani wameficha mali nyingi sana kawenye ardhi ya Tanzania.
View attachment 1022278

Wakati wa utawala wa wajerumani kulikuwa na fedha ambazo zilikuwa zikitumiaka.
Heller na Rupee zilikuwa zikitumiaka. Coin hizo zilikuwa na madini mengi sana tofauti na coin za sasa.
Kwa mfano 1 Heller kwa sasa inauzwa kwa $900 - $1000.
View attachment 1022271

View attachment 1022276

Kwenye vita vya kwanza vya dunia wajerumani walizichimbia hizo mali sehemu mbalimbali kwenye ardhi ya Tanzania kwa ustadi mkubwa.

Katika tafiti nilizozifanya mpaka hivi leo. Maeneo yafuatayo na mengine mengi ndiko zilipogichwa mali hizo. Inatakiwa kujua sasa ni eneo gani masanduku yenye mali yalichimbiwa:-

  1. Ikombe
  2. Mibirizi
  3. Kasanga
  4. Ilembule
  5. Rombo
  6. Nyakanazi
  7. Uvinza
  8. Mlalo
  9. Kisarawe
  10. Kazimzumbwi
  11. Kirondatal
  12. Tukuyu
  13. Leganga
  14. Igulwa
  15. Ushetu
  16. Mnazi
  17. Mikese
  18. Shume
  19. Lumbira
  20. Mbulu
  21. Nansio
  22. Sekenke
  23. Galula
  24. Liuli
  25. Manda
  26. Lushoto
Hizi ni sehemu kadhaa zinazohitajika utafiti wa kina ili kujua ni sehemu zipi mali hizo zilifichwa.

Asanteni
Mkuu mwaka juz jamaa flan raia wa Germany walikuja Lindi ktk ofisi ambayo ilikua ya utawa wa Germany enzi hizo wakazuga kua wanaboresha ili kufanya hotel ya kitalii usiku walikua wanawasha moto kumbe walikua wanalainisha zege
Dah kuja kustuka jamaa washasepa na sanduku kibao za Heller zilifukiwa chini ya ilo jengo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliwaona pindi wanazika? Mbona husemi kuwa babu zako walizika mali nyingi? Acheni akili za kijinga hakuna mambo kama hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu Kapalamsenga Tanzania ni kubwa sana, mambo mengine ikiwa unayasikia kwa mara ya kwanza na huyajui ni bora kunyamaza tu! Kama una akili utanielewa!
 
Ndugu yangu Kapalamsenga Tanzania ni kubwa sana, mambo mengine ikiwa unayasikia kwa mara ya kwanza na huyajui ni bora kunyamaza tu! Kama una akili utanielewa!
Kuna wakati huko Mwanza kulitakiwa kujengwe rada ya hali ya hewa. Sasa bicon iliwekwa tangu Mjerumani anatawala Bongo watu waliozaliwa 80s wakavamia eneo wakajenga. Wamekuja serikali kujenga rada watu wakaanza ubishi wakaletewa nyaraka kuwa bicon ipo humo ndani tangu 1920

Sent using Infinix hot 4
 
Back
Top Bottom