wajue YAKUZA Genge Hatari zaidi la kihalifu Japan lililosambaa Duniani Kote

wajue YAKUZA Genge Hatari zaidi la kihalifu Japan lililosambaa Duniani Kote

C.T.U Mbona wanaonekana "soft touch" tu? Embu muone huyo bonge aliyevaa miwani.


Mkuu hawa watu achana naoni noma kuliko maelezo na siku zote ogopa mabonge

jamii ya kina sammo hung


sammo.jpg
 
Ningependa mkuu pia kama ungeweza ungeongelea chinese the triads na diablo ili atleast tuweze kujua kuhusu hzi cartels pamoja na zinginine mingi zilizopo NY CITY . Maana mi ni mgeni maeneo haya.
 
Ningependa mkuu pia kama ungeweza ungeongelea chinese the triads na diablo ili atleast tuweze kujua kuhusu hzi cartels pamoja na zinginine mingi zilizopo NY CITY . Maana mi ni mgeni maeneo haya.

usiogope wewe ni mtoto mdogo sana jiachie tu mwanawani..
 
Ningependa mkuu pia kama ungeweza ungeongelea chinese the triads na diablo ili atleast tuweze kujua kuhusu hzi cartels pamoja na zinginine mingi zilizopo NY CITY . Maana mi ni mgeni maeneo haya.

umenikumbusha mbali sana
wazee wa mountain masters

wazee wa Triple Wong
May Wong
Mark Wong
Tim Wong

nikipata muda nitaeleza hayo majamaa
 
usiogope wewe ni mtoto mdogo sana jiachie tu mwanawani..

Mkuu mimi ni mzee kuliko unavyofikiri , ila kwenye haya mambozz nakubali ni mtoi . Vp wewe una taarifa zozote kuhusu hawa jamaa ?
 
Yes wako vizuri jamaa. Ever heard of Five Families Of New York? Hapo lazima u'll come across my name; lucchese.
 
kuna movie inaitwa show down in a little tokyo. ni balaa sans hii movie kwa sababu imereflect sehemu ya hali halisi ya kundi hili hatari.members wake ni kweli wamejaa tatoo mwili mzima.ninakubali kila kitu kilichoelezwa na mleta thread.ukiitazama hii movie kuna mengi ya ufahamu kuhusu YAKUZA halisi.
 
Mmenikumbusha Care raisu kwenye kahoteli kamoja Shinjuku...unachagua tokana na idadi ya pili pili kwenye picha...kahoteli (niseme mgahawa) kadogo lakini watu wanaotoka na kuingia wengi utasema mzinga wa nyuki. Hawa jamaa niliwasikia kwa mbali lakini kwa mimi mgeni sikuona madhara yao...tena wenyeji huwa hawapendi kutamka hilo jina. Nchi ikiendelea nayo inakuwa majanga...nimewakumbuka Shibuya Girls... (wanaogopa kivuli)
Sinjuku Acha Kabisa
usiniambie ulilkuwa hubanduki
uogashinihonishi kupata shushi kidogo..
 
Ni muda toka nitoke JP lakini nimekumbuka kama walikuwa wanasema biashara ya pachinko ina uhusiano na hao watu pamoja na muharifu wa Korea...ni biashara haramu (kamali) lakini serikali imeshindwa kuisimamisha kwa kuwa ina maslahi ya watu wasioshikika...Wajapan wengi wamefilisika kwa sababu ya pachinko na vijana kwa wazee wako addicted na zmezagaa kila kona kama njugu
 
Leo nimeona tuwajadili kwa undani kundi kubwa kabisa la kihalifu la kijapani na barani Asia liitwalo YAKUZA
Naamini humu kuna watu wanawajua zaidi yakuza hivyo kile kidogo ambacho ninachokijua kuhusu hawa jamaa nitakiweka hapa na wewe chochote unachokijua kuhusu hawa jamaa kiweke hapa unifaidishe mie na wengine

Binafsi katika elimu hii ya Organised Crimes watu hupenda kuwaongelea MAFIA kama ndio mabingwa wa Organised Crime na kuwasaahau kwa undani sana Yakuza

Yakuza ni genge la kihalifu ambalo chanzo chake ni japan ikikadiriwa kuwa na watu zaidi ya laki moja na elfu tatu
I03,000 na wako duniani kote hawa members wao wamesambaa mabara yote duniani kuanzia Asia, Ulaya, Amerika na Africa yetu hii

Genge hili halikuanza leo ila limeanza tokea mnamo karne ya 17
Hawa majamaa kazi zao sana sana ni Kufanya biashara haramu zote unazozijua wewe pamoja na kufanya shuguli zingine za kihalifu
Hawa majamaa unaambiwa wakitaka roho yako wanakuja kuichukua hata ukiwa umejifungia kwenye chumba cha IGP Mwema

