Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 42,806
- 95,701
Ha haaa kumbe ndo zaoKwa wakati ule ulikuwa ni kupata sadaka ila wengi waliamini ni kuhubiri injili
Sent using Jamii Forums mobile app
Ha haaa kumbe ndo zaoKwa wakati ule ulikuwa ni kupata sadaka ila wengi waliamini ni kuhubiri injili
Mimi nimeanza kufanya kazi za ajabu tangu Niko o level
Nimelima vibarua (NGESE, watu wa Mwanza wanalijua hili Neno) mashamba ya watu nikiwa na jamaa yangu tuliesoma wote, pia nimelima vibarua vya kupalilia viwanja vinavyozunguka nyumba za watu zile zinazojengwa.
Mimi pia nimelima bustani ili kupata pesa ya tuition, nilikua naomba maeneo kwa watu yaliyo karibu na mto, nalima chainizi jioni nikitoka shuleni namwagilia, zikikomaa nabeba mwenyewe napeleka mtaani kwenye beseni nauza, tena ilikua mboga yenye msaada mkubwa Sana nyumbani kipindi hicho mambo hayaeleweki
Mimi pia nimefanya saidia fundi mpaka fundi anakuambia wewe ni msaidizi wangu Sawa Tu na Mke wangu, but unakubali yote kikubwa upate 5000/= yako ya kutwa.
Mimi pia nimefanya kutindua ukuta ili kufanya pipe fitting kwenye nyumba za watu, Ila hii imenifanya nikutane na watu wengi Sana WA maana ambao naomba Mungu huko mbeleni wakawe na msaada kwangu hasa field niliyosoma.
Mimi pia nimefanya serving ya chakula kwenye harusi, hii alipewa mama aka_save chakula maana jirani yetu kulikua na mama anaepika chakula kwa kuchukua tenda kwenye maharusi, then anachukua watu mtaani wanapika na ku_save ukumbini, so Mimi ilibidi nikamsaidie mama ili kuficha Aibu na malipo yake ilikua 5000/= kwa siku nzima mpka sherehe inaisha.
Mimi pia nimeuza tambi (chichili) gengeni, maana Mzee alinunua kimashine cha kutengeneza hivo vi tambi nikaanza kutengeneza nikitoka shule then jioni napeleka gengeni nauza , na pesa ndogo ndogo nilikua napata kiukweli.
Kwa sasa nashukuru Mungu jamaa yangu tuliekua tunapiga nae hizo kazi ni afisa wa jeshi na nyota zake nyingi tu begani, na Mimi Niko huku nakula 80% za wizara Ila sina kazi hustle zinaendelea mtaani.
Sent using Jamii Forums mobile app
doh mkuu umenikumbusha mbali sn[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Daah mkuu umenichekesha Sana kazi ukapata faster tu
House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
Piga gereji za kutosha nimekuwa konda sana mpaka nikaweza endesha gari nilijifunza kupitia hapo hapo baadae nilifanikiwa kupata leseni nikaenda piga mishe za udereva haice bado ilikuwa changamoto [emoji847]japo nashukuru mubebe alikuwa akinisapoti sana
ye aliwahi kuajiriwa mapema japo sikutaka awe na wasiwasi na huzuni na Mimi maana alikuwa akijitoa sana pindi Niko final year ukicheki hana baba hana mama wote tulijuana orphanage ktk mkoa x mapenz yalianza toka tuko msingi [emoji3] daah kweli nilikuwa baharia mdogo .
