Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Ruvuma wakubaliana Rais Magufuli aendelee kuongoza miaka 20 mbele

Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Ruvuma wakubaliana Rais Magufuli aendelee kuongoza miaka 20 mbele

JPM atapiga 25
Kwa nchi hii ilivyo, yawezekana mpaka ikafikia yeye mwenyewe atakaposema basi. Upepo unavyoelekeana jinsi anavyojiwekea mizizi lazima tukubali yale anayoyataka. Hakuna hata mtu anayeweza kumuonya wala kumsema kila mtu yupo kimyaa anasikiliza vibe linavyorindima
 
Leo kulikuwa na kikao cha halmashauri kuu mkoa cha kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ambao mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme alikuwa anawasilisha, Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja na Chanel Ten, wajumbe wa haashauri kuu mkoa wa Ruvuma wamekubaliana Rais Magufuri aendelee KUINGIZA kwa miaka 20 zaidi.

Kama mawazo hayo yataungwa mkono na mikoa mingine ina maana inawezekana Magufuri ndiye Rais atakaye kaa madarakani miaka mingi ikulu kuliko hata Nyerere

Viongozi wastaafu wanasemaje kuhusu hilo suala, kwa sababu tangu lianzishwe hakuna kiongozi yeyote mstaafu aliyewahi kukemea hiyo michezo. Kukaa kwao kimya unaleta shaka kama wanaunga mkono au la

Tujadili kwa pamoja haya ma
Huo ukomo sio wa CCM ni Kwa mujibu wa katiba ya nchi.Nyambafu zao
 
Kusema ukweli sikumbuki hata kirefu chake,unajua tena kitu kikiishia hewani.Ila ilikuwa ni movement ya kupinga mabavu ya rais jinsi alivyokuwa akiendesha nchi.Walizoea operation Sangala,sijui movement of the people.Safari hii wakaogopa.Ndo kabisa sasa wapo kimya hawana mabavu tena ya kutoa dukuduku zao.
Akhsante kwa ufafanuzi
 
Upinzani ni nani? Sema Watanzania wote waoga hadi mi ccm
Wala haujakosea,kweli mimi muoga si unaona hata hapa natumia fake name.Inabidi tuushinde uoaga.Tuwe kama kina MALCOM X,Nelson Mandela,Luther King ,Rosa Parks n.k
 
Leo kulikuwa na kikao cha halmashauri kuu mkoa cha kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ambao mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme alikuwa anawasilisha, Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja na Chanel Ten, wajumbe wa haashauri kuu mkoa wa Ruvuma wamekubaliana Rais Magufuri aendelee KUINGIZA kwa miaka 20 zaidi.

Kama mawazo hayo yataungwa mkono na mikoa mingine ina maana inawezekana Magufuri ndiye Rais atakaye kaa madarakani miaka mingi ikulu kuliko hata Nyerere

Viongozi wastaafu wanasemaje kuhusu hilo suala, kwa sababu tangu lianzishwe hakuna kiongozi yeyote mstaafu aliyewahi kukemea hiyo michezo. Kukaa kwao kimya unaleta shaka kama wanaunga mkono au la

Tujadili kwa pamoja haya ma
Ailinde katiba aliyoapa kuilinda. Hayo yote in uchochezi tu. CCM wanachochea hayo kwa kuwa wanajua kuwa anao uwezo was kuzuia upinzani. Hivyp wanatafuta mazingira ya kutamba bila kupingwa.
 
Inahitaji kuwa na afya ya akili na mwili...si kazi nyepesi kama kujamba..
 
Sitaki kubarikiwa na watu wanàfiki wanaoshabikia uvunjifu wa katiba Kwa masilahi binafs.
Baraka zikitolewa zimetoka kwa mtoa baraka na mpokeaji hana mamlaka ya kuzuia kubarikiwa.
Kwenye hili la Magufuli kuongezewa miaka 20, kuna popote katiba imevunjwa?.
Hata kwa hili ubarikiwe pia.
P
 
JK mwenyewe leo kasema hata nyerere alipopeleka mswada wa vyama vingi asilimia 80 ya watanzania waliukataa lakini kwa hekima zake aliulazimisha ukapita....hapa mimi napata wasiwasi ni kweli watanzania walikuwa hawataki vyama vingi au ndio mwanzo wa kutuaminisha kwamba vyama vingi havina maana..tunaweza kutawaliwa na chama kimoja...je itakuwaje iwapo ccm itashinda kwa kishindo kikuu kuanzia serikali za mitaa mpaka juu...ccm hii ya jiwe asiyekuwa na mpinzani maana wapinzani wake ndani ya chama wanapigwa stop hadi kwenda kuomba msamaha.....na hao wengine ambao ni kundi kubwa wanaotaka aendelee...MIMI NATABIRI ATAONGEZA MUDA....
 
Leo kulikuwa na kikao cha halmashauri kuu mkoa cha kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ambao mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme alikuwa anawasilisha, Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja na Chanel Ten, wajumbe wa haashauri kuu mkoa wa Ruvuma wamekubaliana Rais Magufuri aendelee KUINGIZA kwa miaka 20 zaidi.

