Wakati Arsenal na Man city zimecheza mechi 23 za ligi, Zote Zina penalties 2 tu, Simba mechi 16 penalties 8..Tafakarini

Wakati Arsenal na Man city zimecheza mechi 23 za ligi, Zote Zina penalties 2 tu, Simba mechi 16 penalties 8..Tafakarini

Kila team inayocheza na simba inahaidiwa pesa nono mwisho wa siku wanacheza kwa vurugu kutaka kupata hizo pesa,

Niliangalia match ya simba na SBS yani ni kama uwanja wa vita mda wowote wachezaji wanaumizwa.

Huu mtindo sijui umeanzia wapi.
 
Kuna kila dalili vilabu vyetu vikubwa vinahonga waamuzi..

Hebu fikiria vizuri, ni timu gani popote duniani ambayo ina takwimu za aina hiyo......yaani timu ina wastani wa kupewa penati kila baada ya mechi mbili.

Mkuu: hizi penati zina walakini?
Nijuavyo mimi; penati hutokea kama wapinzani wataruhusu ucheze eneo lao wanapokuwa wanashambulia.
Kama wataruhu makosa kwenye 18, kuna kusababisha penati au kufungwa.
Mi nadhani hii hoja ingekuwa na maana kama hizo penati zingekuwa na walakini.

Kupata penati sio dhambi
 
acha fananisha ligi za maana(technology,financial,ushawishi na ushabiki,kiwango ,aina za wachezaji,aina za marefa ) na hii ya kwetu kalagha baho (bado inakuwa,marefa bado wachanga kwenye fani,wachezaji ,asilimia nyingi bado tunakuwa tukiimanisha kila kitu
 
Mkuu: hizi penati zina walakini?
Nijuavyo mimi; penati hutokea kama wapinzani wataruhusu ucheze eneo lao wanapokuwa wanashambulia.
Kama wataruhu makosa kwenye 18, kuna kusababisha penati au kufungwa.
Mi nadhani hii hoja ingekuwa na maana kama hizo penati zingekuwa na walakini.

Kupata penati sio dhambi
Hizi penalties ni questionable sana.
Yaani saa hivi Simba haichezi mechi 3 mfululizo bila penalty.
Yaani suala la Simba kupewa penalty kila baada ya mechi 2-3 sio utabiri tena.
Ni fact...
Kama ingekuwa betting, possibility ya Simba kupewa penalty au kutopewa
Ni 1.70 Yes na 3.80 No
 
Na sio 8 tu Simba mpaka sasa walistahili kupata penalty si chini ya 12 ila ni uzembe wa waamuzi aina ya Kayoko ndio umepelekea Simba kudhulumiwa haki yao
 
Hizi penalties ni questionable sana.
Yaani saa hivi Simba haichezi mechi 3 mfululizo bila penalty.
Yaani suala la Simba kupewa penalty kila baada ya mechi 2-3 sio utabiri tena.
Ni fact...
Kama ingekuwa betting, possibility ya Simba kupewa penalty au kutopewa
Ni 1.70 Yes na 3.80 No
KWani sheria inataka timu ipewe penalty kila baada ya michezo mingapi angalau?
 
Back
Top Bottom