Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Habari za muda huu wakuu, naimani mko poa na January inaendelea kuyoyoma. Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu.

Kwanza kabisa lazima tukubali kuna muda mtu unapigika na life hadi unaanza kuwaza kazi za ajabu au ambazo hukuwahi dhani utayafanya. Wengine wanafikia maamuzi na wanafanya, na wengine wanaishia kuwaza tu na kabla hawajafanya wanabadili maamuzi au wanapaka kazi nyingine ya kawaida.

Binafsi wakati nimemaliza elimu yangu ya hali ya juu Dar es salaam nilipitia wakati mgumu sana kimaisha kwani sikuwa na wakumtegemea. Nilikuwa napenda sana kuingia JF kujipotezea mawazo.

Siku moja nikakutana na uzi wa jamaa fulani akidai kuwa amepata mchongo wa kuigiza video za kikubwa huko majuu na akadai kuwa yeyote atayehitaji yupo tayari kumuunganishia.

Kiukweli nimelelewa vizuri tu lakini ilibaki kidogo tu nimtafute jamaa aniconnect nizame majuu. Lakini huwa napenda kufanya utafuti wa jambo kabla halijafanyika, hivyo nikazama Google kutafuta undani wa industry ya video za kikubwa.

Nikafahamu mengi sana, faida na hasara, gharama wanazolipa na mambo kibao, mwisho wa siku sauti ndani yangu ikawa inakataa sana hizo shughuli, basi nikaacha nikapambana kutafuta ishu nyingine.

Je wewe ni kazi gani ya ajabu kwako ulifikiria kuifanya kipindi ukiwa huna kazi na life limekunyoosha.

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutembeza vyombo dar ...***** hamna kazi pale kuumia tu
 
Nakumbuka nimemaliza chuo2008 ,nikawa nipo tu home kila siku asubuhi baba wa kambo anafoka sana , na kuanza kutuambia msidhani mpo kwenye urithi wa malinzangu

Maneno yale yalikuwa yananiumiza sana ikanilazimu kwenda kutafuta kazi ya bar , nikawa counter pale kwenye bar

Yaani ugomvi matusi , kudharauli yote yakawa yangu ...usiku nalala mlemle kwenye bar sikutaka kirudi home kwa maneno yale ya mzee wetu!! Ila kazi ikawa na changamoto ukitembea tu na bamedi (sex)dharau zinaanza


Kipindi nipo pale bar nikabahatika kufahamiana na askari game watatu !! Wakawa mabest sana yaan hata kama hawana hela nawadhamini wanakunywa bia ,mwisho wa mwezi wanalipa ....

Wakanipa wazo si tuwe tunaenda na ww kwenye doria tukipata kitu tunakupa kidogo nikawaambia poa!! Ilikuwa ni kambi ya KIJERESHI

Ikawa ikifika uck km siku ya doria namuachia mdogo wangu wa pili ananisaidia kuuza pale bar ,maana tulikuwa kama makinda tukiugua mzee mara agome kutupeleka hospital ,nguo alikuwa hataki kbs ..kutuona tumevaa nguo nzuri [emoji24][emoji24][emoji24]

Tukawa tunaenda doria tukikutana na watu wameingia kwenye eneo la hifadhi tunawanyanganya kuni ,baskeli na kipigo juu kazi yangu ilikuwa kuigiza mizigo kwenye gari .....

Siku moja moja na wao walikuwa wanawinda nyati ,swala au nyumbu wananipa nyama naiuza ...napata hela kidogo kidogo natunza

Nilipokuwa mzoefu ......nikamfata gemu mmoja jina kapuni nikamwambia sasa si unifundishe kutumia bunduki tukawa tunaenda porin wananifundisha shabaa tukiwa tuna winda ..nikawa konki wa L4 ,kuitumia akanifundisha kuifuta na kuifungua

Baadae nikatafuta ya kukodi kwa mtu x alikuwa nayo na lisasi alikuwa akiniuzia moja sh 15000/- imeandikwa mzinga .ganda jekundu ..na zilikuwepo za kupigia tembo ganda jeusi ....ukimchapa na hiyo anaanguka

Nikaanza uharamia wa kuingia porini kwa kuwa nilikuwa na ratiba kamili ya askari game kufanya doria , nikawa nikikutana hata na mzoga wa mnyama nauchukua naupaka chumvi nyingi naukausha juani halafu ...nikirudi mjini natembeza mji kwa mji nyama ya porini watu walikuwa wakiipenda sana iliitwa vimoro

Nilitengeneza hela sana !! Tamaa ikanizidi bwana wakaja wasomali walielekezwa kuwa wakija kwangu hawatakwama njia nyingi nazijua

wanataka niwapeleke porini walikuwa na warundi na land cluzer ambayo ilikuwa na turbo na matenk mawili ...wakiwa na bunduki A.K 47 , NAbunduki moja inastand na mkanda wa risasi wakanilipa dola 250

Walikuwa na gari mbili kenta na land cruser tukaenda nao bwana tukapitia kijiji kinaitwa kijereshi tukaingia kwenye hifadhi ya serngeti

Ilikuwa mida ya saa moja saa tatu usiku jamaa walikuwa wana mwaga risasi kama karanga hawaangalia mnyama mkubwa mdogo !!

