Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania Urais.

Haters wa Samia chalii

Wangapi na waganga na wapiga ramli waliosema hagombei chalii

Waliojiapiza kushindana nae Ili kuzuia chalii

Waliosema ni Mzanzibar haiwezekani chaliii

Waliosema Mwanamke hawezi kuwa mgombea Urais Tanznaia chaliii

Waliosema anamalizia awamu ya 5 chaliii

Waliosema hawezi kutekeleza miradi na ilani chaliiii

Waliomuombea kifo na kupanga chaliii

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😏😏😏😏😏😏

Sasa hivi wamesalia na ramli Moja ya kuombea kifo
 
Uko sahihi, maana sasa hivi mshindi hapatikani kwa njia ya kura tena, bali maagizo toka juu.
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza chagua kibaraka.Wafuasi wa kibaraka mliomjaza upepo mnatafuta chorus za kujifariji 😂😂
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania Urais.

Pascal Mayalla
 
Kikwete ameipangua hoja hiyo kwa akili sana.

"Mwali hatolewi nje mpk siku 30 ziishe"

Kasema wasifanye uamuzi unaokinzana na sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Watu wanasema, Hii ni pre cooked.kila kitu kinachoendelea kilishapangwa.hata kamati kuu inayokaa saaa inaweza kuwa ilishaoangwa na majibu ya maswali yote aliyouliza kikwete juu ya sheria zote za uchaguzi zimeshakuwa reviewed,by the way watunga sheria ndiyo hao hao
 
Kama sheria na kanuni zinaweza kubadilishwa ndani ya masaa machache, kuna haja gani ya kuwa na sheria nyingine kandamizi ambazo zimeshapitwa na wakati huku zikiwa haziishi matakwa ya wananchi kwa kisingizio cha kuwa ni sheria halali?

[Mfano kuna haja gani ya kuwa na sheria ya ndoa ambayo inaruhusu vitoto vya kike vya miaka 14 kuolewa? Wakati umri huu ni mtoto anayetakiwa kuwa shuleni?]

Aka katoto kana utamu gani hadi tukatungie sheria ya kuolewa wakati wapo dada zake wa miaka 30 na kuendelea wanatafuta ndoa kwa udi na uvumba?

Wabunge wanagoma kuiodoa hii sheria; lakini watoto wao wa rika hilo hilo hawataki hata waguswe na wanaume kwamba bado ni wadogo? Wanahitaji kuwa shule!! Kwanini wawe hawa wa walalahoi?

Mzee Kikwete tusaidie na hili kwa hekima zako,busara zako,na sauti yako hapa nchini na ndani ya Chama tawala washauri Wabunge wa Bunge lijalo watunge kanuni na kuondoa hii sheria katika nchi yetu. Ni sheria Kandamizi kwa mabinti zetu.

Maana unakuta kuna mambo mengine hayafanyiki kisa sheria hairuhusu wakati yana maslahi mapana kwa jamii yetu.Kwanini nazo zisifutwe kwa kutengua kanuni ndani ya siku moja?

"Tanzania imara ni kuwa na sheria zinazotoa Haki na Usawa."

2025.
 
Back
Top Bottom