Wakati Marekani ikijiandaa kupeleka binadamu katika sayari ya Mars, Serikali ya Tanzania ina mpango gani kuwapeleka raia wake?

Wakati Marekani ikijiandaa kupeleka binadamu katika sayari ya Mars, Serikali ya Tanzania ina mpango gani kuwapeleka raia wake?

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Marekani imepanga kupeleka raia wake huko sayari ya Mars ifikapo 2030s.

Urusi nayenyewe imepanga kupeleka raia wake Mars ifikapo 2040s .

China nao wamepanga 2040s kama urusi.

Sasa sisi serikali yetu inasubiri nini kwenye huu upande wa teknolojia ya angani? Mpaka sasa kimya hakuna kinachoendelea na muda unazidi kwenda.

Jamani, tunataka kwenda sayari ya Mars! Serikali ya Tanzania iamke sasa walau hata ifikapo na sisi 2040s twende Mars tukaanze kushika mashamba huko?

Screenshot_20220911-223433.jpg
Screenshot_20220911-223454.jpg
 
Kama kuwapa tu huduma za muhimu kama utilities (maji, umeme, gas n.k) na bima za afya wameshindwa halafu Rais anasema nchi ina madini ambayo hata mengine hayajui majina unategema kweli kupelekwa hata hapo Sudan?

Acha waende huko Mars watapunguza msongamano duniani.
Ndio maana nasema ifike muda serikali itambie umuhimu wa utafiti angani na kuanza kuchukua hatua.
 
Nioneshe japo kiwanda cha kutengeneza hata pangaboi la helikopta hapa nchini.

Unadhani wenzetu wamefika hapo kama ajali tu? Kwa mfumo wetu wa elimu wa kutafuta Tanzania One kila mwaka wa mtihani unadhani tutaweza hata kutengeneza koti la mwanaanga?

We need to invest kwenye elimu, tuwekeze katika tafiti, tuwekeze kwenye majaribio ya kisayansi kwa kuanzisha maabara ndani ya majeshi yetu, tuunde mamlaka huru za chunguzi za kisayansi na tuamini kuwa tunamuamini Mungu WETU.

Mengineyo ni ushuzi na kujilisha kunde tu
 
Tunajenga bado matundu ya vyoo kwa misaada.

Na madawati, safari za mars zingoje ngoje kwanza.
Huoni kuna umuhimu wa sisi kuwekeza zaidi kwenye teknolojia ya angani? Sasa kwanini tunasoma geography ikiwa hatuifanyii tafiti!
 
Nioneshe japo kiwanda cha kutengeneza hata pangaboi la helikopta hapa nchini.

Unadhani wenzetu wamefika hapo kama ajali tu? Kwa mfumo wetu wa elimu wa kutafuta Tanzania One kila mwaka wa mtihani unadhani tutaweza hata kutengeneza koti la mwanaanga?

We need to invest kwenye elimu, tuwekeze katika tafiti, tuwekeze kwenye majaribio ya kisayansi kwa kuanzisha maabara ndani ya majeshi yetu, tuunde mamlaka huru za chunguzi za kisayansi na tuamini kuwa tunamuamini Mungu WETU.

Mengineyo ni ushuzi na kujilisha kunde tu
Sure uko sahihi ila kwa hizi zama yote yanawezekana we can borrow technology from walioendelea sioni shida hapo.
 
Mataifa makubwa yamekuwa na kasi ya kuipambania mars. Sijui kuna nn wanaona kinakuja duniani.
 
Mataifa makubwa yamekuwa na kasi ya kuipambania mars. Sijui kuna nn wanaona kinakuja duniani.
Mars inaaminika itakuwa habitable for human na in a long run binaadamu wataanza kwenda kuishi Mars. Ndio maana inaitwa Mars colonization.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Yan nchi yetu yenyewe bado vilaka kibao leo hii tuwaze kwenda mars dah sio kwa nchi hii mzee!!
 
Back
Top Bottom