wajue YAKUZA Genge Hatari zaidi la kihalifu Japan lililosambaa Duniani Kote

wajue YAKUZA Genge Hatari zaidi la kihalifu Japan lililosambaa Duniani Kote

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,074
Reaction score
3,743
Leo nimeona tuwajadili kwa undani kundi kubwa kabisa la kihalifu la kijapani na barani Asia liitwalo YAKUZA
Naamini humu kuna watu wanawajua zaidi yakuza hivyo kile kidogo ambacho ninachokijua kuhusu hawa jamaa nitakiweka hapa na wewe chochote unachokijua kuhusu hawa jamaa kiweke hapa unifaidishe mie na wengine

Binafsi katika elimu hii ya Organised Crimes watu hupenda kuwaongelea MAFIA kama ndio mabingwa wa Organised Crime na kuwasaahau kwa undani sana Yakuza

Yakuza ni genge la kihalifu ambalo chanzo chake ni japan ikikadiriwa kuwa na watu zaidi ya laki moja na elfu tatu
I03,000 na wako duniani kote hawa members wao wamesambaa mabara yote duniani kuanzia Asia, Ulaya, Amerika na Africa yetu hii

Genge hili halikuanza leo ila limeanza tokea mnamo karne ya 17
Hawa majamaa kazi zao sana sana ni Kufanya biashara haramu zote unazozijua wewe pamoja na kufanya shuguli zingine za kihalifu
Hawa majamaa unaambiwa wakitaka roho yako wanakuja kuichukua hata ukiwa umejifungia kwenye chumba cha IGP Mwema

Kwani inasemekana Yakuza Assasins Team ni watu ambao ni proffesional trained NINJITSU members
Ninjitsu ni staili au aina ya martial arts ambayo uki quilify unaitwa NINJA ambaye nina uhakika kwa asilimia mia moja hakuna polisi yeyote wa Mwema anaweza kuwazuia NINJA Assasin Team

Ninja-crouch.jpg



Scene-from-Ninja-Assassin-001.jpg


Hawa yakuza wanapatikana sana Japan ambapo ndio Origin yao hasa kwenye kisiwa kimoja kinaitwa
KYUSHU

Adhabu zao

Yakuza mmoja akifanya kosa huwa anapata adhabu kama ifuatavyo
Akifanya kosa la kwanza adhabu yao ni kukatwa kidole


Utawajuaje Yakuza
Yakuza wengi hupenda kujichora Tatoo mwili mzima

Z
Yakuza-Tattoos.jpg


Kwani tatoo zao ni ishara ya wao kujuana
Hasa wakiwa wanacheza Oicho-Kabu (oicho-kabu ) ni mchezo wa card kama vile baccarat and blackjack huwa wanavua mashati yao ili kujuana kusudi kujikinga na maadui zao ambao huwa wanaweza kujipenyeza kwenye mchezo huo kwa lengo tu la kusaka information


Kama Mafia na Yakuza wana Crime families ambazo ni

Yamaguchi Gumi
Hii ndio familia kubwa zaidi kwa yakuza yenye members asilimia 50 ya yakuza wote


Sumiyoshi Kai
Hii ina members zaidi ya 20,000 wa yakuza


Inagawa Kai
Haka ndio kadogo yenye members zaidi ya 15,000

Na Headquater ya yakuza ni FUKUOKA headquater huwa zinabadilishwa kutokana na upepo unavyoenda ila tokea waichague mwaka 2008 hawajabadilisha tena na mpaka sasa fukuoka Japan ndio inatajwa kuwa ndio Headquater ya Yakuza

Ila hata hivyo wamesambaa sana miji mingine ya japan kama
Tokyo, kumamoto, hiroshima, kyoto, hyogo pamoja na Aichi
Mitaa yao inajulikana kwa wakazi wa Tokyo inajulikana kabisa kuwa mitaa ya Shinjuku ndio ngome kuu ya kujidai kwa yakuza I mean ndio viwanja vyao ila nani sasa aende kuwakamata
Hakuna mtu si polisi, si mamlaka ya usalama na vyombo vya usalama wa japan vinavyothubutu kupeleka pua zao kule

061030154545_shop--sinjuku_shopping_street.jpg


Kwa marekani YAKUZA wanapatikana sana Hawaii vile vile wanapatikana sana miji ya Denver, New York, Huston na Oregon


Hakuna anayemjua Bosi wa Yakuza sura yake haijawahi kuonekana na wala hakuna mtu ambaye alishakutana nae

Hata hivyo sura pekee wa bosi wa yakuza kuoneshwa ni bwana Shinobu Tsukasa yeye ndie bosi mkuu wa familia ya YAMAGUCHI.. ambayo ndio familia kubwa sana ya YAKUZA huyu jamaa yeye na mabosi wengine wa familia zingine zinaripoti kwa bosi mkubwa ambaye anabaki kutokujulikana na mtu yeyote


8033303_13025765814r99.jpg




76768250.jpg


 
Mkuu ina maana hata Marekani ina wagwaya hawa jamaa...?

Nilijua hawawezi kutia pua nchini Marekani kumbe wamejikita kule Hawaii.....!


Vipi kuhusu Ugaidi, hawa hawajwahi kusingiziwa ugaidi kama Al Qaida.....?
 
naomba kuulizahayo ni magorofa ama magari?? hayo yaliyosimama marefu yenye picha.
jamani ushamba mzigo wa kuni msinizodoe.

Yaani kwenye hiyo pic umeshindwa kutofautisha kati ya maghorofa na magari mweh! Kama umeshindwa hiko kidogo tu basi sina budi kusema kuwa hata watu hujawaona. Kweli haya majangaaa
 
mkuu ni majengo hahahaha
mbona kama yanatembea ama ni macho yangu??
ama kweli ndo mana ni watengenezaji wa magai manake hata majengo wanayadesign utfikiri magari khaaaa!!!
 
