Tatizo la wasanii wengi wa bongo fleva sauti zao zinatengenezwa studio na mbaya zaidi hawakupitia hatua za awali na kubobea kuimba iwe kwenye kwaya makanisani au Qasida, kwenye Madrasa kama ilivyo DRC, USA etc hivyo hawawezi kuimba "live"kile kilichotengenezwa studio.
Mashindano yetu ya kama Bongo Star Search hayatuletei vipaji vipya chipukizi ukilinganisha na mataifa mengine kama kwenye Pop Idol,UK, au mashindano ya kuimba kwenye bendi kubwa za muziki kama kule DRC angalia kama PPU (Bendi B) ya JB Mpiana au usajli wa chipukizi wa Werrason.
Banana Zoro pamoja na kwamba alishaanza muziki akiwa mdogo yale mashindano ya Coca Cola Pop Idol ndiyo yalimtambulisha Tanzania kama mwimbaji bora, na kama tukisema waimbaji bora kabisa wazawa bado anaweza kushikilia namba za juu ingawa bado kuna walee wanaoimbia kwenye bendi kama Chalz Baba, Jose Mara, Kalala Junior, Dogo Rama, maana Bela ndiyo ni mkali wa kunata na beats lakini vile vile tusisahau ametokea wapi.
Wasanii wa Bongo Fleva inabidi waende kwenye shule za muziki kujifunza kuimba na ili waimbe "live" au wasione aibu kufanya mazoezi na kupiga live na bendi za muziki kama wanataka kufanikiwa kimataifa zaidi, haya mambo ya kuwekewa "playbacks " na kuanza kucheza inaweza isiwapatie maonesho mengi ya nguvu kwenye anga za kimataifa na ushindani huu unavyokuwa mkali huko mbele wale wenye uwezo wa kuimba "live" au kuimbisha "kijiji" kama anayosema Bela na kucheza pia ndiyo watakuwa na kisu kikali. Zama hubadilika itafika kipindi watu watachoka "playbacks" watataka vitu "live".