Kama mawazo hayo yataungwa mkono na mikoa mingine ina maana inawezekana Magufuri ndiye Rais atakaye kaa madarakani miaka mingi ikulu kuliko hata Nyerere

Viongozi wastaafu wanasemaje kuhusu hilo suala, kwa sababu tangu lianzishwe hakuna kiongozi yeyote mstaafu aliyewahi kukemea hiyo michezo. Kukaa kwao kimya unaleta shaka kama wanaunga mkono au la

Tujadili kwa pamoja haya ma
Mie naunga mikono yote miwili aendelee kuwaingizia hata miaka hamsini kwani hayo ni makubaliano yao.ila katiba yetu iheshimiwe daima.
Asingekuwepo mkuu wa wilaya na mkurugenzi wala wasingetaja jina la raisi.Hawa wateule ndiyo shida.Hii ni alarm kwa wastaafu katiba ya walioba ndiyo wakati wake sasa hawa mliowaachia chama ni punguani hawaheshimu chama tena wanaheshimu matumbo yao tu
 
Jamani kwani katiba inasemaje ? Ila naona katiba itabadilishwa 202......Ok kifo pekee ndo kitamtenganisha Magufuli na Urais. Wapinzani wenyewe waoga kweli. Ukuta tu waliingia mitini.
Wapinzani na wewe ukiwa wapi,wapinzani tuwaache washafanya yao risasi walizopata zinatosha hii sasa zamu ya wananchi
 
Na kosa la magu ni hilo moja tu,kujiona kuwa yeye tu ndiye binadamu aliyekamilika,wengine wote waliopita,waliopo na wajao anawaona kama tu nyumbu!! Ndiyi maana anauliza kama hao wengine wataweza kujenga barabara na reli,anasahau kuwa yeye mwenyewe kaingia dar kwa treni iliyowekwa na wengine,anasahau kuwa kikwete kajenga barabara nyingi zaidi kuliko tawala zingine zote zilizotangulia na hakuwa na majivuno kama huyu!! Tanzanian demigod
Huwezi mlinganisha Hitler na Magufuli.Hitler aliikuta Ujerumani uchumi wake umeharibika sana.Ila Kipindi cha Hitler uchumi ulikua sana tena sana.Nakuambia wasingeingia vitani basi ujerumani ingekuwa number moja kichumi duniani.Kosa la Hitler ni ubaguzi kwa jews na kujiona yeye ni Mwamba na akavamia nchi zingine ambazo alitaka ziwe provinces za Ujerumani.
 
MAGUFULI ATAONDOKA MADARAKANI

1. CHADEMA Kama Chama kikuu Cha upinzania kimefika kwa wanachama Hadi ngazi ya chini na kuandikisha orodha ya wanachama wake. (kura hizo).

2. Mwaka 2015 walivamia kituo Cha ukusanyaji wa matokeo Cha CHADEMA na kuvunja computer zote pamoja na kuwaweka professionals wa IT Computer.. kwa hilo Chama kimejipanga zaidi ya mnavyofikiria.

3. Dunia inaangalia Tanzania kwa jicho la tatu na Kali kutokana na uvunjaji Mkubwa wa haki za binadamu. Na wamejipanga kusaidia kwenye kila hatua kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na haki. Na ikifikia hapo kwenye "Huru na Haki" maccm out.

4. Hali ya uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja Ni duni Sana na kila mwananchi anajua. Kwa hiyo itakuwa ngumu Sana kumdanganya mwananchi wa leo.

5. Kuna visasi kwenye familia nyingi Sana kwa matusi ya Magufuli kwa wananchi wake hasa wanapokuwa wanawasilisha ama kupata na majanga. Kumbuka
✓Kauli alizotoa kule bukoba baada ya janga la tetemeko
✓Kauli alizotoa Bunda wananchi walimwambia kwamba Wana njaa
✓Kauli alizotoa kwenye sakata la Korosho pamoja na kuwatia umaskini aliowaita walanguzi wa kangomba.
✓Kauli zake dhidi ya waliobomolewa majumba yao na kauli aliyoitoa kule Mwanza kuhusu bomoabomoa
✓kuna Kauli alizotoa dhidi ya matajiri kwamba wataishi Kama mashetwani.

6. Suala la Tumbua Tumbua ambayo ilisababisha baadhi ya familia kupoteza wapendwa wao kwa hoja ya hawana vyeti.

7. Suala la ajira kwa vijana, Hadi leo idadi ya ajira alizotoa na idadi ya wahitimu katika vyuo vikuu haviwiani. Na kwa asili ndo wapiga kura wengi kwelikweli. Ukiacha wale walamba viatu wao ambao Ni wachache Sana.

8. Kukataa kuongeza Mishahara kwa Watumishi kwa Miaka karibu minne, Jambo ambalo Ni la kisheria kwa mtumishi.

9. Suala la kupigwa risasi na kupotea kwa akina Azory Gwanda na Beny Sanane haya Ni masuala mazito Sana ingawa wanaccm Ni Kama mnajishaulisha vile. Jambo hili linamuokoaje Magufuli kwenye uchaguzi Mkuu mwakani?

Haya Ni machche Kati ya Mengi ambayo kamwe hawezi kuyarekebisha kwa mwaka mmoja anapokwenda kwenye kampeni. Na ambacho hamkijui Ni kwamba wananchi wamemchoka kweli ila wanaomzunguka wanamdanganya.

Hakika nawaambieni CHADEMA Wana kazi moja pekee ya kuhakikisha wanamleta mgombea makini anayekubalika na wananchi.. na kwa hakika Kama atasimama Lissu hebu tuwe wakweli Magufuli atatokea wapi?

#Sijui wanaojidanganya endeleeni lakini Hadi muda huu CHADEMA wanajua kura zao za mwakani kuazia kwenye kitongoji vyote zaidi ya elfu 64...+
 
Pelekeni laana zenu mbele huko
 
Back
Top Bottom