Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Waliamriwa waondoke na koloni likachukuliwa na mwingereza
Hakika waGerumani ni TAIFA lenye maendeleo, Elimu,technolojia na Akili na uwezo mkubwa usio na mfano!!! Hivi Sasa bila wao (GER) mmmmmh .... Naona tunajidanganya!!!
 
3333.PNG
 
Ndugu zangu wanajamvi.
Nimekuwa katika utafiti wa mali kale na mambo ya asili kwa muda mrefu.
Katika utafiti wangu nimekuja kugundua wajerumani wameficha mali nyingi sana kawenye ardhi ya Tanzania.
View attachment 1022278

Wakati wa utawala wa wajerumani kulikuwa na fedha ambazo zilikuwa zikitumiaka.
Heller na Rupee zilikuwa zikitumiaka. Coin hizo zilikuwa na madini mengi sana tofauti na coin za sasa.
Kwa mfano 1 Heller kwa sasa inauzwa kwa $900 - $1000.
View attachment 1022271

View attachment 1022276

Kwenye vita vya kwanza vya dunia wajerumani walizichimbia hizo mali sehemu mbalimbali kwenye ardhi ya Tanzania kwa ustadi mkubwa.

Katika tafiti nilizozifanya mpaka hivi leo. Maeneo yafuatayo na mengine mengi ndiko zilipogichwa mali hizo. Inatakiwa kujua sasa ni eneo gani masanduku yenye mali yalichimbiwa:-

  1. Ikombe
  2. Mibirizi
  3. Kasanga
  4. Ilembule
  5. Rombo
  6. Nyakanazi
  7. Uvinza
  8. Mlalo
  9. Kisarawe
  10. Kazimzumbwi
  11. Kirondatal
  12. Tukuyu
  13. Leganga
  14. Igulwa
  15. Ushetu
  16. Mnazi
  17. Mikese
  18. Shume
  19. Lumbira
  20. Mbulu
  21. Nansio
  22. Sekenke
  23. Galula
  24. Liuli
  25. Manda
  26. Lushoto
Hizi ni sehemu kadhaa zinazohitajika utafiti wa kina ili kujua ni sehemu zipi mali hizo zilifichwa.

Asanteni
Hii heller mimi ninayo nielekeze sehemu za kuuzia mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msituni wa nou ulioko mpakani mwa mbulu na babati kijiji cha erri kuna mashimo hayo ya wajerumani katika kitongoji kinachopakana na kijiji cha merr.kazi kwenu wa tafiti.kwa u sahihi zaidi tafutamimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha story ya yule jamaa alieanzisha uzushi huu, kijijini akampeleka Bibi aliekua anawauzia watu halafu wakija mjini wanaziuza kwa jamaa, kumbe jamaa alikua anazirudisha kule kijijini. Demand ilivyokua inaongezeka na bei inapanda, watu wakaenda kukopa wakanunua kwa yule bibi kwa gharama kubwa, walipofika town mnunuzi hayupo, waliporudi kijijini Bibi nae hayupo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hiyo noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadithi za kubuni hizi! Wajerumani waliitawala Tanganyika ili kuvuna mali zilizopo Tanganyika na kupeleka kwao Ujerumani na sio kuchukua mali zao kutoka Ujerumani na kuzificha Tanganyika.
 
Bado watu wanaibiwa kwa hizi story za kusadikika za kale.. kweli wajinga hawaishi
 
Ha ha ha... Dunia hii unaweza mfukuza mGermani au (mzungu)?? Hehehe wataka tufe njaa!! Au tuwe was Pole kea nafsi zet......
Hawa jamaa walipoona wanakaribia kushindwa vita walianza kutafuta mbinu ya kuficha mali zao na kweli baada ya kushindwa vita ilibidi waondoke na kumwachia Mwingereza koloni(hawakuruhusiwa kubeba mali yoyote),inasemekana kuna mitego ya kila aina kwenye hayo mashimo ikiwemo milipuko,mitego ya mawe,gas zenye sumu nk.

Bila ramani ya sehemu husika na codes zao hutoi kitu ndo maana waswahili wanaishia kupoteza muda tu lakini vitukuu wao wakija wanatoa mizigo kiulaini kabisa.
 
Suali moja tutafakari ?!!? Wajerumani walikuwa wakipigana Vita na wahasimu wao au walikuwa bizee kuficha Mali.??? Ha ha ha Yaani wapoteze ipi?
FYI, Rasilimali zipo ardhini pote Duniani tatizo ni gharama za kutoa humo NI kubwa Sana!! Hakuna aiwezae!!
 
Ukitaka kufirisika na kupata uchizi ingia kwenye hiyo biashara. Kila mali kale utakayopata utaambiwa siyo. Ukipata hiyo Heloler watakuambia mwaka siyo tunataka ya 1890, ukiipata utaambiwa hap[ana hii imechubuka, mara ilihusisha kifo nk. Utaambiwa kuna pasi, ukiipata watakuambia aah! siyo hii ya mkaa, ipo ya mvuke... Mara utashangaa unapata stress utaota mvi hadi kwenye nyusi.
Hii inanikumbusha kuna jamaa alikuja mtaani akawa anataka tumtafutie shilingi 20 yenye mwaka 1993 kuna anaihitaji na angeweza kutupa milioni 5....dah tulitafuta kuanzia madukani kwa wauza sigara karanga urembo kote tunapata ya mwaka 1992 ilikua balaaa tukakata tamaa hatukupata kwahiyo hizi stori zinachanganya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suali moja tutafakari ?!!? Wajerumani walikuwa wakipigana Vita na wahasimu wao au walikuwa bizee kuficha Mali.??? Ha ha ha Yaani wapoteze ipi?
FYI, Rasilimali zipo ardhini pote Duniani tatizo ni gharama za kutoa humo NI kubwa Sana!! Hakuna aiwezae!!
Kwa akili zako ukisikia vita kuu ya dunia basi unachofikiri ni kwamba kila binadamu anakuwa vitani na kila kona ya dunia ni vita tu si ndiyo?
 
Hii inanikumbusha kuna jamaa alikuja mtaani akawa anataka tumtafutie shilingi 20 yenye mwaka 1993 kuna anaihitaji na angeweza kutupa milioni 5....dah tulitafuta kuanzia madukani kwa wauza sigara karanga urembo kote tunapata ya mwaka 1992 ilikua balaaa tukakata tamaa hatukupata kwahiyo hizi stori zinachanganya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom