Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Ruvuma wakubaliana Rais Magufuli aendelee kuongoza miaka 20 mbele

Wewe tulia tu, mwache tu ajichanganye baada ya miaka yake kumi, hapo ndo utaona nguvu ya JWT ikiwa kazini. Achezee wakuu wa mikoa, NEC USALAMA na washamba wengine, lakini asithubutu zaidi ya miaka 10.ndo maana, hata wastaafu wametulia tu, jeshi letu naliamini sana. Asijidanganye wakizunguka hivyo anajiona anao viganjani. Wale watu bwana hawana urafiki wala uadui wa kudumu...
 
Halmashauri Kuu ya Mkoa??! Ni ya wauza korosho? Wachimba gesi au wachimba makaa ya mawe?
 
Naamini hii inawauma sana CCM kuliko hasa upinzani!! Watanzania tuondoe uvyama tuungane kujinasua na makucha ya huyu mnyama na nyoka hatari kabisa aliyeingia chumbani!!

Hatuna jinsi tumwambie hapana! Huo sio utaratibu!
 
Kitu kama hicho hakiwezekani pamoja na mambo mengine hakitakiwi kamwe, mambo ya kusema mtu fulani anaweza au amefanya mengi mazuri kuliko wwngine ni kujidanganya, hata ofisi na kiti unachokalia walikalia wengine na walijenga wengine pia. Kama wengine walivyo kaa na kuziacha ofisi basi kila mtu kwa wakati wake haijalishi ameikalia ofisi yake kwa muda gani ataicha itakaliwa na mwingine . Nitamaa tu za kimwili lakini kiuhalisia mtu haishi milele tamani uwezavyo lakini kuna siku utaicha ofisi au kazi unayo ifanya ili ifanywe na wenigine .
 
Hata yule mkulima aliefungua kesi akihoji ukomo wa Rais ni baraka kutoka kwake
 
Jamani kwani katiba inasemaje ? Ila naona katiba itabadilishwa 202......Ok kifo pekee ndo kitamtenganisha Magufuli na Urais. Wapinzani wenyewe waoga kweli. Ukuta tu waliingia mitini.
Samahani hivi ukuta ni nini?
 
Huwezi mlinganisha Hitler na Magufuli.Hitler aliikuta Ujerumani uchumi wake umeharibika sana.Ila Kipindi cha Hitler uchumi ulikua sana tena sana.Nakuambia wasingeingia vitani basi ujerumani ingekuwa number moja kichumi duniani.Kosa la Hitler ni ubaguzi kwa jews na kujiona yeye ni Mwamba na akavamia nchi zingine ambazo alitaka ziwe provinces za Ujerumani.
 
Black people cannot think beyond a hundred years (Willie Wrinch).kati
Kati ya hao wajumbe hivi kuna hata mmoja aliyesingiziwa kesi ya uhujumu uchumi au arms robbery???

Weusi siku zote ni mabinafsi sijapata kuona, mateso ya wenyehaki furaha kwa waovu!
 
Asingetoka aliyepita tungempataje huyu tunayemwona the best Ever?. Kila nyakati na nabii wake.
Wakati ukifika tutaletewa mwingine mzuri, madhubuti kuliko yeye.
Kiasi JPM akiwa anamnadi huyo mpya aseme kama JK- nimeleta chuma, kinatema checheeeeee!.
Msiwe na mawazo hayo. Tuendelee tu kula mtori nyama tutazikuta chini.
 
Samahani hivi ukuta ni nini?
Kusema ukweli sikumbuki hata kirefu chake,unajua tena kitu kikiishia hewani.Ila ilikuwa ni movement ya kupinga mabavu ya rais jinsi alivyokuwa akiendesha nchi.Walizoea operation Sangala,sijui movement of the people.Safari hii wakaogopa.Ndo kabisa sasa wapo kimya hawana mabavu tena ya kutoa dukuduku zao.
 
Jamani kwani katiba inasemaje ? Ila naona katiba itabadilishwa 202......Ok kifo pekee ndo kitamtenganisha Magufuli na Urais. Wapinzani wenyewe waoga kweli. Ukuta tu waliingia mitini.
Upinzani ni nani? Sema Watanzania wote waoga hadi mi ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…