T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Mimi sio mwanajeshi na kipindi fulani niliwahi kutaka kwenda ila nikaghairi kuomba nafasi.Mkuu huwa nasoma baadhi ya posts zako uko vizuri sana kwenye mambo ya majeshi, kama hutojali ningependa kujua wewe ni mwanajeshi na kama siyo je unapenda kuwa mwanajeshi, au ni unapenda tu kufuatilia hivyo vitu
Wabongo wengi hukosea kudhani jeshi linajulikana na wanajeshi tu. Huko duniani jeshi linajulikana na watu tofauti na ndio maana kuna vitu kama SIPRI na Jane's ambavyo vina retired military men wachache sana kama washauri ila kazi zinafanywa na raia.
Washauri wa kijeshi wengi huwa sio wanajeshi. Mourinho hajui mpira ila anajua kuufundisha, Lampard mpira kacheza ila kuufundisha hajui. Jeshi lina kawaida ya kudhani linaweza kila kitu hata kama maofisa wamesoma risk management, political science, economics na vitu kibao ila bado ule upepo wa kijeshi wa kudhani wanaweza kila kitu upo. Mtazamaji wa nje anayelijua jeshi vizuri ndio anaweza balance, ukijazana akili za maofisa ndio yale ya Argentina kuanzisha vita na Uingereza. Kile ni kipigo cha wazi kilitafutwa.