Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu

Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu

Bora simba ibaki mikononi mwa mo itakua salama zaidi kuliko hao jamaa.
 
Hapa kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya pazia

1: Mo aliwaamini akina Try Again ili wasimame upande wake, inawezekana wakawa wanampa majibu ya uongo.

2:Viongozi walio upande wa mashabiki walikuwa wapigaji hasa kwenye usajiri, baada ya Mo kutafuta njia nyingine kwenye usajiri wakaona sasa mapigo ya 10% hayapo tena hivyo kilichobaki kuanzisha songombingo.

3:Mo anatoa fedha zake ili siku ikipigwa hesabu basi club ishindwe kulipa ili ajinyakulie umiliki wa club yote iwe mali yake
 
Wahindi, wapemba, wachaga Wana tabia ukiwapangisha wanakukopesha pesa kidogodogo mwisho wa siku wakikudai huna uwezo wa kulipa wanataka uwauzie kwa Bei watakayotaka. Mo alikuwa anacheza mchezo huohuo.
Katika vilabu vya soka vinavyoongozwa na watoto wa mjini na wajanja, wahuni, matapeli ni Simba.
Kuanzia kina Rage, Hasanoo, Marco Masanja ni mfano wao.
Mo alijiona mjanja kuwapa Simba pesa kidogodogo ili baadae awalazimishe kumuuzia timu kwa Bei anavyotaka lakini alisahau kuwa ule ni mchakato wa kisheria na Kuna taratibu za kulipa ili kupata hisa asilimia 49 ambao sio tu haujakamilika Bali pia hajalipia.
Pesa zilitakiwa ilipwe asilimia 20 na malipo kukamilika baada ya mwezi mmoja toka mchakato unakamilika.
Yeye alijiona mjanja kutengeneza madeni kwa kusema Ayoub nilimsajili bilioni 3 ili aonekane ametoa pesa nyingi. Pia alihakikisha Simba haiongezi wanachama ili aweze kuwacontrol waliopo alikataa Simba isisaini mkataba wa bilioni 40 na Azam kwa miaka 10 kwa sababu brand ya Simba ni kubwa na Simba wakiishiwa pesa yeye atatoa.
Hata kauli ya kusema anamiliki Simba aliitoa kupima upepo hapo ndiyo mtu kauziwa cheni bandia na kupewa pesa feki.
 
Anaandika Mhe. Hamisi Kigwangwala

✍️ “Kama ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi wana @SimbaSCTanzania tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!”

“Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye account yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! Kama angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

“Deni la pili: ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam - bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

“Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

“Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

“Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

“Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? Kama mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu - kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

“Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

“Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

“Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu.”
 
img_1717923615634.jpg
 
Huu msimu tuwe busy na kutafuta noti tu, hii Simba itatutoa roho
 
Wajumbe wa bodi ndio wenye timu na asset za Simba.

Mnawachukulia powa sasa ndio mtajuwa bodi maana yake ni nini na huwezi kuwaondowa.

Kama kuna mtu anadhani bodi ni kitu cha mchezo subilini sasa muone na wao ndio wenye nguvu 51%
Hatuna shida wawalipe wachezaji mishahara na watoe pesa za usajili.
 
Hapa kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya pazia

1: Mo aliwaamini akina Try Again ili wasimame upande wake, inawezekana wakawa wanampa majibu ya uongo.

2:Viongozi walio upande wa mashabiki walikuwa wapigaji hasa kwenye usajiri, baada ya Mo kutafuta njia nyingine kwenye usajiri wakaona sasa mapigo ya 10% hayapo tena hivyo kilichobaki kuanzisha songombingo.

3:Mo anatoa fedha zake ili siku ikipigwa hesabu basi club ishindwe kulipa ili ajinyakulie umiliki wa club yote iwe mali yake
Kutoa hela ni kutoa tu hakuna ujanja kwenye kutoa hela hao wajumbe wangekuja na hoja Mo hatoi hela ila anaibambikizia klabu deni ningeungana nao ila kitendo cha kukiri kuwa kweli anatoa ila wao wanataka asihesabu hizo hela kama mtaji wao walizipokeaje
 
Hiyo bodi ni ya hovyo Sana, haiwezekani ipokee pesa za MO bila kujua anazitoa Kwa malengo gani , huyo ni mfanyabiashara na anachohitaji yeye siku zote ni faida. Pamoja na Kuwa sifurahishwi na namna ya uwekezaji wa MO hapo Simba SC lakini kama kuna wajinga wachache waliotafutana pesa zake wakifikiri MO alitoa kama Sadaka basi wanapaswa kuzitaapika alafu wanaSimba SC tunahitaji Bodi yenye uadilifu na watu wenye taaluma na weledi siyo hao waswahili waliojazana hapo msimbazi sasa hivi.

See you next season!
Hapa kuna mgogoro mkubwa sana utaibuka endapo Mo atadai pesa zake
 
Kwanini mlikuwa mnapokea hizo hela, nyie bodi ya wanachama si ndiyo mlimleta manzoki awaombee kura?
Mo alikua anatoa msaada, kupokea msaada sio kosa cha kushangaza sasa hivi anazidai pesa zake la sivyo zifidiwe katika ile bilioni 20 ya kununua hisa zake. Ndipo hapo jamaa anahoji anazidai kwa msingi upi wakati tangu mwanzo hakukubaliana kama wanakopeshana
 
Kuna namna washauri wa muhindi wa Bombay wanampotosha hawezi zingua parefu hivo
Mhindi ni msomi bila hata washauri alikua anajua anachokifanya tatizo aliwachukulia poa wanachama akufikiri kwamba wanaweza kucheza na loopholes wakampiga knock out. Kwa namna alivyozitoa izo pesa ni alikua anatoa msaada hana uhalali wa kuzidai au kutaka zibadilishwe kuwa ile bilioni 20 ya hisa zake
 
Mo alikua anatoa msaada, kupokea msaada sio kosa cha kushangaza sasa hivi anazidai pesa zake la sivyo zifidiwe katika ile bilioni 20 ya kununua hisa zake. Ndipo hapo jamaa anahoji anazidai kwa msingi upi wakati tangu mwanzo hakukubaliana kama wanakopeshana
Walikubaliana kuwa hizo hela ni za msaada?
 
Mhindi ni msomi bila hata washauri alikua anajua anachokifanya tatizo aliwachukulia poa wanachama akufikiri kwamba wanaweza kucheza na loopholes wakampiga knock out. Kwa namna alivyozitoa izo pesa ni alikua anatoa msaada hana uhalali wa kuzidai au kutaka zibadilishwe kuwa ile bilioni 20 ya hisa zake
Round hii wamemshtukia mapema sijajua lile zengwe litaishaje....na aliekua anaongea ni CPA means anauelewa mpana wa masuala ya kifedha
 
Ukitoa pesa bila makubaliano ya kurudishiwa automatically huo ni msaada.
Kwamba Mo alikuwa anaandika cheque ya milioni 500 bila makubaliano? hata mtoto wa la nne hawezi elewa.
Kabla ya Mo hawa wajumbe wa bodi ya wanachama ndo jibu, miaka mitatu wanapokea hela hawasemi baada ya timu kuvurunda na kutakiwa kujiuzulu ndo wanajifanya wanaipenda simba.
 
Kuna yule Swedi alijiuzulu .Nilimshangaa sana kipindi kile.Wanaume hawajiuzulu kwa shinikizo la Mwamedi bwana.
 
Back
Top Bottom