Wakati Tanzania tukisubiri Mvua, China wao wanajenga mito mikubwa kubadilisha Uchumi

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Dunia yabaki midomo wazi! Hii si mito ni mfereji ya China! Maajabu yanayowashangaza wahandisi wengi Duniani.

Mifereji yao ni mikubwa kuliko mito mingi ya asili Afrika. Ukiona utadhani ni bahari zinazopita katikati ya nchi.

China mpaka sasa imetumia zaidi ya dola bilioni 10 kujenga mfereji mkubwa wa maji wenye urefu wa maili 83 unaopatikana katikati ya nchi hiyo.

Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2027, na utafungua njia mpya za biashara ambazo zitaiwezesha China kuokoa takriban dola milioni 750 kila mwaka.

China ina mifereji ambayo inajengwa na binadamu ambayo kimuonekano ni mikubwa kuliko hata mito mingi, China hujenga mifereji kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Biashara na Usafirishaji
Mifereji huruhusu meli kusafirisha mizigo kwa gharama ndogo kuliko barabara au reli.

2. Kusambaza Maji
Baadhi ya maeneo ya China yana ukame mkubwa, hivyo mifereji hupeleka maji kwenye miji na mashamba.

3. Umwagiliaji wa Kilimo
China ina mashamba makubwa sana yanayohitaji maji ya uhakika zaidi ya mvua.

4. Kudhibiti Mafuriko
Mifereji husaidia kuelekeza maji ya ziada nje ya miji na maeneo ya makazi wakati wa mvua kubwa.

5. Kuongeza Uchumi
Mifereji hujenga miji mipya, bandari na maeneo ya viwanda kandokando yake.

6. Usafiri wa Kijeshi na Kimkakati.
Kihistoria, baadhi ya mifereji ya China ilijengwa kusaidia usafirishaji wa wanajeshi na vifaa vya kijeshi.

Kwa ujumla, China imekuwa moja ya nchi zilizofanikiwa zaidi duniani katika matumizi ya mifereji kama sehemu ya maendeleo ya uchumi, biashara, kilimo na usimamizi wa maji.

Ujenzi wa Mifereji Nchini China haukuanza leo wala jana.

Hii ni baadhi ya mifereji mikubwa na maarufu iliyojengwa na binadamu nchini China:

1. MFEREJI WA GRAND CANAL
Ulianza kujengwa karne ya 5 KK, ukapanuliwa sana wakati wa utawala wa Sui (581–618 BK).

Una urefu wa takriban kilomita 1,776, huu ndio mfereji mrefu zaidi duniani uliotengenezwa na binadamu.

Kazi zake ni kusafirisha bidhaa kati ya kaskazini na kusini mwa China.

Kusafirisha nafaka na chakula. Huu mfereji huunganisha mito mikubwa miwili iitwayo Yellow River na Yangtze River.

2. SOUTH TO NORTH WATER DIVERSION PROJECT.
Huu mradi ulianza Mwaka 2002, China ilidhamiria kujenga mradi mkubwa wa kupeleka maji kutoka kusini yenye maji mengi kwenda kaskazini yenye ukame.

Hivyo nia ya mfereji huu ilikua ni kusambaza maji ya kunywa, kusaidia viwanda, kupunguza uhaba wa maji Beijing na maeneo mengine ya kaskazini na kukuza kilimo.

5. PINGLU CANAL
Huu ulianza kujengwa mwaka 2022 mfereji huu mpya unalenga kuunganisha maeneo ya ndani ya China na yale ya Pwani ya bahari.

Hivyo lengo kuu ni kufungua njia mpya za biashara, kupunguza gharama za usafirishaji pia kuongeza biashara ya kimataifa.

20260508_170749.jpg
20260508_170752.jpg
20260508_170807.jpg
20260508_170804.jpg
20260508_170810.jpg
​
20260508_170822.jpg
20260508_170827.jpg

20260508_170824.jpg
downloadfile-28.jpg
downloadfile-31.jpg

downloadfile-19.jpg
downloadfile-30.jpg
20260508_170755.jpg
20260508_170758.jpg
 
Baadhi ya mito mikubwa nchini Tanzania ambayo inaweza kuwa na uwezo wa kuunganishwa au kusaidia miradi ya mifereji kwa ajili ya umwagiliaji, usafiri wa maji, uzalishaji wa umeme au kudhibiti mafuriko ni:

Mto Rufiji — mmoja wa mito mikubwa kabisa Tanzania, una maji mengi na unaweza kusaidia mifereji ya kilimo na usafiri.

