Wajua msikiti wa Al aqsa Jerusalem ulijengwa likiwa ni kanisa la Byzantine (Byzantine church)?

Embu tukae hapa kwenye Yesu kuwa muislamu.... Mmesema Yesu alikuwa Myahudi.... Wakati huo uyahudi ni dini na unaesma sio lazima kuwa myahudi na kupractice uyahudi.... Moja, una uthibitisho gani kwamba Yesu hakuuishi Uyahudi japokuwa yeye mwenyewe kuwa myahudi?

Lakini pia kuna utata kwa yeyote anayejaribu kufikiri swala hili.... Yaani Mungu awatumie Manabii na mitume wayahudi( wenye chimbuko la Israel yaani Yakobo)kila walipokosea ila kwa mara moja tu mwaka 600 AD ndo aende kumtumia mtume kutoka macca tena amtoe nabii kutoka katika jsmii ya watu(waqureish) ambao hata walikuwa hawamjui huyo Mungu na taratibu zake, yaani aache kuendelea kutoa mitume kutoka kwa watu ambao aliwapa sharia yake aende akamwinue mtume kutoka kwa wapagani ambao walikuwa hawamjui Mungu kabisa? Hii inafikirisha kukubali uhalali wa mtume Muhammed S. A,.

Lakini pia kwanini mna quote habari zilizopo kwenye Bible alafu mistari ya mbele yake mnaipuuza hamuoni kuwa mnakosa ujumbe wote kwa kutafuta kile mnchotaka kusikia tu?
Mfano; mnakubali kuwa yesu alisujudu, alivaa kanzu kama ushahidi wenu wa kuwa alikuwa muislamu, lakini swala la kubatizwa hilo mnakataa ikiwa vyote vinatoka kwenye kitabu kimoja hamuoni kama mnakosa mantiki katika hoja zenu?
 
Sasa kama Biblia imemtaja au tuseme Injil Yenu imemtaja Mtume Mohammad SAW kama mtume ajaye kwanini na Yesu asiwe muislam. Nilitegemea labda utaniambia ushahidi wangu nilio utoa ni wa uwongo lakini huna ushahidi wa kupinga nilicho sema. Nikosoe kwa ushahidi basi ndio maana tunasema Biblia Yenu ya sasa imekuwa corrupted sio original kama mapokezi ya zamani. Kila miaka inavo zidi kuongezeka kuna mafundisho kadhaa yanatolewa na mengine yanaongezwa. Miaka 50 ijayo Bible yenu itaruhusu mapenzi ya jinsia moja sababu wakristo wengi hawaisomi biblia na pia mafundisho ya ukweli hawayapati.