Baadae wakawa wanachambua wanyama wanatupia kwenye kenta mpk ikajaaa , kumbe askari game walisikia milio ya risasi wakaja aise ......zilitembezwa risasi na wale maharamia wa kisomali bunduki ilikuwa inashikiliwa na watu wawilo ....

Game wakazidiwa kabisa tukaondoka tukarudi mpk lamadi wakaniacha mida ya saa 8 usiku wakacha mwendo tokea hapo nikahapa sitakwenda porini

Maisha haya nikajikuta nimetengeneza km m1 ....yaani mpk naenda kulipot kazini tarehe 1-09-2009 ..
Nikawa nipo vizuri sana

Mafanikio ya mtu yanatengenezwa na kujitoa sadaka !! Siwez kusahau



sent from toyota Allex
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] inachekesha..wazee wakazi walimwaga risasi za kutosha..mjegejo Ni hatari
 
Piga gereji za kutosha nimekuwa konda sana mpaka nikaweza endesha gari nilijifunza kupitia hapo hapo baadae nilifanikiwa kupata leseni nikaenda piga mishe za udereva haice bado ilikuwa changamoto [emoji847]japo nashukuru mubebe alikuwa akinisapoti sana


ye aliwahi kuajiriwa mapema japo sikutaka awe na wasiwasi na huzuni na Mimi maana alikuwa akijitoa sana pindi Niko final year ukicheki hana baba hana mama wote tulijuana orphanage ktk mkoa x mapenz yalianza toka tuko msingi [emoji3] daah kweli nilikuwa baharia mdogo .


mi koz yangu ilikuwa ya miaka minne ye mitatu alipomaliza akapata bahat ya ajira baada ya chuo nikaamua niende mkoa x kutafuta life hakupenda uamuzi wangu wala sikumuaga na nilikuwa simtajii nipo wapi dah nimepiga dayworker sana hapo nishamaliza chuo


Kupiga pasi ndefu kwangu ilikuwa kawaida nakunywa chai nzito na cha usiku nilikuwa nakula kiporo cha ugali nauchoma na chai na viazi vitamu vya kuchemsha hapo nimechimba kwenye shamba la watu

Kupiga rondo au kutembea kwa miguu usiseme mpaka kuota masagamba sikuwaga na nauli mpaka kobazi zikaisha ila nilikuwa navaa hivohivo kibishi


Nilikuwaga na suruali mbili na mashat matatu in short nilizoeleka na zile nguo kuna shati nlikuwa navaaga wananitania shati LA kijiji maana hilo hilo nilikuwa nikionekana nalo kwa sana ama kweli nilidharaulika


Nilipanga nyumba haina umeme in short haijamalizika vzur bomba pia LA maji halijavutwa ila kulikuwa na kisima kwahyo getho ni mwendo wa kibatali siku nyengine nala nje kwenye baraza la jiran kufata mwanga sometimes akiniona barazani anazima taa au napika maeneo ya nje ambao mwanga unafika nikikosa hela ya maftataa yaani kulala Giza ilikuwa kawaida


Nyumba yenyewe madirisha jamaa hajaweka wavu ameweka nondo ikabidi nizibe na safleti sasa hao mbu walinipiga doso kisawasawa plus baridi sina godoro nalalia hzo nguo zangu chache kuna siku sikuonekana nje siku nzima kumbe Niko ndani naumwa yalikuwa malaria ktk vitu nilivyojifunza Cheka na kila MTU tenda mazur kuwa mtiifu ata kama Fulani anakushambulia sababu kuna vijana na watu walikuwa wakinikubali walikuwa hawanioni wakapata wasiwasi wakachungulia ndani wakaniona ktk ile hali walinisaidia kunipeleka hospital


Mtaani kuzushiwa wizi na kina mama,Dada,baba majirani ambao Niko nao karibu kuitwa kwa mwenyekiti daah we acha tu na Yale manywele yangu yamekuwa makubwa hayana afya sina ela ya kunyoa ukicheki na nguo zimechanika utasema muhuni


Kwenda kusaidia wavuvi kuna kipindi ngalawa au chombo chetu kilipigwa na wimbi yaani tulijua tunakufa tukaanza kutoa maji na visada we acha tu .ukitoka hapo unapewa buku mbili na kisado cha uono

Maisha yalivyonizidi nikasepa nikadandia fuso yaani kweli nilikuwa mpuuz nadandia fuso litakaponipeleka ndo hapohapo na kifuko changu cha nguo (zile adidas za mgongoni) nilishawahi fika mpaka huko singida mpaka shinyanga nilikuwa nalala stendi asubuh kazi na kutafuta vibarua nakumbuka kuna mzee nilizoeana nae hapo shy mjini akanikaribisha kwake nikawa House boy


