Wajir: Askari Wanyamapori waua raia wawili kwa risasi, wananchi walipuka

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mtu mmoja Ijumaa alidaiwa kupigwa risasi na kuuawa na maafisa wa polisi baada ya maandamano kuzuka katika mji wa Wajir.

Maandamano hayo yalizuka baada ya maafisa wa Shirika la Huduma ya Wanyamapori (KWS) kudaiwa kuwaua watu wawili wanaoaminika kuwa wawindaji haramu Alhamisi jioni.

Mauaji hayo yalizua maandamano ya hasira kutoka kwa Wakaazi wa Wajir waliomiminika barabarani, kuziba barabara na kuwasha moto kuonesha hasira zao.

Kulingana na maafisa wa KWS, washukiwa hao walimuua twiga na walikuwa wakisafirisha nyama yake, na kwamba juhudi za kuwazuia hazikufua dafu, hali iliyowafanya kufyatua risasi.

Wakazi wa Wajir waliwakosoa maafisa wa KWS kwa kuwaua wawili hao badala ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.

"Ninawataja maafisa ambao wamefanya vitendo hivyo kama wahalifu wanaotumia risasi za serikali kuua raia wasio na hatia," akalalamika mmoja wa wakazi.

Naibu Gavana wa Wajir Ahmed Mohamed aliwataka polisi wajizuie wanapowashughulikia waandamanaji.

"Vyombo vya usalama lazima vibadilishe mtazamo. Wasitujibu kwa risasi kila wakati kunapotokea suala,” alisema DG.

Viongozi wa eneo hilo pia walikashifu mauaji hayo na kutaka kuweko utulivu huku uchunguzi ukianza.

"Ni bahati mbaya kwamba tumepoteza maisha. Maisha yoyote yanayopotea ni mengi sana lakini kuendelea na yale yale hakuwezi kuleta suluhu.

Tutashirikiana na vyombo vya usalama ili kuhakikisha kwamba haki inatolewa kwa familia zilizopoteza wapendwa wao,” Mbunge wa Wajir Kaskazini, Ibrahim Saney alisema.

Maandamano hayo ya siku nzima yalitatiza shughuli za kawaida za biashara katika eneo hilo huku polisi wakishirikiana na wakaazi kuendesha vita na kuwaacha kadhaa wakijeruhiwa.
 
Wakenya kiswahili chenu ni kama mnatumia google translater

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom