Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Mimali ya thamani iliyopo ardhi ni ambayo hiyo hiyo ndiyo waliifata Wajerumani inawashinda wanakuja akina Barick kuisomba nyie mnataka kuleta utapeli wa sarafu.

Haiwezekani Hawa wazungu mbumbumbu wa leo wakina BARICK waweze kuja kubeba mali nyingi namna hiyo ya dhahabu halafu watu wenye akili kama wajerumani wasiwe wamechukua dhahabu kutoka bongo!! Wajerumani walisomba madini mengi sana na yale ambapo yaliwashinda kubeba baada ya vita ndio hayo waliyoyaficha sehemu mbali mbali nchini.

Nakumbuka wazee wazamani wakisimulia habari hizi! Kule TUKUYU kwa mfano inasemekana wajerumani walitupa mali nyingi sana kwenye mto Kiwira sehemu moja inaitwa KIJUNGU [ sehemu hii ina kina kirefu sana]. Kuna mzee mmoja sasa marehemu inasemekana yeye alikuwa anaweza kuzama sehemu hiyo sasa sijui kama kuna mtu anaweza shuhuri hiyo hivi leo, kwani inasemekana kuzama sehemu hiyo kuna matambiko yake!!
 
Sasa tumeliacha tu na tumeamua tulime tu kwanza lakini tukiwa na matumaini kwamba ipo siku.
Sasa najiuliza,au tutakuta marehemu mzungu tena au la ....nakaribisha wadau,kama unaweza kuleta Scaveta njoo tujaribu bahati.
Sio Nkasi huko ,maana rafiki zangu walikua huko mwaka juz walichimba sana ,wakawa wanasubili Mtambo gani sijui wa kumalizia kazi sijapata ripoti zao tena
 

Huu ni uvumi usio na ukweli wowote. Binafsi nimeshuhudia baadhi ya marafiki zangu wakifilisika kutokamna na huu upuuzi. kuna mmoja alifukuzwa kazi yake ya Jeshi kwa kuwa alikuwa bise kutafuta hazina ya kijeruman. Haingii akilini mjerumani pamoja na level ya maendeleo aliyoifikia eti achimbie "hazina" chini. tena atafute "majini na vinyamkela" vya kulinda.

Kama yeye alifukia kwa nini asije tu wakati huu kuifukua hazina yake? Watch out mtawapa waganga fedha za bure, mtawalipa watu wa kuchimba fedha za bure. Tafadhali ukiona jamaa yako anaota hizi ndoto mzindue hata kwa kumpiga kofi atakushukuru kesho kutwa.
 
Nashukuru kwa kujua chimbuko la msamiati maarufu wa kiswahili na katika mtandao wetu pendwa wa jf, neno "hela" kumbe lilitoholewa kwenye neno la kijerumani lililokuwa linawakilisha pesa enzi za ukoloni yani "heller"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…