Dollar hermees
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 517
- 1,045
Uislam wa zama kabla ya Mitume wengine zilikuwa tofauti na uislam alio upokea mtume Mohammad SAW.Sasa wewe ndugu kuna kitu gani ulichokielezea hapa.....
1. Unasema Yesu alifunga, alivaa kanzu, na mengine mengi... Tena kwa kutumia reference ya kwenye biblia, mbona hamsemi Yesu alishika sabato alafu waislamu hamuishiki, mbona Bible inasema Yesu alikufa na kufufuka ila nyie hamuamini, alafu unapouzungumzia ukristo akili yako usijifunge kwa wakatoliki madhehebu ni mengi na wanaamini tofauti kuna ambao hawaamini katika kusali rosali na maria fuatilia..... Kwa kifupi tamaduni za maisha ya Yesu hayathibitishi kuwa Yesu alikuwa muislamu na umeshasema zinathibitisha kuwa alikuwa myahudi na ndugu uyahudi sio uislamu, tikea zamani wanaabudu Mungu wao na sio Allah, wanataratibu zao za kiibada tofauti na waslamu hivyo Yesu hakuwa muislamu.
2. Sasa unasema biblia inajichanganya kuhusu kubatizwa kwa Yesu mbona huoneshi inavyojichnganya sasa..... Unaishia kusema tu Yesu na YOHANA walikuwa ni ndugu sasa undugu wao unathibitishaje kuwa Yesu hakubatizwa?
3. Alafu hizo video sijajua zina maana gani sababu hazifafanui chochote kati ya tunachokizungumza...
Hapo kwenye kufa na kufufuka anaye sema hivo ni nani? Yesu mwenyewe au vijana wake?
Niambie katika lugha ya ki hebrew neno Mungu lina tamkwaje?
Kwenye post zilizo pita nimeonyesha uhusiano wa karibu baina ya uislam na uyahudi. Kapitie tena uje.
2. Nimeonyesha ilivo jichanganya kwa kusema undugu wa Yesu na Yohana. Wakati Yohana anauliwa Yesu hakuwepo katika mji huo. Kwa maana kama angekuwepo na yeye angeuliwa. Yesu alirudi kwenye huo mji baada ya yule mtawala alio muua Yohana na Yeye kuwa wote wamekufa? Swali ni je alibatizwa mda gani hapo? Sijui ume elewa swali langu vizuri? Kuna maandiko yenu ya uwongo yanasema Yesu alibatizwa au kubatiza? Kipindi anafanya hivo, huku kwengine inasema Yohana aliuliwa na Mayahudi. Swali ni je amebatizwa na nani?
3. Video nilizo zituma zina fafanua kwa ukubwa sana udhaifu wa maandiko neno sababu hata neno biblia halipo kwenye maandiko yenu. Pili kuna video moja inaelezea andiko moja linalo ongelea kuhusu kufunga na kusali. Na matoleo mengine yamefuta hiko kipengele sasa ukisema hujaelewa hivo video ni dharau au kitu gani?
Video nyengine inaelezea kwanini uislam ni dini sahihi sababu toka kuletwa na Mtume Mohammad kama mtume wa mwisho hakuna kilicho badilika. Sasa ukisema video zangu huja zielewa ni wewe hujataka kuelewa.
Kwa maelezo hayo nilio yatoa natarajia ulete majibu sahihi kuhusu maswali yangu na usikimbie kwa kutafuta maswali mengine. Yaani tuendelee pale tulipo ishia ndio vizuri.