Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,203
- 37,906
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha sasa akiwaua nyie je??Mtaalamu alisema kuna vito vya kutosha sana, tulipofiikia kuna vigaae vikubwa vimefunika na pembeni yake kuna ukuta wa mawe umejengwa,sasa kuna ngema juu imeninginia na kuna kiwe, inafaa lilipuliwe na litolewe.
Tulikutana na mauza uza kibao lakini tyliyashinda,kubwa ilikuwa nyoka wa kutisha wa kutosha, tuliambiwa hapana kumuuwa hata mmoja,mbinde ilikuwa kuwatoa humo shimoni.
Sent using Jamii Forums mobile app
🙄🙄🙄
Ugumu wake upi mkuu kwamba ukichimba hupati au kunamambo ya gizaWadau haya mambo nimeshiriki sana kweli vitu vipo nimefika ktk eneo husika sema kutoa mzigo ni shughuli na mpaka niliamua kuacha kwasababu unapoteza muda mwingi na pesa kufuatilia but kuna eneo najua kuna mzigo ila kuchukua sasa ni kugumu nimekutana na huo.ugumu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni kweli pia na Mm nineshuhudia kuna mzee mmoja kama wa miaka 89 au 90 alikuwa na ramani ya hazina kubwa sana iliyopo around Mwadui Shinyanga.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mauzauza mengi mkuu
Kuna baadhi ya hazina ni ngumu kupatikana bila ya kuwepo kwa mwongozo maana kama Mwadui kuna sehemu ukionekana lazima wazee wakuulize kuwa umekwenda kufanya nini hukoRamani na uwepo wa hazina ni vitu viwili tofauti kabisa. Anyway nimetahadharisha kwakuwa nafahamu ninachokiandika. Nasubiri ushuhuda kwa aliyepata hizo hazina.Haya mambo ni ya kufikirika zaidi fanyeni utafiti wa kina mtanielewa ninachokimaanisha hapa.
Umesahau Pangani mkuu, tena huku wamezika ardhini kabisa, hawa jamaa walikuwa na mbinu kali sana
Kuna mmoja kyela eneo lake inasemekana chini kuna pango huko masanduku na gari moja lipo wazungu wakaomba wampe gari na wamjengee nyumba nzuri ilo eneo wapewe wao jamaa akakataa akasema atachimba yeye..
kitu cha kushangaza kila lipokua anachimba vile vitu vinashuka chini... Akatengeneza mashimo makubwa matatu na maji kwake bila mafanikio
Hivyo vitu vya kishirikina hatari
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi story ya kubandua jini uliimaliza we jamaa ni tapeli unatafuta makoloKama unajua utapeli kwanini unaongelea kuhusu biashara inafanyika eBay? Kwahiyo eBay ni utapeli?
Mbona unajichanganya sana Sister?
Kubali kwa hili ndugu wewe ni mbumbumbu, mambo haya yapo,na wenye bahati zao wanatusua,mie nimeona kwa macho yangu, na mwisho ilikuwa ni singida, bibi kizee aliuza pasi kwa Muizraeli, alikuja na helicopter akachukua pasi yake na akaondoka na ajuza huyo na mjukuu wake,japo walipewa pesa kiduchu sana, mil 30 na ushee hivi.
Wapo wanaochemka kutokana na mauzauza hayo,wengine wanakutana na maiti na wengine wachache pia wanabahatika. Utajiri baba unanjia nyingi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya nguvu za gizabhalafu unaweza kuhatarisha maisha unaweza kufa
Ukitaka kufirisika na kupata uchizi ingia kwenye hiyo biashara. Kila mali kale utakayopata utaambiwa siyo. Ukipata hiyo Heller watakuambia mwaka siyo tunataka ya 1890, ukiipata utaambiwa hapana hii imechubuka, mara ilihusisha kifo nk. Utaambiwa kuna pasi, ukiipata watakuambia aah! siyo hii ya mkaa, ipo ya mvuke... Mara utashangaa unapata stress utaota mvi hadi kwenye nyusi.Ndugu zangu wanajamvi.
Nimekuwa katika utafiti wa mali kale na mambo ya asili kwa muda mrefu.
Katika utafiti wangu nimekuja kugundua wajerumani wameficha mali nyingi sana kawenye ardhi ya Tanzania.
View attachment 1022278
Wakati wa utawala wa wajerumani kulikuwa na fedha ambazo zilikuwa zikitumiaka.
Heller na Rupee zilikuwa zikitumiaka. Coin hizo zilikuwa na madini mengi sana tofauti na coin za sasa.
Kwa mfano 1 Heller kwa sasa inauzwa kwa $900 - $1000.
View attachment 1022271
View attachment 1022276
Kwenye vita vya kwanza vya dunia wajerumani walizichimbia hizo mali sehemu mbalimbali kwenye ardhi ya Tanzania kwa ustadi mkubwa.
Katika tafiti nilizozifanya mpaka hivi leo. Maeneo yafuatayo na mengine mengi ndiko zilipogichwa mali hizo. Inatakiwa kujua sasa ni eneo gani masanduku yenye mali yalichimbiwa:-
Hizi ni sehemu kadhaa zinazohitajika utafiti wa kina ili kujua ni sehemu zipi mali hizo zilifichwa.
- Ikombe
- Mibirizi
- Kasanga
- Ilembule
- Rombo
- Nyakanazi
- Uvinza
- Mlalo
- Kisarawe
- Kazimzumbwi
- Kirondatal
- Tukuyu
- Leganga
- Igulwa
- Ushetu
- Mnazi
- Mikese
- Shume
- Lumbira
- Mbulu
- Nansio
- Sekenke
- Galula
- Liuli
- Manda
- Lushoto
Asanteni
Hekaya tu hizi za bunuwasi.Kuna jamaa alikuwa anawinda mbugani na baba yake wakapita sehemu wakakuta mawe mengi ya dhahabu yamerundikwa kwenye mti wa mwembe, hawakuyatilia maanani wakaendelea na uwindaji walipo rudi kijijini wakawasimulia watu. Watu walivyo sikia hivyo wakambembeleza kijana awapeleke. Kabla kijana hajawapeleka wakaenda kwa kwa mganga kupiga ramli.
Mganga akawambia waende ila anaona giza mbele ya huyo kijana anayewapeleka. Wakasisitiza japo kijana aliogopa. Basi mganga akawambia wakifika kuna kitu kitatokea ila wasiseme neno lolote.
Story ni ndefu ila nitaifupisha.
Walipokaribia kwenye ule mti kweli waliziona zile dhahabu ghafla kikatokea kimbunga kikali kikamyanyua mzee moja. Mkwe wa yule mzee kuona hivyo akasema "haiwezekani baba mkwe aende"
Ghafla walitokea nyani kusiko julikana wakawapa kichapo si cha nchi hii alafu ikanyesha mvua kubwa hawajawahi kuona. Ikaharibu chakula chote walicho kuwa nacho.
Ilikuwa ni safari ya siku nne kurudi bila msosi
Sent using Jamii Forums mobile app