Unakutana na demu mkali. Unaomba namba ya simu anakupa. Kesho Unakuja kumpigia kumsalimia anaitikia fresh tu na masham sham kama yote.
Unamwuliza u wapi anajibu home. Unamwuliza lini tunaweza onana anakuambia hata muda huu mi fresh tu. Unamwuliza nikutumie nauli anasema tuma lakini si kwa namba hii voda wananidai. Ngoja nikupe namba nyingine. Unashtuka kidogo.
Anakupa unatuma tsh 5000. Anakuambia mwelekeze mtakapo onana. Kama ni gheto kwako au guest house. Unashtuka kidogo
Unamwelekeza ghetto anakuuliza unazo condom au mtapiga kavu kavu? Unashtuka kidogo
Hamu inakata. Why? Why? Kwanini? Mtu amekurahisishia unaanza mwona hafai unakatwa stim? Sisi wanaume hatujui tutakalo.