mi koz yangu ilikuwa ya miaka minne ye mitatu alipomaliza akapata bahat ya ajira baada ya chuo nikaamua niende mkoa x kutafuta life hakupenda uamuzi wangu wala sikumuaga na nilikuwa simtajii nipo wapi dah nimepiga dayworker sana hapo nishamaliza chuo
Kupiga pasi ndefu kwangu ilikuwa kawaida nakunywa chai nzito na cha usiku nilikuwa nakula kiporo cha ugali nauchoma na chai na viazi vitamu vya kuchemsha hapo nimechimba kwenye shamba la watu
Kupiga rondo au kutembea kwa miguu usiseme mpaka kuota masagamba sikuwaga na nauli mpaka kobazi zikaisha ila nilikuwa navaa hivohivo kibishi
Nilikuwaga na suruali mbili na mashat matatu in short nilizoeleka na zile nguo kuna shati nlikuwa navaaga wananitania shati LA kijiji maana hilo hilo nilikuwa nikionekana nalo kwa sana ama kweli nilidharaulika
Nilipanga nyumba haina umeme in short haijamalizika vzur bomba pia LA maji halijavutwa ila kulikuwa na kisima kwahyo getho ni mwendo wa kibatali siku nyengine nala nje kwenye baraza la jiran kufata mwanga sometimes akiniona barazani anazima taa au napika maeneo ya nje ambao mwanga unafika nikikosa hela ya maftataa yaani kulala Giza ilikuwa kawaida
Nyumba yenyewe madirisha jamaa hajaweka wavu ameweka nondo ikabidi nizibe na safleti sasa hao mbu walinipiga doso kisawasawa plus baridi sina godoro nalalia hzo nguo zangu chache kuna siku sikuonekana nje siku nzima kumbe Niko ndani naumwa yalikuwa malaria ktk vitu nilivyojifunza Cheka na kila MTU tenda mazur kuwa mtiifu ata kama Fulani anakushambulia sababu kuna vijana na watu walikuwa wakinikubali walikuwa hawanioni wakapata wasiwasi wakachungulia ndani wakaniona ktk ile hali walinisaidia kunipeleka hospital
Mtaani kuzushiwa wizi na kina mama,Dada,baba majirani ambao Niko nao karibu kuitwa kwa mwenyekiti daah we acha tu na Yale manywele yangu yamekuwa makubwa hayana afya sina ela ya kunyoa ukicheki na nguo zimechanika utasema muhuni
Kwenda kusaidia wavuvi kuna kipindi ngalawa au chombo chetu kilipigwa na wimbi yaani tulijua tunakufa tukaanza kutoa maji na visada we acha tu .ukitoka hapo unapewa buku mbili na kisado cha uono
Maisha yalivyonizidi nikasepa nikadandia fuso yaani kweli nilikuwa mpuuz nadandia fuso litakaponipeleka ndo hapohapo na kifuko changu cha nguo (zile adidas za mgongoni) nilishawahi fika mpaka huko singida mpaka shinyanga nilikuwa nalala stendi asubuh kazi na kutafuta vibarua nakumbuka kuna mzee nilizoeana nae hapo shy mjini akanikaribisha kwake nikawa House boy
Daah hiyo mikazi ni balaa baadae akanipa baiskeli niwe bodaboda nimletee ela ( boda boda za baiskeli ) sjui kama sahiv zipo mkoa kama dar hamna na tanga zilikuwepogo nilikuwa shy twn
Ila kuufatilia magezeti kuuliza connection na wale niliosoma nao nilikuwa sichoki baadae nikasave save nikaanzisha genge lilinipa ela sana nikaeka na kibanda cha chipsi pemben pia nikamwambia mke wa yule mzee awe anatengeneza juice nimuuzie hapo tayar nishajichomoa kwake nilipata faida sana
Mungu hamptupi mja wake nikapata nafasi kwenye kampuni x INA deal na mambo ya agribusiness genge na mtaji nikamuachia mzee nikamwambia undugu kufaana sio kufanana nikapotea shy na nauli na faida tu hapo ndo nilijiwekaza sana kwenye Hio kampuni sikufanya makosa [emoji3]inaitwa fungulia mbwa nilikula mema ya nchi halafu siku narudi natoka shy nakutana na mpenz wangu namuhadithia alilia sana na alinilaumu sana kwa nn sikutaka msaada wake wakat huo na yeye alipiga hatua sana mi baharia nilikuwa napigika tu [emoji3]
Nb: kama ningejua yaan kama ningejua nisingekubali kuajiriwa pale kwenye ile kampuni bora ningepiga mishe zangu hapo hapo paliniletea maumivu kuliko kote ...the rest is history
Nowdays Niko good sina shida sina stress laifu linaenda
Sent using Jamii Forums mobile app
And yes kujibu swali la Uzi nishawahi kuwaza niwe jambazi nitumie silaha kama panga visu nk
Kwenye hii post mkuu unaonekana upo real, post nyingine huwa masikhara mengi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaha
huyo mpenzi wako ulikuja kumuoa? Kama Hapana siku hizi yupo wap na wewe umeoa?
Alikufa akiwa mjamzitoHi
huyo mpenzi wako ulikuja kumuoa? Kama Hapana siku hizi yupo wap na wewe umeoa?
Duh nini kilimuua? Ujauzito ulikuwa wako?
Hahha ungekataa wali huo mkuu ungerudi unatambaa mana dar njaa inaumaga mpaka unajiuliza na mkoani wanajiskia njaa kiasi hiki?Nilipigika ikabidi nikachukue mashati ya buku buku tandale, nikanyosha vizuri nikaenda kuuza kinondoni hadi baharini bila kuuza hata shati moja, wakati huo sina hata mia na njaa inagonga kishenzi.
Mwisho wa siku nikaenda kwenye mti jirani na aghakan nikaanza kupumzika huku napata upepo wa bahari mida kama ya saa tisa alasiri hivi.
