Kama Nchi kuna sehem tuliteleza, haiwezekani professor wa chuo kikuu anawaza kufuga kuku ili aongeze kipato chake, badala ya kutumia muda wake kufanya tafiti, , ndio maana wengi wanakimbilia kwenye siasa, siasa inatakiwa iwe ya mwisho kwenye vipaumbele vya Nchi.
Tuawafanye wana taaluma yetu wasiwe na shida ndogo ndogo kama chakula, usafiri, nk. watumie muda wao mwingi kwenye kufanya tafiti mbali mbali, sio kutumia muda wao kuwaza familia itakula nini, atasomeshaje watoto, mwisho wa siku productivity inakua chini.
Narudia tena, tuwekeze kwenye elimu na teknolojia weka siasa mbembeni, iwe ya mwisho, fumua mitaala ya elimu kuanzia chini primary hadi chuo kikuu, bado hatujachelewa,
Leo hii kenya wameanza kufundisha Coding/Programming primary school, sisi tumelala, Tembelea shule za msingi tulizo nazo nchini utatoa machozi, shule zimechakaa, mabati ya shule yamejaa kutu, ndani hakuna paving kumejaa vumbi,
Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi kwenye majiji unaweza sema hatuna watawala, serikali inashindwa kununua mabasi kadhaa yawe yanapeleka wanafunzi mashuleni na kuwarudisha jioni kweli? badala yake tumewekeza kwenye siasa, hayo ma v8, uzeni nunulieni wanafunzi mabasi kwa ajili ya usafiri, viongozi tumieni usafiri wa pamoja, badala ya kijinunulia ma v8, tumieni usafiri wa umma kama wanachi wengine tutaokoa mabilioni ya fedha za mafuta mnayotumia kwenye hayo ma v8,
Tuifanye elimu yetu iwe na thamani, chukua wanafunzi walio na ufaulu wa juu ndio wakasomee ualimu, wekeni mazingira ya walimu yawe mazuri, wapeni motisha walimu wetu, wezesheni miundominu ya shule za msingi na sekondari, ondoeni changamoto za usafiri kwa shule zetu za umma, mwanafunzi anakaa kuanzia asubuhi hadi saa nane mchana hajatia kitu mdomoni, akili ya kujifunza itatoka wapi.
Nchi haiwezi kuendelea bila kufanya tafiti na kuwekeza kwenye elimu/teknolojia. Tunatumia mabilioni ya shilingi kunanunua mifumo/systems za computer kwa wahindi, usalama wakati huo tunazalisha graduates wa computer science, na IT kila mwaka,
barabara na madaraja tenda wanachukua wachina, na vyuo vyetu vinazalisha civil engeneers kila mwaka, Tufumue mitaala ya elimu kuanzia chini hadi chuo kikuu, tuwape kipaumbele wahitimu wetu, hata hao walioendelea wamewekeza sana tu kwa wazawa,
Kwenye Hospitali zetu specialists wanawaza kupiga vijiwe kujiongezea vipato , wagonjwa wanahudumiwa na interns Doctors na Residents, badala ya kutumia muda wao mwingi kuwahudumia wagonjwa na kufanya tafiti,
Kama Nchi inabidi tujitafakari.