JINSI NILIVYO INGIA KWENYE ISHU ZA KUUZA BANGI ENZI HIZOOO MIAKA HIYOO
Maisha yangu yalikuwa ni mpole sana sio mtu wa kuji mix sana ilikuwa nikitoka zangu chuo naenda getoo nikifunga mlango basi kufungua either ni dukani au chuo kila kitu nilikuwa nafanyia ndani.
Basi baada ya kuishi maisha hayoo nakumbuka siku moja nilipata jirani ambaye tulikuwa tuna soma nae so akawa kama jamaa yangu wa karibu sana.
Akafanya nikawa natoka nje mara kwa mara sasa mimi nilikuwa mtu wa movie sana yani kila week lazima niwe na movie mpyaa. Ila jamaa yangu alikuwa hawezi yeye ni mziki tu kila mda.
Sasa katika kupiga story na jamaa akasema yeye sana anapenda WEED yanii ni kama kila kitu kwenye maisha yake mimi nikawa namshangaa nikaona sio kesi kaniuliza mimi, mimi nikamjibu kuwa ni movie,music, na tech basi. Akanidadisi mpka akajua natumia kilevi sema sio sana.
Sasa miezi imeenda kumbe jamaa alikuwa anatoka jioni anaenda kwa rasta anakula ganja anarudi ana lala sasa alipo karibia kufulia hapo ndo ishu za biashara zika anza. Na kumbe jamaa alikuwa ametumbua adaa kiasii kama nusu hivi.
Siku moja niko ndani na sikiliza album ya Ace Hood - Trials & Tribulations naimba kipande cha HOPE akanifuata akaanza kuonge jinsi ya kupiga pesa. Kiukweli nilikuwa naitikia ila nilijua hawezi fanya ishu ya ganja tukakubaliana kuwa mimi nita kuwa nauza yeye angependa mimi kwasababu situmiii nikasema sio kesi.
Siku ya siku jamaa akaleta stock pisi 50 kama kuangalia soko. Sikufichi hakuna siku nilitetemeka kama naona bangi live na kidogo nikatae na kwa nchi za watu mgeni ukikamatwa ukitupwa jela sahau maana kesi yako ni moja kwa moja unaweza usipitie mahakamani. Na lugha yaoo ndo kuongea huwezi basi.
Nikafunga mlango cha kwanza nikafichaa nikamwambia jamaa asepe anipe mda na nione inakuwaje.
Nikaweka zote juu ya dali na kulikuwa na giza basi niliweka kwenye kona kabisa so mteja akitaka mimi napanda darini natoa namletea.
Week ya kwanza tu stock imeishaa
50x 1000= 50,000
Ila yeye ali nunua kwa 25,000 cash so faida ni nusu.
Akanipa 10,000 fresh.
Akaona kabisa hapa kuna soko akaenda kuleta pisi zaidi ya 100 hata week haijaisha mzigo umekata.
Kiukweli nilikuwa si lali kuna jamaa alikuwa anakuja anatoa 10k anachukua kumbe na yeye anaenda kuuza anapata 15k.
Kilaa baada ya 15 minute mtu anataka hiyoo ni kwakuwa nilikuwa nimezungukwa na wa Nigeria na wakenyaa.
Kuna mda sasa nikaanza kupokea watu siwajuii habari ikaanza kuenea kuwa nina product safi, na jamaa akienda kuvuta sehemu mpyaa anawaambia kuwa nauza.
Basi jamaa akanifuata akaniambia ngoja aonge na jamaa kuwa amtengenezee pisi zaidi ya 300 nikasema sawa mimi sina noma.
Week inayo kuja zikaja stiki dhaa nikajiuliza HIVI NIKIDAKWA INAKUWAJE maana zilikuwa zina tembea balaa.
Nikachoka ile ishu ya kupanda darini kwenda kuchukua stiki ikabid ni buni njia mpyaaa ya hapo hapo ndani kwangu.
Nikachonga kopo la shuga kwa ndani nikatengeneza uwazi nikawa naweka kule stick 50 tu basi. Ila nilikuja kutoa baada ya majamaa kuja na kufungua mara kwa mara.
Nikaona dawa ni kuweka kwenye kopo la vim vim zile za chooni kama unazijua. Basi ndo ikawa depot yangu mtu akija naingia toi kwenye kopo la vim natoa fastaa nampa.
Siku moja niko nje nimekaaa tu sina ili wala lile nasubiria wateja waje kama kawaida napika msosi taratibu niko na eagle lager pembeni ghafla naona jamaa anakuja.
