WAJUZI WA SHERIA: Mgao wa urithi kwa kesi kama hii mnaisolve kivipi?

Hii hotel baada ya Baba kufariki familia mzima walishindwa kuafiki kwa sababu ilionyesha ni kampuni ya mke na mume yani mama ana percentage yake na baba anapercentage yale .
Ila nafikili hata wakubwa waliacha kwa sababu ya mama kumueshimu tuu.
 
Mkuu DNA inamadhara sana usipokuwa makini ndo maana hata TZ ukitaka kupima DNA kuna mlolongo kinoma.
Sio rahisi ndugu watoke uko waseme huyu hakuwa mtoto wa kaka yetu. Unakithibitisho gani.

Hawakubali hivi hivi kupima DNA.
 
"Hakimu akaagiza kipimo cha DNA..watu wakamuwahi Mkemia fasta kitu kikasoma negativ...Hakimu akamng'oa kwenye mirathi..."

Aiseee..... Kumbe huwa iko hivi... So SAD
Hata mtoto hakiwa sio wa Baba kumbuka kuna Mama yek kwenye mali so atabeba za mama yake tuu.
 
Wapate ushauri kwa wakili lakini, mambo ya Kijinga sana kushindwa kupatana ndugu mpaka mahakaman.

Ni kama laaana, inaweza kuwa safari ya mda mrefu yenye visasi, chuki, wakati mwingine hata watu kuuana inawezekana.
Wasipokuwa makini.... Hii unaweza kuwa ni mwanzo wa chuki, visasi ambayo unaweza kwenda vizazi hata vizazi....
 
Ok Ngoja nikuabliane na wewe kwamba majibu yameenda sawa ila report ya kwenda mahakamani imeandikwa tofauti na mtu kachinjwa...
Mkuu nakuambia kitu nilichowahi kushuhudia...

Naamini Sana katika wataalamu wetu na wanafnya kazi vizuri ila unajua handling ya Majibu na hatua zake zote...
Ni mlolongo mrefu ingekuwa ni moja kwa moja sawa ila huo mlolongo ndo chanzo cha kuchange matokeo ksa namna moja ama nyingine na lazma wadeal na mkemia kwanza..Na usifikiri wanafanya bila kuwa na majibu ya kujihami mkuu No..
proffesionalism majibu ya kujihami huwa hayakosekani endapo Deal imeenda spoil
 
Lakini Huyo dogo inatakiwa ashauriwe Wakae chini wamshauri aache uppuuzi atapoteza kwa kujifanya kuchwa Ngumu..
Dunia inabadilika sana chuki,VisasI....
Na watu wanauwana kisa mali so aww care sana ...
Na apatane na ndugu zake
 
Nimesikitika sana kusoma comments za aina hii hapo juu....
Ni watu tu kutokufahamu ufanyaji kazi wa ofisi ya Mkemia Mkuu mwisho wa siku wanaandika porojo na propaganda.

Kitu kirahisi tu majibu ya DNA anapewa aliyeomba ifanyike DNA na hapo anaweza kuwa wakili, Mahakama, polisi au ofisi yoyote ya serikali.

Yule anayetolewa sampuli huwa sio muombaji yeye amekuja tu kutolewa sampuli na majibu yakitoka wala sio ya kwake sababu yeye sio muombaji

Yaani kwa urahisi ni kuwa, wapenzi wanataka kupima mtoto wao DNA, lakini wao hawawi waombaji wa kipimo kwa Mkemia badala yake wanatafuta Wakili ambaye ndio atakuwa muombaji wa kipimo na majibu yakitoka kwa Mkemia ni ya Wakili na sio ya wao wapenzi.

Sasa Wakili yeye atawasomea tu majibu alafu atabaki nayo maana sio ya hao wapeni bali ni ya kwake.

Na hapo wakili anafhmaau kabisa akijichanganya tu madhara yake hataweza kuyabeba kabisa, kivipi akubali kuchezeaha matokeo maana mtu anaweza akarudi kwa Mkemia ukafanyika uchunguzi wakili au muombaji yoyote mwenye hayo majibu ya kubumba akakutana na matatizo makubwa tu. Hapo jela mtu anaichungulia wazi wazi tena kijinga kwa maslahi ya wachache.
 