Yesu alikuwa Myahudi lakini hakuishi dini ya kiyahudi
Dini ya kiyahudi unajua ni dini ya aina gani? Ni kitabu cha Torati au tuseme kitabu cha MUSA AS. Kitabu hiki kina mafundisho sawa sawa na uislam isipo kuwa mitume tu. kitabu cha taurati kimepokelewa na Mtume Musa AS na kitabu cha Quran kimepokelewa na Mtume Mohammad SAW
  1. Dini zote zina amini Mungu ni mmoja hana Mshirika. Masuala ya trinity au miungu 3 hatuna.
  2. Kuoa zaidi ya mke mmoja inaruhusiwa kote na mwisho ni wake 4.
  3. Mapenzi ya jinsia moja yamekatazwa.
  4. Riba imekatazwa au hakuna kabisa.
  5. Ukitaka kuchinja unaelekea Qibla(waislam) na kwa wayahudi unaelekea Yerusalem. Pia lazima utaje jina la Mungu kabla ya kuchinja.
  6. Mtoto akizaliwa wa kiume lazima atahiriwe ndani ya siku 7 21 na kendelea. Wayahudi wao ni siku ya 8.
  7. Kula kwa kutumia mkono wa kulia.
  8. kufanya Hijja kwa mwenye uwezo Makka(waislam) na Wayahudi ni Yerusalem.
  9. Kufunga siku ya ASHURAA. Nimebold ili uwende kuitafuta hii uje na majibu maana unapiga maswali nakujibu unaleta maswali tena. Hii siku kwa waislam tuna funga tofauti ili tusiendane na mila za KIYAHUDI ndio maana tunatakiwa tufunge siku tatu 9,10,11 au 9,10 au 10,11. Siku ya ASHURAA ni siku ya kumi ya Mwezi. Wayahudi wao wanafunga siku ya 10 tu. Hii ni tamaduni walio achiwa na mababu zao toka enzi na enzi za mitume wao. Bado wa iendeleza.
  10. Hauzikwi na jeneza. Ni wewe na sanda yako. Wayahudi nao huzika hivo. Vita vya Palestina si una vifuatilia. Basi utajifunza kitu.
  11. Kiarabu na Kihebrew vina landana kwa zaidi ya 40%. Myahudi akiongea na mwarabu wanasikilizana. kama lugha tu zina shabihiana lakini ukisikia uislam unaona ni tofauti. This is not fair.
  12. Hairuhusiwi kumpa mkono au kumshika mwanamke ambaye unaweza kumuoa.
  13. Eneo la kufanyia ibada lazima uvue viatu japo sehemu chach wana ingia navyo.
  14. Neno KAFIR linatumika dini zote mbili kama mpinga dini. Mtu tofauti na Dini yao ni kafir. Sasa wao ndio wanau hatar
  15. Tukija kwenye kufanya ibada sasa. Wote tunafunga mikono wakati wa swala. mkono wa kushoto chini juu wa kulia. Japo waislam wengine hawafungi ila wengi wanafunga. Kutoa salam baada ya ibada kugeuka kulia then kushoto. Wayahudi wao hurudi nyuma hatua tatu then shingo wanageuza kulia then kushoto na anakuwa kamaliza.
Umeona haya mafundisho niliyo yaeleza hapo juu. Sasa niambie wayahudi wa sasa wanafanya hayo mafundisho. Ni wachache sasa. Kinacho badilika ni mapokezi ya mafundisho tu. Yesu au Issa bin Mariam ndiye aliye kabidhiwa Injil na hii ndio kitabu kilicho chakachuliwa. Kuna wanafunzi au tuseme wapokezi wa hii Injil wameandika vitu ambavyo Yesu mwenyewe hakuyasema au kuruhusu.

Ukiwaangalia wayahudi na waarabu haswa wa huko Palestina sio rahisi kuwatofautisha sababu wanafanana. kwani kutoka Macca kwenda Yerusalem kuna Umbali gani. Mitume hawa wote ni wa Mwenyezi Mungu na wanatumwa kwa ajili ya kufikisha utukufu wa Mwenyezi Mungu. Pia wanatoka kwenye koo moja. kwahyo kusema Mohammad SAW mara ukoo wa QURIASHI. Haina shida ni damu hiyo hiyo ya MZEE IBRAHIM A.S.
 
Lakini pia kwanini mna quote habari zilizopo kwenye Bible alafu mistari ya mbele yake mnaipuuza hamuoni kuwa mnakosa ujumbe wote kwa kutafuta kile mnchotaka kusikia tu?
YESU HAKUBATIZWA
YESU HAKUBATIZWA
YESU HAKUBATIZWA
YOHANA 4:2-3
2 (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,)
3 aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.

NITAENDELEA BAADAE
 
Kuwa submissive to the will of God ni kuzitii amri zake kumi, mtume alizitii? mtume hakuua? hakuzini?.....
 
YESU HAKUBATIZWA
YESU HAKUBATIZWA
YESU HAKUBATIZWA
YOHANA 4:2-3
2 (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,)
3 aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.

NITAENDELEA BAADAE
Unamaanisha haujui utofauti kati ya kubatizwa na kubatiza?
 