Mto Wami — unaweza kusaidia umwagiliaji maeneo ya ukanda wa pwani.

Mto Ruvuma — una uwezo mkubwa wa miradi ya maji na kilimo kusini mwa Tanzania.

Mto Pangani — tayari unatumiwa kwa umeme na unaweza kuongezewa mifereji ya umwagiliaji.

Mto Kilombero — eneo lenye rutuba kubwa sana kwa kilimo cha mpunga na mazao mengine.

Mto Kagera — una maji ya kudumu na umuhimu mkubwa kwa kilimo na mazingira.

Mto Ruaha Mkuu — unaweza kusaidia kilimo na uhifadhi wa maji katikati mwa nchi.

Mto Malagarasi — moja ya mito mirefu yenye uwezo mkubwa wa maendeleo ya maji magharibi mwa Tanzania.

Tanzania Ina Mito Mikubwa Kuliko Nchi Nyingi Afrika. Kinachokosekana Ni Maamuzi ya Kujenga Mifereji ya Kisasa
​
 
CCM Ikiondoka Tanzania Tunaifikia China Kwenye Uchumi
Ripoti ya hivi karibuni imeonyesha Tanzania imeshuka kiuchumi ilikuwa kati ya nchi 10 za Afrika zenye GDP kubwa sasa hivi imeshuka hadi nafasi ya 11
 
Karibu irrigation scheme zote kubwa zimejengwa miaka hiyo kwa misaada ya wahisani. Huwa tunadhani vitu vizuri vinaweza kuja vyenyewe.
Nchi ya kutegemea wahisani haiwezi kuendelea

Wahisani hadi kwenye kujengewa matundu ya vyoo shuleni, nje ya choo bango linasoma USAID au UKAID

Mbunge anakuja na Land Cruiser LC300 ya milioni 500 kuja kuzindua choo cha msaada
 
mzee wa ubwabwa alisha waambia,akiingia ikulu ataifikisha bahari dodoma hamkumuelewa. basi nyie endeleeni kulalamika hivyohivyo na ccm lenu.
 
Baadhi ya mito mikubwa nchini Tanzania ambayo inaweza kuwa na uwezo wa kuunganishwa au kusaidia miradi ya mifereji kwa ajili ya umwagiliaji, usafiri wa maji, uzalishaji wa umeme au kudhibiti mafuriko ni:

Mto Rufiji — mmoja wa mito mikubwa kabisa Tanzania, una maji mengi na unaweza kusaidia mifereji ya kilimo na usafiri.

Mto Wami — unaweza kusaidia umwagiliaji maeneo ya ukanda wa pwani.

Mto Ruvuma — una uwezo mkubwa wa miradi ya maji na kilimo kusini mwa Tanzania.

Mto Pangani — tayari unatumiwa kwa umeme na unaweza kuongezewa mifereji ya umwagiliaji.

Mto Kilombero — eneo lenye rutuba kubwa sana kwa kilimo cha mpunga na mazao mengine.

Mto Kagera — una maji ya kudumu na umuhimu mkubwa kwa kilimo na mazingira.

Mto Ruaha Mkuu — unaweza kusaidia kilimo na uhifadhi wa maji katikati mwa nchi.

Mto Malagarasi — moja ya mito mirefu yenye uwezo mkubwa wa maendeleo ya maji magharibi mwa Tanzania.

Tanzania Ina Mito Mikubwa Kuliko Nchi Nyingi Afrika. Kinachokosekana Ni Maamuzi ya Kujenga Mifereji ya Kisasa
​
Kuna wale jamaa wanitwaga wabobezi wa uchumi na wasomaji wa takwimu za uchumi hapa wao hawaoni kabisa kuwa nayo hii mito ni fursa?! au bado wapo kwenye upembuzi yakinifu?
 
Wale Ni Genge La Uharifu Tu
 
Nchi inahitaji udikteta aina ya Magufuli kutukwamua hapa tulito sio hawa majizi wanaonunua Real Estate Dubai kuhujumu rasilimali za watanzania..
Umesema vyema yule mzee ana mapungufu yake kidogo alikuwa na maono
 
Kuna wale jamaa wanitwaga wabobezi wa uchumi na wasomaji wa takwimu za uchumi hapa wao hawaoni kabisa kuwa nayo hii mito ni fursa?! au bado wapo kwenye upembuzi yakinifu?
Tatizo la Tanzania kila kitu kimekuwa ni siasa, ukianza kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi lazima mpoteane. Nchi inaendeshwa kwa irani ya CCM!
 
