Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Mkuu japo kitambo sana... Naomba kujua hizo ped za kufua haziaribiki ukitia maji..? Wanunuaji hawazigundui..? Ulikua unazitoa wapi..? All in all pole sana umepitia life gumu ktk utafutaji
Nimsaidie kujibu, ni material ya vitambaa
Ipo hivi
1660087876878_100.jpg
Screenshot_20220810-023059_KiKUU.jpg
 
Nilikuwa nimemaliza kidato cha sita nikachukua likizo ya mwaka
Usiku kucha mkononi panga na tochi kwenye mashamba ya mpunga na vitunguu unapambania maji ili mazao yasikauke mda mwingine ukiwa unatumia mashine kunyesha inabidi ulale pembeni ya wando wa mfereji mpaka aliyeko shambani amalize au kama mnanyesha kwa zamu unalala sehemu ambayo maji yatapita ili yakifika pale uamke na hizi shughuli zote zilikuwa zinafanyika kuanzia saa tano usiku mpaka saa moja asubuhi.

Mara ukiwa unafungulia maji yaingie kwenye majaruba fisi anapita mbele yako, nyoka kwenye majani ndio usiseme ukitoa kupiga dawa kwenye vitunguu unanuka zaidi ya choo cha stendi.

Nikaweka na kiapo sitawahi kushika tena jembe kulima chochote .
 
Nimemaliza form six niko kitaani sina mbele wala nyuma, nimefaulu ila chuo sikuweza kwenda home hawakuwa vizuri. Nikaona nijichanganye mtaani maisha yaende, nikaenda kiwanda cha hizi sabuni za Kleesoft kipo Kibaha kule ndo kilikuwa kimeanza anza, asee kupata kazi ilikuwa mtiti...nikaunganishwa na jamaa mmoja hivi ni in charge mule ndani jamaa kuniona akacheka kwanza, akaniuliza mdogo wangu unaweza kazi?! Nikamwambia ndio naweza, akanambia twende nikakuoneshe kazi iliyopo, aseee nikapelekwa sehemu vipo vipande vya watu vinachimba mashimo sijui ya nini yale.
Jamaa akaniuliza tena mdogo wangu unaweza kuchimba shimo urefu wako?! Nikajitutumua tu nitaweza ila kiukweli nisingeweza hata kidogo[emoji28]. Akanambia basi niachie namba zako nitakupigia, aah wapi jamaa hakunitafuta wala nini.
 
Kuuza viatu vya matairi round about mwenge, huku kipindi hicho wife alikuwa anakuja kunipa company, ananinulia mahindi ya kuchoma

Kuzoa takataka maeneo ya toangoma, kibada na mkiwambe miaka ya 2015 kuna siku nilikutana na mwalimu na mwalimu wa.programming akashangaa.. nkasema maisha propose maana software wqhindi wqnatunyonya

Kuwa dalali wa mboga za majani wakati nafanya internship kampuni ya bima ya afya, napita mabonde ya mbagara nachukua bahia kwenye ndoo kwa bei nafuu naweka kwenye mifuko zile rambo nyeusi zilikuwa zinauzwa 50 ( fungu la buku bamia za kutosha kama 30) kipindi kile bamiq zilikuwa nyingi ndoo kubwa elfu 5, faida unapata hata 10,000.

Saidia fundi, kubeba tofali hii ndo sirudii hata maana unachukua tofali unakimbia nalo unampatia fundi anajenga kozi juu ya linta

Kuanzisha mradi ya kuzalisha funza,kwenda feri kuchukua utumbo wa samaki na kuufanyia mafekieche uoze na utoe funza the ukaushe uwauze funza( kuna siku nilikuwa kanisani kitoto cha kishua kinamwambia mwanangu Pole baba yako ananuka uvundo.. nilitoa tusi mpaka mzee wa kanisa akacheka)

Anyways kazi zote hizo nilikuwa napga bado niko pembeni na mama watoto.

Mungu kanifanyia kicheko
Una mke mwema ana akili mwerevu busara na hekima... Endelea kumtunza... Sisi wengine tuliokota vituko
 
Nimerudia kusoma ×5

YAANI UMESEMA

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Then umeachishwa kazi huna kitu.

Hivi ni sijaelewa au sijasoma vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Unashangaa huyo wa mil 2.8.. wabunge wa mil 10 plus mwisho wa siku wanaishia kuwa makapuku je
 
Nimemaliza form six niko kitaani sina mbele wala nyuma, nimefaulu ila chuo sikuweza kwenda home hawakuwa vizuri. Nikaona nijichanganye mtaani maisha yaende, nikaenda kiwanda cha hizi sabuni za Kleesoft kipo Kibaha kule ndo kilikuwa kimeanza anza, asee kupata kazi ilikuwa mtiti...nikaunganishwa na jamaa mmoja hivi ni in charge mule ndani jamaa kuniona akacheka kwanza, akaniuliza mdogo wangu unaweza kazi?! Nikamwambia ndio naweza, akanambia twende nikakuoneshe kazi iliyopo, aseee nikapelekwa sehemu vipo vipande vya watu vinachimba mashimo sijui ya nini yale.
Jamaa akaniuliza tena mdogo wangu unaweza kuchimba shimo urefu wako?! Nikajitutumua tu nitaweza ila kiukweli nisingeweza hata kidogo[emoji28]. Akanambia basi niachie namba zako nitakupigia, aah wapi jamaa hakunitafuta wala nini.
Noma sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..

Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu

Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.

Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..

Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..

Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!

Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..

Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..

Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana
 
Baada ya kusoma comments za wadau nikipata muda nitadrop a true story about my jobless life since 2020 nikiwa chuo pale UCC

Based on a true story kuanzia maisha yangu ya chuo, maisha yangu ya forex na msoto niliopitia baada ya kufilisika kwenye forex mpaka nikaingia site nakujifunza ufundi, kubeba zege, kubeba tofali, na saidia fundi mpaka sasa mm ni mason japo sina uzoefu mkubwa...

In general afya ndio mtaji wa kwanza wa mwanadamu, fanya vyote ila usisahau kuilinda afya yako
 
Back
Top Bottom