Kuwa submissive to the will of God ni kuzitii amri zake kumi, mtume alizitii? mtume hakuua? hakuzini?.....
Sio tu kutii amri kumi maana ukisema amri kumi unaongelea mafundisho ya Musa AS. Yesu hakupewa amri kumi bali aliendeleza mafundisho ya Injil.
Sio tu mtume wetu Mohammad SAW. Mitume wote walitii.
Kuhusu kuuwa ina ruhusiwa vitani na kuhusu kuzini hakuna mtume mzinifu sababu mitume wana zaliwa mitume by nature.
 
Umeona sasa, wewe unasema Yesu hakubatizwa kifungu ulichokitoa kina sema Yesu hakubatiza...
Huoni utofauti hapo ni kama nikisema kupigwa na kupiga haya maneno yana maana mbili tofauti kaangalie kwenye kiswahili kauli ya kutenda na kutendwa...
Lakini pia Uyahudi uliozungumzwa hapo kwenye aya iliyofuata sio Uyahudi kama dini ila ni Uyahudi kama eneo ukiangalia kwenye
bible ya kingereza inapaita Judea wakati Uyahudi kama dini unaitwa Judaism, kiswahili nadhani ndo hayo maneno mawili yanaweza kutamkwa vilevile lakini ikamaanisha vingine kutokana na muktadha...

John 4:3
[3]He left Judaea, and departed again into Galilee.
aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.......umeona utofauti sasa?
 
Alhamdullilah
leo nimepata time nimalize kile nilicho bakisha.
Yesu ndio hakubatizwa wala hakumbatiza mtu. Hapo nilipo quote nimeonyesha hakumbatiza mtu kwahyo unataka ushahidi wa kubatizwa.
lakini kabda ya kufika huko naomba nikueleze jambo kuwa katika lugha ya Hebrew au Kiarabu. Sababu hizi lugha zina fanana kwa zaidi ya asilimia 40. Hakuna neno J kwenye herufi sana. kwahyo Yesu jina lake lilikuwa anaitwa Yoshua na JOHN mnaye muita John mbatizaji jina lake ni Yahya. Sasa hawa wawili ni ndugu kwa maana ni mabinamu. Yahya naye ali uliwa na mayahudi katika kisa chake alijificha kwenye mti a mayahudi waka ukata ule mti na Nabii yule akafa.
Unajua tukisema bible yenu imekuwa fabricated mnadhani tunawatania lakini ndio ukweli mtupu, angalia haya maandiko alafu unipe majibu

Ama kauli inayodaiwa na Wainjilisti hao kutolewa na Yohana akimweleza Yesu kwamba "Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu". Kisha Yesu naye eti akamjibu na kumwambia Yohana kuwa "kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavvyo kuitimiza haki yote", inamwonyesha Yesu hapa akipinga wazi maelezo ya Nabii Yohana (a.s.) jambo ambalo katu haliwezi kufanywa na Yesu (a.s.) kwani Yesu anajua wazi kuwa Nabii yoyote hasemi kitu ila ni Wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu. (Tazama 2Petro 1:21).

kwa hiyo ndugu yangu biblia inasema Yesu alibatizwa na Yohana. Lakini Yohana ali uliwa na mfalme Herode wakati huo Yesu alikuwa yupo Misri ili kuepushwa asi uliwe. Pia kitu kingine ukiacha tu kuwa ndugu wawili na pia ni manabii lakini pia wamezaliwa zama moja na wamepishana miezi sita kiumri. Naomba ufanye reseach zaidi kuhusu uzao wao na mpaka kufika kifo cha mmoja wao alafu upige hesabu kujua Yesu alibatizwa vipi na lini?

"aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.......umeona utofauti sasa?"
nadhani hapa hukuelewa haku maanisha hivi. Yudea ulikuwa ni mji ambao ulikuwa eneo la Palestina ukingoni mwa Jordan ambao kwa sasa waisraeli wanasema ni mji wao.
Japo kuwa Yudea lina maana nyingi kama ila ki asili linatokana na YAKOBO AS. Lakii ukitumia Uyahudi kufafanua neno Yudea unapoteza maana.