Ananiambia kuwa nimpe ganja nikamuambia mimi siuzii akanikazia kuwa nauza nikamwambia siuzzii mzee, mpaka hasira zikanishika akasema kuna siku aliona nauza nikamwambia mimi sijawahii wala kuwa interest na bangi hata hapo nilikuwa na hofu kuwa jamaa atakuwa amatumwa nini? maana sio kwa kujiamini kule. Akawa kama anafoka kwa mbali
Basi akasepa akaenda jirani akatoa pesa akamtuma mtu anaenifahamu akaja akanunua ndo akamtambulisha na akasema huyu ni mkenya dhaa ndo akili ikakasawa, tukapiga story basi akawa mteja,
Kama unavyo jua sio kila mtu atakupenda kwa kila jambo.
Kuna watu walienda wakaongea na police kuhusu ishu kuwa kuna muuza NIAJE maeneo yetu sema sasa huyo mmbea hakupeleka taarifa inavyo takiwa asubuhi na mapema ndo siku ya police kuja mimi nilikuwa sijuii ila mungu mkubwa huwezi amini siku hiyooo niliamka mapema kuliko watu wote pale eneo ninalo ishi.
Akaja jamaa kavaa kiraia akaniambia kuwa anataka bangi na mimi nilikuwa simjuii kumbuka kakutana na pusha mwenyewe nikamwambia huku hawauzi ila akasema kuwa kuna mtu kamwambia kuwa kuna kuna kijana anauza maeneo haya nikasema huku hamna labda tu wavutaji na sio mwengi ni wa sudanii na sio eneo hilii ni upande wa nyuma huko nikawa namuuza ghafla naona akarudi nyuma kumbe defender ilikuwa iko mitaa hiyo nikatoka nikaenda dukani nikaona askari kama 6 yani nilikuwa sina uoga hata kidogo.
Kucheki naona jamaa wawili nawajua na mmoja ndo ananifahamu sema sina urafiki nae sana nahisi aliwaambia kuwa ndo mimi, ile naingia getini naona askari wanakuja nyuma taratibu,
Si kwenda kwangu nikaenda kwa jamaa yangu wakasimama kisha wakaenda mitaa ya kwangu. Nikasema leo ndo leo sikimbi hapa lazima nisimame kidete basi askari mmoja alikuwa anajua Kiswahili tukaongea hapo ndo alikosea kabisa.
Nilikuwa najiaminiii sana nikamkaribisha ndani nikamwambia afande kagua kimoja kimoja paka urizike ila naomba umuite boss wa hiii eneo kwanzaa basi kaja msaidizi wake akasema huyu jamaa yeye sio nan i ungo na hili eneo hakuna muuzaji na huyu ni mtu wa mademu tu.
Basi polisi wakacheka mmoja akaingia hadi chooni kuangalia akakuta hamna kitu ni vikorokocho tu vya toi kumbe ndo sehemu naweka bidha wakaondokaa.
Yanii tokea story police walivyo kuja kuenea nilikuwa nauza balaa piss 300 week haishii nisha malizaaa
Baadae tukaja kukosana na jamaa kisa kidogo tu maana mimi nilimwambia ukija kwangu hata kama mzigo ni wako njo na cash basi akilewa anakuja na jamaa zake siwajuii anaropoka nimpe zagaa na wanavuuta mlangoni kwangu basi tukapishana kauli mara kwa mara na nilimuambia kuwa nataka tupige pasu kwa pasu maana mimi mda wangu unakuwa finyu tofauti na wewe akagoma akadai yeye ndo boss na kama siwezi nirudishe biashara yake kwake.
Basi nikaona sio mbaya maana urafiki ulipungua jamaa wakamjaza ujinga wakadaii kuwa ninabaa ukubwa wa stick. (napunguza kwa kila stick kisha na roll zangu pembeni kwao nawauzia ndogo na sioo haki)
Akachukua nikarudi kwenye maisha yangu huku nikiwa nimepunguza mzigo mkubwa ada na kodi
Nilinunua vitu nilikuwa sina pamoja na PC mpyaa vitu baadhi
Jamaa week moja tu biashara ili mshinda maana alikuwa anavuta sana gari moshi ikasome, jamaa zake wakija anatoa bure wanavutaa weee akaja akakamwatwa na polisi kila siku kesi akaondoka sijui kaishia wapi ila alifungwa miezi 4 mzee wake akamtoa.
Alinitumia msg tu
“Mr. am regretful for every think that happen to the past between me and you I was unwise enough”
Sent using
Jamii Forums mobile app