Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Nilikuwa nimemaliza kidato cha sita nikachukua likizo ya mwaka
Usiku kucha mkononi panga na tochi kwenye mashamba ya mpunga na vitunguu unapambania maji ili mazao yasikauke mda mwingine ukiwa unatumia mashine kunyesha inabidi ulale pembeni ya wando wa mfereji mpaka aliyeko shambani amalize au kama mnanyesha kwa zamu unalala sehemu ambayo maji yatapita ili yakifika pale uamke na hizi shughuli zote zilikuwa zinafanyika kuanzia saa tano usiku mpaka saa moja asubuhi.

Mara ukiwa unafungulia maji yaingie kwenye majaruba fisi anapita mbele yako, nyoka kwenye majani ndio usiseme ukitoa kupiga dawa kwenye vitunguu unanuka zaidi ya choo cha stendi.

Nikaweka na kiapo sitawahi kushika tena jembe kulima chochote .
 
Nimemaliza form six niko kitaani sina mbele wala nyuma, nimefaulu ila chuo sikuweza kwenda home hawakuwa vizuri. Nikaona nijichanganye mtaani maisha yaende, nikaenda kiwanda cha hizi sabuni za Kleesoft kipo Kibaha kule ndo kilikuwa kimeanza anza, asee kupata kazi ilikuwa mtiti...nikaunganishwa na jamaa mmoja hivi ni in charge mule ndani jamaa kuniona akacheka kwanza, akaniuliza mdogo wangu unaweza kazi?! Nikamwambia ndio naweza, akanambia twende nikakuoneshe kazi iliyopo, aseee nikapelekwa sehemu vipo vipande vya watu vinachimba mashimo sijui ya nini yale.
Jamaa akaniuliza tena mdogo wangu unaweza kuchimba shimo urefu wako?! Nikajitutumua tu nitaweza ila kiukweli nisingeweza hata kidogo[emoji28]. Akanambia basi niachie namba zako nitakupigia, aah wapi jamaa hakunitafuta wala nini.
 
Una mke mwema ana akili mwerevu busara na hekima... Endelea kumtunza... Sisi wengine tuliokota vituko
 
Unashangaa huyo wa mil 2.8.. wabunge wa mil 10 plus mwisho wa siku wanaishia kuwa makapuku je
 
Noma sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Pole sana
 
Baada ya kusoma comments za wadau nikipata muda nitadrop a true story about my jobless life since 2020 nikiwa chuo pale UCC

Based on a true story kuanzia maisha yangu ya chuo, maisha yangu ya forex na msoto niliopitia baada ya kufilisika kwenye forex mpaka nikaingia site nakujifunza ufundi, kubeba zege, kubeba tofali, na saidia fundi mpaka sasa mm ni mason japo sina uzoefu mkubwa...

In general afya ndio mtaji wa kwanza wa mwanadamu, fanya vyote ila usisahau kuilinda afya yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…