Sasa huo uhuni haujafanywa ofisi ya Mkemia, na huo uhuni ni kosa la jinai chini ya sheria zinazosimamia hilo zoezi.

Hao waliofanya huo uhuni wana uwezo mdogo sana wa kufikiri na kuchambua mambo Mkuu, maana aliyefanyiwa hicho kitendo akirudi kwa Mkemia kujiridhisha amini hao wajinga watakamatwa kama kuku wa broiler.
 
Asante Sana. Umefafanua vizuri Mkuu🙏🏾
 
Huyo baba alienda kwa huyo mama wa pili na mtaji alioupata kutoka kwa mama wa kwanza ndio ikaanzishwa hiyo investment kwahiyo mi naona wagawane kama watoto na sio kama wawekezaji,
Wangekuwa wawekezaji ndio wangesema wafuate percentage

Sent from my SM-T225N using JamiiForums mobile app
 
hapa sasa ndo umeongea point ya kweli ambapo huyo wakili anaweza aka act kama mediator kati yao na sio tu mediator hata wanapohitaji kufanya mgawanyo wataufanya kulingana na sheria na Taratibu....

Na kingine kuhusu Msimamizi wa mirathi anasaini Fomu ile namba sita (6) ya mirathi na form ya kugawanya mali chini ya usimamizi wa mahakama na sheria zinazosimamia mirathi ...
Labda huenda hawakuwa na msimamizi wa mirathi
 
Mm nahisi huyo mtoto mdogo ni wewe.
Na mimi ndo nilikohisi Ila Kiukweli kama ni yeye au ni rafiki yake namshauri rudi mezani ongea vizuri na ndugu zako muelewane unaweza ukang'ang'ania kuuzwa kwa hizo mali linalotokea la kutokea Mali huwa hazna mdhamana bhna zikapeperuka ...
Harafu ukaacha chuki mioyoni mwa ndugu zako na visasi unafikir atakayekushika mkono ni nani?
Au ndo tena utakuja kuanzisha uzi kuwa "ndugu zangu wananitenga baada ya kufa kwa Baba"

Cc: Mr shika
 
Mkuu nafahamu na Mpka ninazo Procedure zote hata kwenye simu hapa ninazo na naweza kutuma ukitaka nachoongelea sio kile kilicho kwenye proffesional au misingi ya kazi nachoongea ni Office corruption
 
Mkuu nafikili hata mama wa mtoto wa mwisho nae alienda na mtaji wake.
 
Hivi unafikili mama wa huyo mtoto angekuwa hai angewapo watoto wa mume wake mali alizoangaikia yeye kama yeye binafsi?????
Jibu.
 
Hivi unafikili mama wa huyo mtoto angekuwa hai angewapo watoto wa mume wake mali alizoangaikia yeye kama yeye binafsi?????
Jibu.
Hahaha Mkuu umedhihirisha kwamba kweli ni wewe 🤣🤣🤣.....
Tatizo lipo sehemu moja tu ambalo naliona kwako mkuu...
Hutaki kuamini kwamba Hizo mali ni za kwenu wote ila unaamini kuwa ni zako peke yako...
Jibu: Angekubali tu, umeshasahau mara hii yaliyomtokea Vicky kamata
 
Mkuu nafahamu na Mpka ninazo Procedure zote hata kwenye simu hapa ninazo na naweza kutuma ukitaka nachoongelea sio kile kilicho kwenye proffesional au misingi ya kazi nachoongea ni Office corruption
mwanzo kabisa ulichokisema kilikuwa ni kama vile watu wa Ofisi ya Mkemia wanaweza kuhongwa wakatoa matokeo ya vipimo vya DNA tofauti. Ndio nikasema hilo haliwezekani kabisa sababu matokeo ya DNA ni sayansi endapo yakapatikana pengine hilo jambo halibebeki.

Siwezi kukataa moja kwa moja kuwa wapokea majibu wanaweza wakafanya uhuni ila bado ni rahisi kuweza kubaini ukweli, sababu bado matokeo yatakuwepo kwa Mkemia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…