Dunia yabaki midomo wazi! Hii si mito ni mfereji ya China! Maajabu yanayowashangaza wahandisi wengi Duniani.

Mifereji yao ni mikubwa kuliko mito mingi ya asili Afrika. Ukiona utadhani ni bahari zinazopita katikati ya nchi.

China mpaka sasa imetumia zaidi ya dola bilioni 10 kujenga mfereji mkubwa wa maji wenye urefu wa maili 83 unaopatikana katikati ya nchi hiyo.

Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2027, na utafungua njia mpya za biashara ambazo zitaiwezesha China kuokoa takriban dola milioni 750 kila mwaka.

China ina mifereji ambayo inajengwa na binadamu ambayo kimuonekano ni mikubwa kuliko hata mito mingi, China hujenga mifereji kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Biashara na Usafirishaji
Mifereji huruhusu meli kusafirisha mizigo kwa gharama ndogo kuliko barabara au reli.

2. Kusambaza Maji
Baadhi ya maeneo ya China yana ukame mkubwa, hivyo mifereji hupeleka maji kwenye miji na mashamba.

3. Umwagiliaji wa Kilimo
China ina mashamba makubwa sana yanayohitaji maji ya uhakika zaidi ya mvua.

4. Kudhibiti Mafuriko
Mifereji husaidia kuelekeza maji ya ziada nje ya miji na maeneo ya makazi wakati wa mvua kubwa.

5. Kuongeza Uchumi
Mifereji hujenga miji mipya, bandari na maeneo ya viwanda kandokando yake.

6. Usafiri wa Kijeshi na Kimkakati.
Kihistoria, baadhi ya mifereji ya China ilijengwa kusaidia usafirishaji wa wanajeshi na vifaa vya kijeshi.

Kwa ujumla, China imekuwa moja ya nchi zilizofanikiwa zaidi duniani katika matumizi ya mifereji kama sehemu ya maendeleo ya uchumi, biashara, kilimo na usimamizi wa maji.

Ujenzi wa Mifereji Nchini China haukuanza leo wala jana.

Hii ni baadhi ya mifereji mikubwa na maarufu iliyojengwa na binadamu nchini China:

1. MFEREJI WA GRAND CANAL
Ulianza kujengwa karne ya 5 KK, ukapanuliwa sana wakati wa utawala wa Sui (581–618 BK).

Una urefu wa takriban kilomita 1,776, huu ndio mfereji mrefu zaidi duniani uliotengenezwa na binadamu.

Kazi zake ni kusafirisha bidhaa kati ya kaskazini na kusini mwa China.

Kusafirisha nafaka na chakula. Huu mfereji huunganisha mito mikubwa miwili iitwayo Yellow River na Yangtze River.

2. SOUTH TO NORTH WATER DIVERSION PROJECT.
Huu mradi ulianza Mwaka 2002, China ilidhamiria kujenga mradi mkubwa wa kupeleka maji kutoka kusini yenye maji mengi kwenda kaskazini yenye ukame.

Hivyo nia ya mfereji huu ilikua ni kusambaza maji ya kunywa, kusaidia viwanda, kupunguza uhaba wa maji Beijing na maeneo mengine ya kaskazini na kukuza kilimo.

5. PINGLU CANAL
Huu ulianza kujengwa mwaka 2022 mfereji huu mpya unalenga kuunganisha maeneo ya ndani ya China na yale ya Pwani ya bahari.

Hivyo lengo kuu ni kufungua njia mpya za biashara, kupunguza gharama za usafirishaji pia kuongeza biashara ya kimataifa.

View attachment 3585739View attachment 3585740View attachment 3585741View attachment 3585742View attachment 3585743
​
View attachment 3585744View attachment 3585745
View attachment 3585746View attachment 3585749View attachment 3585750
View attachment 3585751View attachment 3585752View attachment 3585747View attachment 3585748
Talk about thinking outside the box is this...
Siyo ya kina kigwangala, usanii, ufisadi na wizi wa rasilimali na maliasili...
 
Back
Top Bottom