Wakati Feisal anawafanyia Yanga uhuni mashabiki wengi wa simba walimsuport haya sasa imetokea kwa Kibu Dennis wamsuport

Kwanini isiwezekane? Shida ipo kama atavunja mkataba kinyume na makubaliano katika mkataba.

Tutofautishe uungwana na takwa la kimkataba. Kukaa pande mbili na kukubaliana ni uungwana ila hiyo haimaanishi kwamba kama mchezaji akiamua kuvunja mkataba wake kwa kufuata sharti lililopo la kuvunja mkataba wake bila kukaa na wewe mkazungumza mkataba hauvunjiki, mkataba unavunjika vizuri tu.
 
Sasa kwa nini lisitokee, ikiwa kila siku wachezaji wanajiamulia na kujisikia watakavyo,juzi Fei, jana Dube leo Kibu,hujui itakuwaje siku zijazo.
Mkuu, mchezaji hajiamulii atakavyo, anafata mkataba wake mmekubaliana nini pale ambapo anataka kuondoka.

Kama mmekubaliana kuwa ili aondoke anatakiwa aandike barua ya kuvunja mkataba na alipe gharama za usajili plus mishahara ya miezi 12 yeye akifanya hivyo hata asipokuja kukaa na wewe kuzungumza tayari katimiza takwa la mkataba la kuvunja mkataba wake. Yaani hata wakifanya kikosi kizima inawezekana kabisa na timu yako itagawa p3 za bure kwa wengine usubiri msimu uishe.
 
Mtu mwenyewe wa goli moja. Si wamwache aende tu! Wanapungukiwa nini?
 
Kulipa ni swala jingine na timu inayo mmiliki kukubali hayo malipo ni swala jingine. Dube alitaka kuilipa Azam USD 100k,Azam wakakataa, Fei kailipa Yanga 110m Yanga wakakataa.

Ngojea tuwaone nyinyi, ikitokea Kibu akiwalipa kiasi atakacho jipangia wenyewe mtafanyaje, tunataka tuwaone mtakavyo chomoka.
 
Kulipa ni swala jingine na timu inayo mmiliki kukubali hayo malipo ni swala jingine. Dube alitaka kuilipa Azam USD 100k,Azam wakakataa, Fei kailipa Yanga 110m Yanga wakakataa.
Kama Dube hesabu alizopiga zilikuwa tofauti na makubaliano Azam wapo sahihi kabisa kukataa, ila unapokataa unasema unataka Tsh ngapi kulingana na mkataba wenu, Azam alikuwa sahihi kabisa. Fei alipokataliwa hakuambiwa alete kiasi gani mpaka raisi alipoingilia, na hapo ndo utofauti wa suala la Fei na Dube unapokuja.
Ngojea tuwaone nyinyi, ikitokea Kibu akiwalipa kiasi atakacho jipangia wenyewe mtafanyaje, tunataka tuwaone mtakavyo chomoka.
Kibu hawezi jipangia, akilipa pungufu tutasema hii ni pungufu inayotakiwa ni kiasi hichi.

MKUU, hapa hakuna kukomoana kuna maslahi. Umesaini mkataba, umeamua hutaki tena lipa kulingana na makubaliano safari njema huko uendako.
 
 
Na hizo ndio best option mambo ya kuvunja mikataba kihuni hakubaliki sasa hivi issue ya Feisali itatumika kama reference mpira hauta chezeka kwa style hii
 
Sasa nikuambie kiasi gani ili iweje, hii business kila mtu anaiendesha kwa style yake.Kuna dogo juzi kasajiliwa na Man kutoka Lille, ila dogo aliitaka Madrid. Lille hawakutangaza dau , walikaa kimya ila waliwaita mezani wanao mtaka, then Madrid kaja na Pound 25m,Man Utd kaja Pound 50m hatimae Man kampata dogo kutoka Lille japo dogo moyo wake ulitaka aende Madrid. What If Lille angesema dogo anauzwa kwa Pound 10m au 20 unazani Lille angeipata hiyo Pound 50m.Ndio maana Fei akapewa options ya kuileta timu inayo mtaka mezani.

Mimi nawasubiria kwa hamu tuwaone, mtatoboa, kwa style gani. Mimi najua unaruka ruka,ila alichofanya Fei ,Dube na Kibu ni uhuni.
 
Yaani wakati mkataba mna sign pande mbili alaf wakati wa kuvunja unavujwa pande moja? Hivi kweli hili nalo linahitaji kwenda shule?
 
Lile li mama tapeli liliwajaza ujinga na nyie mka jaa kwenye 18 zake, yaani ukijaribu kuvunja mkataba unakua usha vunjika? Basi Kibu yupo huru maana katoroka achaneni nae
 
Hata feisal alikua na uwezo wa kuvunja mkataba ndo maana mwishoni alifuata taratibu akavunja

Ila mwanzoni alifanya uhuni na imekua ni darasa kwa wachezaji wengine mfano wa dube na sasa kibu
Feisal hajawahi kuwafanyia uhuni yanga bali alifata matakwa ya mkataba shida ikaja kwa yanga kulazimisha wakae mezani wakati mkataba ulikuwa unajiekeza kila kitu, pili kusema baadae alifata nakataa, ishu ya fei iliisha baada ya maza kuingilia show ikabidi yanga waufyate
 
Yanga na azam walikaa mbona ilikua wazi bila kificho ndo sakata la fei likaisha
Kuna mda una-question uwezo wa mashabiki wa simba wanatetea mambo ya kijinga sana
Sakata la fei liliishia ikulu kila mtu anafahamu, hivi unazani yanga wana ubavu wa kumdindia rais wa nchi? Mzanzibari aliingilia kati ishu ya mzanzibar mwenzie.
 
Kibu is useless
 
Buy out clause haina concequences zozote, unanunua mkataba unasepa zako. Kikubwa ni kutoa notice ya ku activate hicho kipengele.
 
Kuna sehemu simba wamewekewa pesa na KIBU wakagoma?
 
Acha uongo kiasi cha kurudisha ili uvunje mkataba haamui mchezaji bali unapaswa kufuata mkataba unasrmaje, fei alifata mkataba unasemaje ila dube hakutaka kufata mkataba unachosema.
 
Sakata la fei liliishia ikulu kila mtu anafahamu, hivi unazani yanga wana ubavu wa kumdindia rais wa nchi? Mzanzibari aliingilia kati ishu ya mzanzibar mwenzie.
Hiki kiherehere cha Feisali ndio kiliwaponza mkadondokea shirikisho, mlipata nini baada Feisali kuondoka?
 
Utapiga porojo upigavyo lakini ukweli unabaki kuwa mchezaji ni MALI YA CLUB. Chochote mchezaji atakachotaka kufanya ni lazima kwanza amuhusishe Mwajiri wake ambayo ni club yake . Huwezi kuwa mchezaji unajichukulia tu maamuzi bila kuihusisha club Yako .

NAKUKUMBUSHA KUWA .
Thamani ya mchezaji inapangwa na kuamuliwa na club yake Na si vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…