Kuna jamaa alikuwa anawinda mbugani na baba yake wakapita sehemu wakakuta mawe mengi ya dhahabu yamerundikwa kwenye mti wa mwembe, hawakuyatilia maanani wakaendelea na uwindaji walipo rudi kijijini wakawasimulia watu. Watu walivyo sikia hivyo wakambembeleza kijana awapeleke. Kabla kijana hajawapeleka wakaenda kwa kwa mganga kupiga ramli.
Mganga akawambia waende ila anaona giza mbele ya huyo kijana anayewapeleka. Wakasisitiza japo kijana aliogopa. Basi mganga akawambia wakifika kuna kitu kitatokea ila wasiseme neno lolote.
Story ni ndefu ila nitaifupisha.
Walipokaribia kwenye ule mti kweli waliziona zile dhahabu ghafla kikatokea kimbunga kikali kikamyanyua mzee moja. Mkwe wa yule mzee kuona hivyo akasema "haiwezekani baba mkwe aende"
Ghafla walitokea nyani kusiko julikana wakawapa kichapo si cha nchi hii alafu ikanyesha mvua kubwa hawajawahi kuona. Ikaharibu chakula chote walicho kuwa nacho.
Ilikuwa ni safari ya siku nne kurudi bila msosi
Sent using
Jamii Forums mobile app