 

Attachments

  • christians.jpg
    38.7 KB · Views: 8
Sasa mbona unajipinga mwenyewe mwanzo umesema kwamba Yesu hakubatizwa na wala hakubatiza tena ukatoa na andiko linaloonesha kabisa kwamba Yohana hakutaka kumbatiza Yesu.... Andiko ambalo umelitafisri unavyotaka wewe.....
Lakini wewe mwenyewe Maelezo yako ya mbele umekiri kuwa Yesu alibatizwa ila shaka yako sijui ni umri.... Sasa kuna shida gani kwa watu wanaotofautia na miezi sita...... Alaf stori ya kufungwa si ilitokea baada ya ubatizo.... Nimekwambia shida yenu huwa mnatafuta sehemu chache bila kusoma aya nzima zile sehemu zinazowapinga mnaziacha kwa makusudi na kupotosha ujumbe kabisa.... Hili ni tatizo
Kuhusu swala la uyahudi nimekwambia usisome biblia ya kiswahili peke yake nimekupa kwenye biblia ya kiingereza ambayo ndio tafsiri ya kiswahili imetokea wametumia neno 'Judaea' hili lilikuwa ni eneo la kabila la Yuda mtoto wa Yakobo baada ya wana wa israeli kugawana maenwo ya kaanani kimipaka ya makabila, kwa kiswahili ndio ikatafsirika kama Uyahudi.. Hii haiusiani na uyahudi kama dini bali ni eneo, unaweza kusoma zaidi kwenye biblia... Unaweza angalia hapa pia kwa kujifunza zaidi..... Lafu pia unasema Yohana ni Yahya sema hivi kama ambavyo Yeshua kiarabu mnammwita Isa, na Yohana mnammwita Yahya ila jina Yahya halina uandishi au matamshi ya kiyahudi sema Mohamed baada ya kujifunza utamaduni wa kiyahudi akawabadilisha na majina ili waonekane kweli ni waislamu kumbe ni uongo wao walikuwa wayahudi na majina yao ni ya kiyahudi na kwenye hisoria za wayahudi wapo ila historia za kale za waarabu hawapo...
 
0
Na kudai hadi Adam na Eva walikuwa Waislam wenzao, sijui walisilimu wapi wakati aliyeleta Uislam Mtume Mudy hakuwepo

Wafuasi wa Bwn.Mudy wanachekesha sana

[emoji317][emoji317][emoji317]
Unajua mnashindwa kuelewa kuwa hiyo ndiyo iman! Kama unavyoamini wewe ukristo ni Dini wakati neno kristo limetokana na lugha ya kigiriki likiwa na maana ya Masihi au mkombozi au kiongozi hivo kristo ni cheo ila leo hii wote wanajua ukristo ni Dini cos mmeaminishwa kuwa dini japo Yesu hakuketa Dini ulimwenguni hapa.
 
Kaka dini kwa kifupi ni mtindo wa maisha kwa hio wale wanaoishi kama kristo anavyosema hao ndo wanitwa wa kristo sio mpaka iandikwe kwamba ukristo ni dini iaminini...
Mfano pia uisilamu umeanza miaka ya 600AD je kuna sehemu yeyote kabla ya mida huo inayosema kwamba uislamu ulikuwa ni dini kabla ya Mohamed.... Ila waislamu wote wanaamini ilikuwepo sio kwa sabababu ya kusemwa au kunadikwa bali kwa lifestyle
 
Kama unajua ni lofestle basi hakuna haja ya kuwacheka wenzenu wanasema Uislamu ulikuwepo kabla ata ya Muhammad maana imani yao imewaambia hivo na issue za iman huwezi hoji kwa bahati mbaya.
 
Kama unajua ni lofestle basi hakuna haja ya kuwacheka wenzenu wanasema Uislamu ulikuwepo kabla ata ya Muhammad maana imani yao imewaambia hivo na issue za iman huwezi hoji kwa bahati mbaya.
N kwa kusema hivyo unakubali kuwa ukristo ni dini sio?
 