Kwani inasemekana Yakuza Assasins Team ni watu ambao ni proffesional trained NINJITSU members
Ninjitsu ni staili au aina ya martial arts ambayo uki quilify unaitwa NINJA ambaye nina uhakika kwa asilimia mia moja hakuna polisi yeyote wa Mwema anaweza kuwazuia NINJA Assasin Team

Ninja-crouch.jpg



Scene-from-Ninja-Assassin-001.jpg


Hawa yakuza wanapatikana sana Japan ambapo ndio Origin yao hasa kwenye kisiwa kimoja kinaitwa
KYUSHU

Adhabu zao

Yakuza mmoja akifanya kosa huwa anapata adhabu kama ifuatavyo
Akifanya kosa la kwanza adhabu yao ni kukatwa kidole


Utawajuaje Yakuza
Yakuza wengi hupenda kujichora Tatoo mwili mzima

Z
Yakuza-Tattoos.jpg


Kwani tatoo zao ni ishara ya wao kujuana
Hasa wakiwa wanacheza Oicho-Kabu (oicho-kabu ) ni mchezo wa card kama vile baccarat and blackjack huwa wanavua mashati yao ili kujuana kusudi kujikinga na maadui zao ambao huwa wanaweza kujipenyeza kwenye mchezo huo kwa lengo tu la kusaka information


Kama Mafia na Yakuza wana Crime families ambazo ni

Yamaguchi Gumi
Hii ndio familia kubwa zaidi kwa yakuza yenye members asilimia 50 ya yakuza wote


Sumiyoshi Kai
Hii ina members zaidi ya 20,000 wa yakuza


Inagawa Kai
Haka ndio kadogo yenye members zaidi ya 15,000

Na Headquater ya yakuza ni FUKUOKA headquater huwa zinabadilishwa kutokana na upepo unavyoenda ila tokea waichague mwaka 2008 hawajabadilisha tena na mpaka sasa fukuoka Japan ndio inatajwa kuwa ndio Headquater ya Yakuza

Ila hata hivyo wamesambaa sana miji mingine ya japan kama
Tokyo, kumamoto, hiroshima, kyoto, hyogo pamoja na Aichi
Mitaa yao inajulikana kwa wakazi wa Tokyo inajulikana kabisa kuwa mitaa ya Shinjuku ndio ngome kuu ya kujidai kwa yakuza I mean ndio viwanja vyao ila nani sasa aende kuwakamata
Hakuna mtu si polisi, si mamlaka ya usalama na vyombo vya usalama wa japan vinavyothubutu kupeleka pua zao kule

061030154545_shop--sinjuku_shopping_street.jpg


Kwa marekani YAKUZA wanapatikana sana Hawaii vile vile wanapatikana sana miji ya Denver, New York, Huston na Oregon


Hakuna anayemjua Bosi wa Yakuza sura yake haijawahi kuonekana na wala hakuna mtu ambaye alishakutana nae

Hata hivyo sura pekee wa bosi wa yakuza kuoneshwa ni bwana Shinobu Tsukasa yeye ndie bosi mkuu wa familia ya YAMAGUCHI.. ambayo ndio familia kubwa sana ya YAKUZA huyu jamaa yeye na mabosi wengine wa familia zingine zinaripoti kwa bosi mkubwa ambaye anabaki kutokujulikana na mtu yeyote


8033303_13025765814r99.jpg




76768250.jpg



Ni genge lipi hatari kati ya MAFIA na YAKUZA?
 
mkuu hawa wako kila sehemu hawaogopi mtu na wanajua wanachokifanya na huwa wana mitaa yao huko

marekani hii hii pale New York kuna kitongoji kinaitwa China Town huko wamejaa makundi kama

14k Group
Wo Group
black Dragons
Ang sung Tong
Gee Hin Kongsi

hizi ni organised crimes za china ambazo zimesambaa sehemu mbali mbali duniani... na New York wamejaa mpaka kuform kamji au kitongoji chao ndani ya New York inachoitwa China Town

na kuhusu swala la ugaidi mie naona huwezi kuta hata siku moja hawa Yakuza wakawa listed kwenye suala ugaidi ila wanayoyafanya ni Uhalifu

kuna tofauti kati ya Ugaidi na Uhalifu

wataalamu wa kucheza na kamusi hebu tupeni tafsiri hapa

Uhalifu ni uvunjifu wa sheria wa kupangwa sio lazima kuua ila ugaidi ni mauji yaliyopangwa kiitikadi
 
Back
Top Bottom