Yaani kwenye hiyo pic umeshindwa kutofautisha kati ya maghorofa na magari mweh! Kama umeshindwa hiko kidogo tu basi sina budi kusema kuwa hata watu hujawaona. Kweli haya majangaaa

hebu tizama vyema hayo majengo halafu uniambie kama hayajasadifu gari lililoshehen mzigo mkubwa tena wa magodoro ama makopo ya rangi
 
Mkuu ina maana hata Marekani ina wagwaya hawa jamaa...?

Nilijua hawawezi kutia pua nchini Marekani kumbe wamejikita kule Hawaii.....!


Vipi kuhusu Ugaidi, hawa hawajwahi kusingiziwa ugaidi kama Al Qaida.....?


mkuu hawa wako kila sehemu hawaogopi mtu na wanajua wanachokifanya na huwa wana mitaa yao huko

marekani hii hii pale New York kuna kitongoji kinaitwa China Town huko wamejaa makundi kama

14k Group
Wo Group
black Dragons
Ang sung Tong
Gee Hin Kongsi

hizi ni organised crimes za china ambazo zimesambaa sehemu mbali mbali duniani... na New York wamejaa mpaka kuform kamji au kitongoji chao ndani ya New York inachoitwa China Town

na kuhusu swala la ugaidi mie naona huwezi kuta hata siku moja hawa Yakuza wakawa listed kwenye suala ugaidi ila wanayoyafanya ni Uhalifu

kuna tofauti kati ya Ugaidi na Uhalifu

wataalamu wa kucheza na kamusi hebu tupeni tafsiri hapa
 
Yakuza Mob ni hatari kuna mtu alishakatwa ulimi aliwadhurumu pesa za sembe.

kuna dada mthailand mmoja bartender alitoa siri yao hawa jamaa sasa alikuwa ameweka kipini kwenye chuchu zake si unajua madada ma bartender wa kithai waliopinda basi walikivuta kile kipini kilichokuwa kwenye chuchu...
damu zilizotoka hapo sio za kitoto
 
Asa hiko kibabu kilichovaa mawani na kofia ya ng'ombe mimi si ninaweza kukapiga tanganyika jeki?
 
hebu tizama vyema hayo majengo halafu uniambie kama hayajasadifu gari lililoshehen mzigo mkubwa tena wa magodoro ama makopo ya rangi

Mkuu kwani chini kabisa huyaoni magari hapo na watu wanatembea pemben mwa barabara? Mhhh au unatumia device gani kuaccess JF? Basi hata kama ni cm bas sijui itakuwa ya aina gani haha.
 
Asa hiko kibabu kilichovaa mawani na kofia ya ng'ombe mimi si ninaweza kukapiga tanganyika jeki?


umeona watu waliomzunguka??

na chochote utakachokifanya jiandae kutembelewa na ma NINJA

hao ndio ma mastermind wenyewe

hata JK unaweza kumpiga Tanganyika jeki sasa swali ni kuwa utamfikia mpaka alipo na kumpiga hiyo Tanganyika jeki ?
 
Hao ni kama tu komandoo yosso wa enzi hizi,hawana chochote cha zaidi ila kuvuta unga,bange,pombe na kisha kukwapua vipochi na vihereni vya wakina dada,kuwaweka hawa kundi moja na Mafia ni tusi!Yakuza ilipata umaarufu miaka ya nyuma kabla watu hawajapambazuka,sasa hivi hawana tofauti na vibaka wa manzese au unga ltd.
 
Hao ni kama tu komandoo yosso wa enzi hizi,hawana chochote cha zaidi ila kuvuta unga,bange,pombe na kisha kukwapua vipochi na vihereni vya wakina dada,kuwaweka hawa kundi moja na Mafia ni tusi!Yakuza ilipata umaarufu miaka ya nyuma kabla watu hawajapambazuka,sasa hivi hawana tofauti na vibaka wa manzese au unga ltd.


mkuu unafikiri wale kina yakuza vibaka wa uswahilini ndio hawa?
walikwapua tu jina
nadhani huwajui YAKUZA vizuri na naomba tu usiwajue kwani mambo yao ya ndani yanatisha
 
umeona watu waliomzunguka??

na chochote utakachokifanya jiandae kutembelewa na ma NINJA

hao ndio ma mastermind wenyewe

hata jk unaweza kumpiga tanganyika jeki sasa swali ni kuwa utamfikia mpaka alipo na kumpiga hiyo tanganyika jeki ?

Mweh!
Basi shughuli.
 
Asa hiko kibabu kilichovaa mawani na kofia ya ng'ombe mimi si ninaweza kukapiga tanganyika jeki?

hivi si umesikia ili uwe huyo jacuzzi ni lazima ufuzu mafunzo ya Ninja.......?.....
na je.. C.T.U......hao wapo Tanzania.....?.....nataka mafunzo tu sitaki uhalifu wao............
 
Last edited by a moderator:
Na kwa hapa Tz, Maskani ya YAKUZA ni wapi?
Au ndo wale YAKUZA MOBB wa kiswazi?
Dah!
Kweli hilo kundi latisha.
Na ninani anaewalipa vibaraka wote hao?
Au ndo kazi ya kujitolea mkuu C.T.U?
 
Last edited by a moderator:
Vipi kuhusu Ugaidi, hawa hawajwahi kusingiziwa ugaidi kama Al Qaida.....?

Mkuu kama ilivyo kwa Illuminati, Freemason n.k Yakuza ni moja ya 'secret societies' ambapo missions zao ni tofauti kidogo na hawa magaidi kama Al Qaida.
 
Back
Top Bottom