Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Vijana wa upinzani Tanzania hasa kupitia vyama vikubwa vya chadema na act wazalendo ,wamejikita twita! Wanadhani kwa mabishano na kelele za twita wanaweza kuleta mageuzi yoyote katika nchi hii !! Watu wenye akili na weledi na wapiga kura wa kweli hata twita hawapo na wengine hata hawaijui kabisa twita ,Vijana wa upinzani sijui kwa sababu ya uvivu kuanzia asubuhi mpaka asubuhi wapo twita kubishana ! Kuparuana na nakusherehesha mtandao kwa vimikutano uchwara vya online ! Wenzenu ccm wanajikita kwenye vijiji kutoa elimu mbali mbali kuhusu uchaguzi na kueneza sera za chama chao! Kijiji kwa Kijiji na hakuna kwa sasa Kijiji ambacho ccm wamekiacha yaani wametawanyika wapo mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba,jifunzeni matumizi mazuri ya ruzuku ! Matumizi ya ruzuku huwa kazi yake ni kujiimarisha kupitia kwa makundi mbali mbali ya chama ,timu zingekuwa zimetawanywa huku na kule ,lakini Leo anaeonekana anapambana ni mbowe na Tundu peke yao ! Kwanini wawe wao tu ! Ni kwa sababu ya ubinafsi wa kuogopa kutenga bajeti ya kuwezesha vijana kwenda kukipambania chama ! Kwa maana ya bawacha na bavicha ! Lakini inaonekana bajeti ya kifedha haitoshi kitu ambacho sio kweli ,matumizi ya ruzuku ya chadema ni ya anasa zaidi kuliko kukijenga chama chenyewe! Magari ya chama kwenye Kanda kwa sasa hayaonekani yaliko ! Haya yangesaidia kuzipeleka timu za hamasa vijijini ,sijajua yaliuzwa au yamefichwa sehemu ! Chama kimejaa ubinafsi kupitiliza ! Kama mtakaa kitako twita na kuwaachia kazi Tundu na freeman peke yao ,nawaambia pasi na shaka uchaguzi ujao hamtaambulia hata Jimbo Moja hata kama nyinyi ndio mtaruhusiwa kuhesabu kura na kusimamia uchaguzi na ccm wakalale nyumbani hamtachukua Jimbo hata Moja !