BInafsi sijawahi kutamani wala kufikiria kuhusu haya mambo ya mali kale,lakini naamini na nathibitisha kabisa zipo
Babu yangu alishawahi kuniadithia sana kuhusu haya mambo maana yeye ndo alikuwa anajishughulisha na haya mambo
Na anasema enzi za ujana wake, walifanikiwa kupata mali nyingi sana na walikuwa matajiri kweli,sema walianza kufilisika taratibu baada ya kukosea miongozo flani
Kipindi ananiadithia alikua akinificha baadhi ya Siri kubwa kubwa kuhusu haya mambo,kwasababu alishanisoma ndani ya moyo wangu kuwa sina interest kabisa na hayo mambo.
Anasema kama ningeonyesha interest kidogo,basi angenifungukia siri zooote na kunirithisha rasmi nyenzo zake za kufanya izo kazi.
Anasema lengo lake kuu alitaka mimi nizitafute izo mali ili niweze kuukomboa ukoo wangu na umaskini,maana yeye alipewa iyo nafasi akaichezea...( yeye naye alifundishwa na baba ake,yaaan baba wa babu yangu)
Babu yangu alifariki 2014 akiwa na miaka 98...kuna sehemu moja uko kijijini kwetu katika mashamba yake,aliacha usia kwamba pasichimbwe ,wala kupandwa kitu chochote kile juu ya ile ardhi mpaka pale atakapotokea mteule katika ukoo wetu na atapewa ishara maalumu
Iyo sehemu katika shamba,kwa juu kuna mchanga mweupee ambao ni mkavu kipindi chote hata mvua inyeshe namna gani hapaloi
Ukoo wote unaamini pengine ilo eneo ndo sehemu alipohifadhia nyenzo zake za kufanya izo kazi za kutafuta mali za kale.