Wajue waimba gospel wa kike ambao wamevunja ndoa zao baada ya kuwa maarufu

Question:- Anyways hata wewe una makandokando yake ni vile tu hatukujua punguza judgement

Answer:- Ni mpango wa Mungu sio?
Watakupa likes kama zote wale wa 'Only God can judge me'

#YNWA

Muasisi!unataka kunielezeaje hapo?
 
Duh watukufu wa Mungu wote Hawa ni vilala ngamvye😂😂
 
Aisee!
Nilikua nawapenda sana vile walivyokuwa pamoja kwenye nyimbo zao haswa zile za kuabudu, aisee kumbe ndoa sio mchezoe?
Waliutendea haki Ukristo, injili hata huduma wa uimbaji kipindi hicho sana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Me naona kama tunataka kuwaona waimbaji kama malaika,hamna kitu ni binadamu wenzetu tu wale,wanamadhaifu ya kibinadamu sema tunaona sana makosa yao Kwa vile ni mashuhuri!
Hii comment inafanana kila kitu na comments za "mchepuko" wangu mmoja juu ya watumishi wa Mungu wanaofanya "uovu" huku wakijifisha katika joho la "utumishi wa Mungu nao ni binadamu na si malaika'!!!
 
Ke ana kibali gani cha kuoa?

Wapi Ke katoa posa au mahari?

Kuoana [emoji777] .

Kuoa/Kuolewa [emoji736].
Hapo ulipoweka alama ya "X" ndipo penye shida.
Wanawake 89% au zaidi wanaamini "mnaoana" na sio kuoa/kuolewa.

Hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Nitakuka na uzi kuhusu hili jambo siku moja, Mungu akiniwezesha.
 
Kiukweli Huwa sijui nini alifanya
Il inasemekana mumewe mpole
Issue iko hivi (sad story)

Yule Pastor aliyekuwa amemuoa Christina Shusho ni mtu poa sana, real Pastor, mtu mwenye kujiheshimu na kupenda kumtumikia Mungu kwa haki siku zote.

Jamaa alimkuta Christina akiwa hoi bin taaban kijamii huko mikoani, asiyekuwa na mbele wala nyuma, mshamba kwa 100% lakini Pastor akagundua kipaji cha Uimbaji kilichojificha ndani ya Christina. Jamaa akaingia chimbo kukiboresha kipaji, muonekano wake na swaga mpaka binti akawa presentable kwenye jamii, akamtafutia walimu wazuri wa sauti, melody na muziki, akasaka mashairi kwa watu mbalimbali, akazama studio kufanya audio rekodi, akawapa wataalamu wakazipitia ili kuona mapungufu, na kurejea upya studio ili kuziweka vyema, zilipo tiki, akaingia madhabahuni kuziombea ili ujumbe wa zile nyimbo upenye kwa watu, kisha video shooting ikafanyika na kurudiwa mara kadhaa, wataalamu waliporidhika, nyimbo zikaanza kuachiwa moja baada ya nyingine na zika hit balaa, mfano wa Unikumbuke, Wakuabudiwa nk.

Vision aliyokuwa nayo Pastor kupitia sauti ya uimbaji wa Christina ilikuwa ni kuhakikisha gospel inapigwa world wide, alitaka kumuona Christina akiimba gospel hadi viunga vya Ikulu mbalimbali dunia mfano Tz, Kenya, Nigeria, South Africa, USA, UK nk akialikwa kama honorable gospel singer kwenye special events za new year festivals, inauguration ceremony nk. Jamaa hakuwa na mipango ya kutaka kutajirika kupitia gospel.

Sasa wakati cheche kidogo tu za mafanikio zilipoanza kuchipuka, Christina akaanza kubadilika, tamaa ya pesa ikamuingia, Christina akaamua kuuza talanta yake ya thamani kwa kuona aibu ya kuwa mwanapunda wa kumbeba Yesu (wito wa kumtumikia Mungu) lakini akaona fahari ya kuwa nguruwe kisa kavikwa pini ya dhahabu puani (umaarufu wa kisanii), na kilichofuata kimebakia kuwa ni historia. Leo hii Christina ni mtu wa kutafuta followers mitandaoni hadi kwa kick, kuimba ili kupata pesa, kudanga na wanaume mbalimbali. Ndoa ilishakufa kitambo sana baada ya kumkimbia mumewe na wito wa kumtumikia Mungu kupitia uimbaji ulishayeyuka zamani. Ni mwendo wa kuanzisha makanisa ya kitapeli mtaani (Christina ana kanisa lake Manzese), kuandaa matamasha ya kisanii sanii na kutrend mitandaoni kwa mambo ya kijinga kabisa.

Very poor Christina.
 
Shetani/Lucifer tunaambiwa ndiye aliyekuwa mkuu wa kusifu na kuabudu.

Anajua vizuri jinsi ya kupata wafuasi wengi kupitia "sauti za ala za muziki na maneno".

Ni rahisi sana kwake kukutega popote ilimradi unapenda muziki, iwe R&B, Rhumba, Gospel, Kaswida, Rock, Country, Amapiano, Hip Hop, Bongo Flava na nyinginezo.

Amefanikiwa kwa hilo, lakini naamini kwa kuwa Mungu Baba wa Mbinguni anatupenda binadamu wake kuzidi upeo, mwisho wa siku tutaokoka kutoka kwenye huo udanganyifu wa huyo shetani kwa Neema ya Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…