Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania Urais.
View attachment 3206168
Imetoka hiyo,wale wa Samia hagombei tena wako wapi? 😂😂😂
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 mgombea wa CCM 2025 ni Samia SH.

Haters wake wote chalii

Wapiga ramli chaliii

Waliopanga Kumhujumu chaliii

Waliojisemesha kwamba hawezi chaliii

Wachawi chaliii

Yaani kiufupi Mama ni 🔥🔥🔥

Hongera sana Wajumbe Kwa Kasi nzuri.
Japo mimi si shabiki wa CCM, ni kichaa peke yake ambaye angeweza kudhani kuwa Samia hagombei atakatwa sijui hata walikuwa wanawaza nini.
Na ni kichaa peke yake anayeweza kuwaza kuwa uchaguzi CCM kwa sasa inaweza kushindwa kwa kura za uchaguzi. Huenda ni wishful thinking.
Haijalishi hupendi kitu kiasi gani, ila inabidi uishi katika uhalisia wa mambo.
Na wewe mwanzisha thread inabidi kwa upande wa wishful thinking yako ya uchaguzi wa CHADEMA uishi katika uhalisia kuwa mbowe anadondoka asubuhi na mapema.
 
Back
Top Bottom