Hata hilo unalosema ni hekalu lililojengwa na Sulemani ambalo lilivunjwa na Warumi, halikujengwa na Sulemani,bali lilijengwa na Wayahudi baada ya kurudi kutoka uhamishoni Babeli, hekalu la Sulemani lilivunjwa na mfalme Nebukadreza mwaka 586 BC
Nadhani Nebukadreza hskubomoa hekalu bali alichoma moto malango, Nehemia na Ezra walifanya kuripea palipoharibiwa baada ya kutoka uhamishoni...nitarudi kwa usahihi zaidi

(
1 Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni,
Nehemia 1:1

2 Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliopona, hao watu wa uhamisho waliosalia; na habari za Yerusalemu.
Nehemia 1:2

3 Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Nehemia 1:3

4 Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni;
Nehemia 1:4)
 
Mda mwengine inakubidi utumie hadi video kuwa elimisha ndugu zangu wakristo sababu naamini ukweli mna ujua ila kutokana na kukariri na kukosa mtu sahihi wa kukushauri una bakia kama mkiwa.
Wakristo mnadhani uislam umeanza miaka 600AD huko lakini mna sahau kuwa Yesu hakula nguruwe, alifunga bila kula kitu chochote kama sisi, alikuwa aki sujudu wakati wa kufanya ibada, Alikuwa aki muomba Mungu moja kwa moja hakumtaja Maria wala roho mtakatifu, alifuga ndevu pia alivaa kanzu. Lakini uki uliza kwa matendo haya mkristo gani anayafanya utakuja kwa wayahudi.
Uyahudi na uislam umetofautiana mitume tu. Maana hata Yesu ni Myahudi ki asili.
Tukija kwenye Yesu kubatizwa maandiko yenu yana pishana. Tuki waambia huyo Yohana mbatizaji kama mnavo muita alikuwa na yeye ni Mtume vile vile kwahyo yeye na Yesu walikuwa ndugu. Waislam tuna Muita Yahya. Ali uwawa na mayahudi.
Shida mlio nayo wakristo wengi mki kosa hoja mna tafuta contradiction nyengine.
Fanyeni toba kabla nafsi zenu hazija wekwa mihuri ya motoni. Ni ile hali ya kufanya jambo baya alafu nafsi yako haikusuti. Ogopa sana hiyo
 

Attachments

  • iamshahinmalek-20240124-0001.mp4
    14 MB
  • iamtonykyle-20240124-0001.mp4
    14.4 MB
  • alphareminder-20240124-0001.mp4
    3.8 MB
  • wsf02-20240124-0001.mp4
    7.3 MB
  • nosaybalogy-20240124-0001.mp4
    1.2 MB
Sasa wewe ndugu kuna kitu gani ulichokielezea hapa.....
1. Unasema Yesu alifunga, alivaa kanzu, na mengine mengi... Tena kwa kutumia reference ya kwenye biblia, mbona hamsemi Yesu alishika sabato alafu waislamu hamuishiki, mbona Bible inasema Yesu alikufa na kufufuka ila nyie hamuamini, alafu unapouzungumzia ukristo akili yako usijifunge kwa wakatoliki madhehebu ni mengi na wanaamini tofauti kuna ambao hawaamini katika kusali rosali na maria fuatilia..... Kwa kifupi tamaduni za maisha ya Yesu hayathibitishi kuwa Yesu alikuwa muislamu na umeshasema zinathibitisha kuwa alikuwa myahudi na ndugu uyahudi sio uislamu, tikea zamani wanaabudu Mungu wao na sio Allah, wanataratibu zao za kiibada tofauti na waslamu hivyo Yesu hakuwa muislamu.

2. Sasa unasema biblia inajichanganya kuhusu kubatizwa kwa Yesu mbona huoneshi inavyojichnganya sasa..... Unaishia kusema tu Yesu na YOHANA walikuwa ni ndugu sasa undugu wao unathibitishaje kuwa Yesu hakubatizwa?
3. Alafu hizo video sijajua zina maana gani sababu hazifafanui chochote kati ya tunachokizungumza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…