Wajinga ndio wanadhani utawala wa Putin utaanguka

Mkuu huwa nasoma baadhi ya posts zako uko vizuri sana kwenye mambo ya majeshi, kama hutojali ningependa kujua wewe ni mwanajeshi na kama siyo je unapenda kuwa mwanajeshi, au ni unapenda tu kufuatilia hivyo vitu
Mimi sio mwanajeshi na kipindi fulani niliwahi kutaka kwenda ila nikaghairi kuomba nafasi.
Wabongo wengi hukosea kudhani jeshi linajulikana na wanajeshi tu. Huko duniani jeshi linajulikana na watu tofauti na ndio maana kuna vitu kama SIPRI na Jane's ambavyo vina retired military men wachache sana kama washauri ila kazi zinafanywa na raia.

Washauri wa kijeshi wengi huwa sio wanajeshi. Mourinho hajui mpira ila anajua kuufundisha, Lampard mpira kacheza ila kuufundisha hajui. Jeshi lina kawaida ya kudhani linaweza kila kitu hata kama maofisa wamesoma risk management, political science, economics na vitu kibao ila bado ule upepo wa kijeshi wa kudhani wanaweza kila kitu upo. Mtazamaji wa nje anayelijua jeshi vizuri ndio anaweza balance, ukijazana akili za maofisa ndio yale ya Argentina kuanzisha vita na Uingereza. Kile ni kipigo cha wazi kilitafutwa.
 
Kumbuka russia mwanzoni mwa hii vita walipanga msururu wa vifaru kuelekea kyiv urefu wa macho kutoona mwisho. Vifaru vyenyewe vile dhaifu tu. Jeshi lote la ukraine likahamia kuhami mji mkuu huku warusi wakiteka kirahisi sehemu kubwa ya majimbo manne waliyoyatangaza kama sehemu ya nchi yao.
Kwa hivyo hii mambo ya wagner huenda ni mbinu nyingine kumhadaa mchekeshaji zelensky na mabwana zake wa nato.
 
States ilitumia miaka 20 kupigana na taleban.

At the end of the day taleban wameshika hatamu.

Hii ni successful au failure?
 
States ilitumia miaka 20 kupigana na taleban.

At the end of the day taleban wameshika hatamu.

Hii ni successful au failure?
Mujahideen walipewa silaha na USA kupigana na uvamizi wa Soviet Union, Soviets wakatimua mbio mwaka 1989. Ikaja Taliban ikatawala Afghanistan na kuhifadhi magaidi, Marekani ikaja kupambana nao kukamata magaidi. Ikawaondoa madarakani tangu 2001 ikakaa zaidi ya miaka 20. Ikapambana na ugaidi ikamaliza mission ikawaacha Afghanistan wajuane na mambo yao. Taliban ikarudi madarakani baada ya makubaliano na Marekani.

Unataka success gani tena? Au success ya kumshinda babantilie na kampuni yake.
 
Ni mchezo unachezwa hapo si rahisi Putini kuangushwa kirahisi namna hiyo
 
Nimeshawaambia sana watu huu uasi ungekuwa ndani ya jeshi la URUSI hapo ndio pangekuwa mtiti kwa Putin

Lakini wanajeshi wakukodiwa ndio waiangushe serikali ya Putin ni ndoto ya mchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…