Baadae kidogo akaniamsha dada mmoja ana wali ambao umepakiwa kabisa kwenye vile vifungashio, akanambia alikuwa na oda kwa mafundi sasa mmoja hayupo na chakula kishalipiwa, na akasema aliniona toka nikiwa kwa fundi viatu jirani na AZANIA BANK maeneo yale yale ya agakhan.
Nikajisemea moyoni hapa inabidi nisiigize kama desturi ya sisi waafrika, kitu unataka halafu unasema ahsante nimeshiba! Nikamwambia ahsante sana, kweli nilikuwa na njaa.
Niligonga ule wali ndio akili ikakaa sawa (yaani njaa ikizidi hata akili inakuwa na mawenge)
Safari ya kurudi home ikaanza na nikaja kuuza shati moja kwa 2000 pale salander bridge jioni kabisa.
Haha mkuu ukataka uanze kazi hata jumamosi tu,hongera kwa kuwa mvumilivu aise.Nilipitia kipindi kigumu sana hadi nguo ziliisha na ilibidi hata wakati wa kukaa Navizia maana ikipasuka tu, kiraka kitanihusu na pesa ya kiraka sina, muda huo huo suruali zilikuwa 2 na hapo ni graduate. Asiwaambie mtu wanajf, nilikuwa naamka ucku nawaza na ndugu pamoja na rafiki walinikacha kisa mkwanja. Niliwaza kufungua biashara ndogo ya kuuza half cakes kupitia vijana wanaotembeza maana naishi mjini. Nikande ngano na vijana wangu na waende kuuza na kuwalipa kitakachopatikana. Ila nilishindwa maana sikuwa na pesa na pia sina nyumba kwani nakaa kwa mama, na mama ananidharau na watoto wake. Ghafla nikapigiwa simu na rafiki yangu wa zamani sana kuwa nikafanye interview katika kampuni moja katika huo mji niliokuwa naishi, nikaenda na nilikuwa peke yangu, nikapigiwa simu kuanza kazi.
Unaambiwa ilikuwa saa 11 jioni mdada aliniambia..... nanukuu " When you expect to start your new job" Nilimjibu hata sasa hivi, mdada alicheka sana kwani ilikuwa jumamosi ila aliniambia tulia Mr. Baadae akaniambia utaanza jumanne ijayo na nimetuma offer kwa email yako, isaini na baada ya hapo uanze kazi. Sasa nashukuru nguo nimenunua, simu ninayo, dharau zimeisha home, nashukuru heshima imerudi.
Funzo: Usimdharau aliyesoma hasa mwenye elimu kuanzia degree 1, pia nikagundua kuwa nguo zikichakaa huwa zinawahi kuchafuka na zinachelewa kutakata unapozifua.
Tusomeshe watoto, huu ndio urithi pekee.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee si mchezo,umenikumbusha niliona habari wana wamebeba magunia ya bangi kwenye ambulance ya hospitali [emoji3][emoji3][emoji3]Dah maisha haya nakumbuka miaka kadhaa baada ya kumaliza elimu ya msingi nikashindwa kuendelea japo nilipenda kusoma ila sikuwa na kitu nikaingia kuchimba kokoto maeneo ya kunduchi dah jua kali ila ninakomaa tu nikapata ka elf 20 ndio nikapewa mchongo wa kusafilisha bangi kutoka masasi na hapa ndio nilipopata mwanga wa maisha mpk sasa hivi nipo vyema japo biashala hiyo nishaiacha miaka 6 nyuma ila nashukulu Mungu miladi niliyonayo inanifanya niishi kidon mjini hapa na kuheshimika juu
Huyo ni rafiki wa kweli,anaelewa Risk zake na hakutaka zipate wewe rafiki yake.Jamaa nimemkubali sana.Mwaka 2013 nimerud chuo baada ya Kuahirisha mwaka 2012, nipo hapo kwa mwanangu Kino Shamba sina be wala che hapo chuo ni city centre. Kule bila pesa hakukaliki, nikapiga hesabuuuuuu nikasema hataaa!
Wacha nimfike mwanangu aniunganishe niwe Punda, hapo nikawa nshapiga hesabu chsp, nikipeleka mzigo mara 4, hapo tayar nina ada na pesa ya kutumia mpaka namaliza chuo. Nikamfuata mwana nikamuelezea akanijibu tu
Siwezi kukunganisha ukabebe unga nikupoteze, wewe kama maisha magumu, we kaza tu. Aliponambia hivyo nikayachuja yale manenoooo nikaisikia sauti ndani mwangu ikinambia nisihifu kila kitu kitakaa sawa