Ikawa wanadamu walipoongezeka usoni pa nchi,wana wa kike wazuri na wa kuvutia walizaliwa kwao.Na malaika,wana wa mbinguni,waliwaona hao binti za wanadamu,wakawatamani.Basi wakaambizana wao kwa wao,"Twendeni,tukajitwalie wake katika binti za wanadamu,nao watuzalie wana".Na Semjaza,kiongozi wao,akawaambia:"Naogopa ya kwamba hamtakubali kutenda jambo hili,na mimi pekee nitaibeba adhabu ya dhambi hii kubwa".Wote wakamjibu na kumuambia 'Na tujifunge kwa kiapo,ya kwamba tutatekeleza jambo hili'.Wote wakajifunga kwa kiapo.Na jumla yao walikuwa mia mbili,walioshuka katika kilele cha mlima Hermon,katika siku za Jared.Pakaitwa mahali pale Hermon,kwa sababu ya kiapo kile.Na haya ndio majina ya wakuu wao:Semjaza,Araklba,Rameel,Kokablel,Tamlel,Ramlel,Danel,Ezeqeel,Baraqijal,Asael,Armaros,Batarel,Ananel,Zaqlel,Samsapeel,Satarel,Turel,Jomjael na Sariel.Hawa ndio wakuu wa vikosi.Na wengineo wote waliokuwa pamoja nao walijitwalia wake,kila mmoja akaoa mke mmoja,wakawaendea na kujinajisi pamoja nao,wakawafundisha elimu ya hirizi na uchawi,na mizizi,na kuwafahamisha elimu ya miti.Wakawatunga mimba,nao wakawazalia wana,ambao walikua na kufikia urefu wa eli elfu tatu(futi 450),wakawalisha chakula chao chote hadi pale waliposhindwa kuwahudumia zaidi,majitu yakawageuka binadamu na kuanza kuwatafuna.Majitu yakanajisi ndege wa angani,wanyama,viumbe vitambaavyo,samaki na hata wenyewe kwa wenyewe walitafunana,na kunywa damu.Dunia ikalaaniwa,ikaomboleza kwa ajili ya viumbe hawa wasio na sheria wala ustaarabu.Na Azazel(malaika) akawafundisha watu kufua chuma,kutengeneza upanga,na visu,na ngao,na dirii,akawafahamisha madini yaliyoko chini ya ardhi na jinsi ya kuyageuza kwa matumizi,na vikuku,na mapambo,na matumizi ya wanja,na jinsi ya kupamba kope za macho,na mawe yote ya thamani,na rangi zote za maji.Kukatokea uovu mkubwa sana,wakafanya uasherati,wanadamu wakapotoshwa,na kuharibika njia zao zote.Semjaza akawafundisha uchawi na mizizi,Armaros akafundisha uganga(kutatua uchawi),Baraqijal unajimu,Kokablel akafundisha elimu ya buruji(constellations),Ezeqeel elimu ya mawingu,Araqiel ishara za dunia,Shamsiel ishara za jua,na Sariel elimu kuhusu Mwezi.Binadamu wakaangamia,na walivyozidi kuangamia walilia,na kilio chao kilifika hadi mbinguni.Na Michael,Uriel,Raphael na Gabriel wakatazama chini, na kuona damu nyingi ikimwagika duniani,na uovu wote,wakaambizana wao kwa wao,"Dunia iliumbwa huku wakazi wake wakiwa hawajui huzuni wala vilio,mbona tunawasikia wakilia hadi kwenye milango ya mbinguni?Enyi watakatifu wa mbinguni,roho za wanadamu zinatulilia zikisema,pelekeni kilio chetu mbele yake Aliye Juu."Wakamwambia Bwana wa enzi,"Ewe Bwana wa Mabwana,Mungu wa Miungu,Mfalme wa Wafalme,na Mungu wa enzi zote,kiti cha enzi cha ufalme wako kinasimama katika vizazi vyote,na Jina lako takatifu na tukufu limebarikiwa katika vizazi vyote!Umeumba vyote,una nguvu juu ya yote,na mambo yote yako wazi machoni pako,unayaona yote na hakuna linalojificha mbele zako.Umeyaona yote Azazel aliyofanya,kuwafundisha wanadamu uovu wote na kuwafunulia siri zilizofichwa mbinguni,ambazo binadamu alihangaika kujifunza kuzielewa:Na Semjaza uliyempa mamlaka juu ya malaika wenzake.Nao wamekwenda kwa binti za wanadamu duniani,wakalala nao,wakajinajisi,wakawafunulia kila aina ya dhambi.Na wanawake hao wamezaa majitu,na dunia yote imejazwa damu na dhuluma.Tazama,roho za wale waliouawa zinalia na kutoa mashtaka yake katika milango ya mbinguni,na maombolezo yao yamezidi,wala hayaishi kutokana na dhuluma inayotendwa duniani.Wewe unajua mambo yote kabla hayajatokea,unayaona haya yote na yanakuumiza,lakini hujatuambia la kufanya juu ya yote haya."......