Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Katika uingereza ya kale, siku moja mtabiri mmoja alitabiri kuwa, ndani ya mwaka mmoja ujao kutatokea upepo mkubwa sana... Upepo huo utaangamiza mji wote ule... .. Upepo huo utavuma usiku mida ya saa 2 .... Upepo huo utavuma kutokea bondeni... Mtabiri huyo akashauri kuwa watu wachukue tahadhari, upepo ukianza watu wakimbilie mlimani kwani ndio itakuwa salama yao.

Basi kweli muda huo ulipita, siku hiyo jioni mida ya saa mbili. Bwana mmoja alimuona mama akikimbia akitimua mbio kuelekea mlimani. Haikupita muda mwanaume alikuwa nyuma yake.. Bwana yule akakumbuka kuwa mtabiri alitabiri. Na wakati ndio huo, naye akatoka mbio na familia yake, majirani nao wakafuata, majirani wa majirani wakakimbia wakipiga kelele cha kimbunga huku wakielekea mlimani.

Wakiwa kule mlimani, wakaanza ulizana juu ya ukubwa wa kimbunga hicho.. Kila mmoja akasema alimuona jirani anakimbia naye akafuata. Hatimaye yule bwana wa kwanza kukimbia akasema mimi nilimuona mama anakimbia nikajua ndio utabiri wa mtabiri umefika...

Yule mama kuulizwa akasema yeye alikimbia baada ya mumewe kutaka kumpiga usiku ule, na mume naye akawa anamkimbiza mkewe ili amkamate wala hawajaona kimbunga.

Swali, mlishawahi ziona hizo mali? Au ni hadithi kama za kimbunga au samaki mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ankali wangu kateseka sana na hizi mambo na hadi leo huenda bado yuko huko "mgodini", kama ni mauza uza basi itakuwa kuna namna kichwa kinavurugwa unakuwa unaamini umezikaribia mali..... Pia hapo ulivyotaja Lumbira (kama ndo ile ya Mbeya) nimesoma shule moja maeneo yale nakumbuka kuna bweni hata walimu walichangia kulivunja eti kuna mali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuu..mzeebaba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kakojoe ukalale,jambo usilolijua wala usihangaike nalo....waache wanaojua vitu hivi.

Kwa akili yako unadhani kila kitu ni cha kuchimba,kuna vingine waliachiwa watu, hata hizo heller,zingine wanazo wakongwe ,,,.!!

Hizi akili za darasani wakati mwingine huwafanya watu more mbumbumbu....!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Maswali hujajibu unasisitiza umbumbu wangu. Anyway the motion is closed na sorry kwa kuwaharibia biashara.
 
Kuna mahali huko Tanga Korogwe kijiji cha Lutindi Wajerumani wamejenga kanisa na hospitali ya vichaa.
Ukipanda huko juu kuna kilele cha mlima hao wajerumani wameweka zinga moja ya msalaba wa zege sa sijui na hapo kuna mali au vipi.
Mleta uzi kama upo tayari kunilipa ntakupeleka tukachimbe mana hali ngumu.
 
Ukiuchimba huo msalaba wa zege, kilichomo ndani ni kajitabu kadogo ka rangi ya njano na kijani.. Kana maneno yasomekayo "ILANI YA CCM"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka nimefika kijungu na daraja la mungu. Nimepaona kwa macho yangu. Majo ya mto yanaingia kwenye hicho kijungu. Na kuna kijisehem cha kupita na unaambiwa shart unapopita utangulize mguu wa kushoto.

sent using [emoji85]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…