Daah hiyo mikazi ni balaa baadae akanipa baiskeli niwe bodaboda nimletee ela ( boda boda za baiskeli ) sjui kama sahiv zipo mkoa kama dar hamna na tanga zilikuwepogo nilikuwa shy twn



Ila kuufatilia magezeti kuuliza connection na wale niliosoma nao nilikuwa sichoki baadae nikasave save nikaanzisha genge lilinipa ela sana nikaeka na kibanda cha chipsi pemben pia nikamwambia mke wa yule mzee awe anatengeneza juice nimuuzie hapo tayar nishajichomoa kwake nilipata faida sana

Mungu hamptupi mja wake nikapata nafasi kwenye kampuni x INA deal na mambo ya agribusiness genge na mtaji nikamuachia mzee nikamwambia undugu kufaana sio kufanana nikapotea shy na nauli na faida tu hapo ndo nilijiwekaza sana kwenye Hio kampuni sikufanya makosa [emoji3]inaitwa fungulia mbwa nilikula mema ya nchi halafu siku narudi natoka shy nakutana na mpenz wangu namuhadithia alilia sana na alinilaumu sana kwa nn sikutaka msaada wake wakat huo na yeye alipiga hatua sana mi baharia nilikuwa napigika tu [emoji3]

Nb: kama ningejua yaan kama ningejua nisingekubali kuajiriwa pale kwenye ile kampuni bora ningepiga mishe zangu hapo hapo paliniletea maumivu kuliko kote ...the rest is history


Nowdays Niko good sina shida sina stress laifu linaenda


Sent using Jamii Forums mobile app


And yes kujibu swali la Uzi nishawahi kuwaza niwe jambazi nitumie silaha kama panga visu nk

Umepitia mengi pole sana ingawa yamepita
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
@kidukulilo akija kutoa ushuhuda wake mambo yatakuwa hivi:..

"Nimeteseka sana mimi..
Wakati nimemaliza shule pale IST nikaamua kuliko kukaa bure bora nitafute kazi
Nikaongea na mzee wangu anitafutie connection

Mzee akaniambia kuna issue canada nikasema sawa..
Nimeenda nikakuta kazi yenyewe ni kupanga mafile katika ofisi flani kwa masaa matatu kwa siku
Halafu mshahara wenyewe mdogo tu usd 300 kwa siku, nilisikitika sana...

niliteseka mimi, nyie acheni tu..

Ngoja aje humu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.

Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=

Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.

Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahah wewe ni shujaa
Mnyaki mpambanaji
 
Watu tunapitia mambo mengi sana mpaka kufikia hatua ya maisha yakueleweka kiasi fulani.

Tabu na mateso mengi hutusaidia
Kujifunza zaidi
 
Mwaka jana wakati nimefulia kodi nadaiwa, mfukoni hakuna kitu kuna jamaa yangu nikakutana nae akaniambia niende Somalia kutengeneza engine za boti kule mafundi wachache sana.

Nauli ya kufika Somalia ikawa tatizo kufika Kenya kwa kuunga ingewezekana. Kenya kwenda Somalia njia alizonipa ngumu sana.
Ikanibidi nibaki hapa hapa Tanzania.
Ukamalizaje tatizo la Kodi?
 
Hahahaha nilishaenda Amani- Muheza Tanga kwenye mashamba ya Chain, dah ule mziki wa kuchuma chai kumbe ni habari nyingine nikashindwa!

Nikarudi Muheza mjini tukaanzisha Tuition Mimi na jamaa yangu, dah tukapata mademu kadhaa na washkaji wawili hivi, kazi ikawa nzito, tukahamisshiia tuition home! Duh, mademu wawili wanakuja kila siku kutaka tuwafundishe! Tukaona huku tunakoelekea tutakopwa! Sijui waliishia wapi.


Tukajifanya mafundi Ujenzi, tukatafuta kazi kwa Mama Mmasi dah, kazi ilikua kuezeka choo! Tukaezeka, hatukulipwa maana tuliezeka vibaya!

Tukapata kazi ya kuchimba mashimo ya nguzo za Umeme za Tanesco kwenda kijiji kinaitwa Kicheba! Tukaenda na mshkaji wangu, tukakuta ardhi ni ngumu balaa na pesa ni ndogo mno!

Dah baada ya pale tukaamua tuombe nafasi za Upolisi! Jamaa yangu akaja kupata hio post Mimi nikaambiwa mfupi na marehemu RPC wa Tanga Mama Faith Amour.

Sasa hivi jamaa yangu ana cheo kikubwa tu huko kwa Sirro!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe mam faith amour alishadanja kitambo duuh

Niliwahi kaa nae mtaa mmojs kwenye nyumba ya RPC kule nguvumali ikulu
 
..kuwapiga miti mademu wa muvi za X na kujipatia kipato nje ya nchi .....hapa ningepata starehe na pesa pia...
 
1. Kuzibua vyoo
2. Kufanya usafi nyumba ya kulala wageni(logde)
3. Kubeba zege (Saidia fundi)
 
Back
Top Bottom