Wakati wa kukabidhi kombe kwa Chelsea jana sikuona Rais Trump akiwa na walinzi

Wakati wa kukabidhi kombe kwa Chelsea jana sikuona Rais Trump akiwa na walinzi

Japo ninaamini walinzi walikuwepo tena ulinzi mkubwa.

Lakini hoja yangu ni hii :

Jana kule Marekani mara baada ya fainali ya kombe la Dunia kwa vilabu wakati Chelsea wanakabidhiwa kombe , Rais wa Marekani Mhe Donald Trump alijumuika nao pamoja na Rais wa Fifa pale uwanjani .
Kilichonishangaza ni pale uwanjani ambapo Trump alijumuika na Chelsea wakati wananyanyua kombe juu na kushangilia, pia uwanja ulikuwa na watu wengi sana lakini sikuona walinzi wa Trump hata mmoja akiwa amemkaribia pale uwanjani.

Tofauti na huku kwetu Africa ambapo huwa tunaona kila sehemu Rais lazima azungukwe na wanajeshi wenye Magwanda na mitutu mizito na wengine wakiwa wamevaa suti. Pia wakati Trump amekaa jukwaani sikuona wanajeshi hata mmoja wala walinzi na mituti wakiwa wanawaangalia watazamaji.

Najuwa wenzetu wazungu wapo mbali sana katika teknolojia ndio maana huwezi kuona ulinzi manually kama Africa. Natamani sana na huku kwetu wana usalama wetu wajengewe uwezo zaidi katika vifaa vya kisasa.
Hii itasaidia pia kupunguza muingiliano katika shughuli za viongozi wetu kwani mara nyingi katika hadhira unakuta wananchi badala ya kumfuatilia Rais anachofanya au kuongea unakuta wananchi wanashangaa wanajeshi wenye mitutu.
Bila shaka wenzetu hili walishaliona na ndio maana kila ziara ya Kiongozi mkuu unakuta hakuna taswira nyingine ya kumvuta mtazamaji au msikilizaji zaidi ya Rais au Kiongozi aliyepo.
Ila Kiongozi anapofanya ziara kwenye maeneo ya vita au usalama mdogo ni kawaida kukuta majeshi na mitutu .

Tukio la.jana kule Marekani lilinifikirisha sana nikiangalia huku kwetu Africa kama Rwanda, Uganda na kwa kiasi kidogo hapa kwetu. Japo hapa kwetu ilianzia kipindi cha JPM
Hapa kwetu ni mbwembwe nyingi wakati ni magalasa matupu
 
Hauko Serious,

Rais wa USA - Ndiye Rais anayelindwa zaidi duniani. kuanzia kusweep eneo, Ulinzi kidijiti, Idadi ya walinzi waliopo on the ground, Layers za ulinzi, Snippers nk nk. Jaribu kufuatilia kuanzia kabla ya tukio (maandalizi) nk nk hizo clips huwa zipo Youtube.

Huku kwetu kwa sababu ya kutokuwa na uwezo mkubwa wa kimifumo, inalazimika walinzi kuwa karibu sana na VIP.

Agalia siku Trump anashambuliwa, Namna walinzi zaidi ya 10 walivyowahi jukwaani kuweka shield, - walikuwa kwenye jukwaa hapo hapo kwa chini - sasa imagine Rais analindwa na watu wangapi? tusijidanganye kwa kuwa TV hazichukui maeneo yenye walinzi - tukadhani hawapo>
Upo sahihi. Ndio maana nimesema natamani sana na huku kwetu wajengewe uwezo katika vifaa na kupunguza ulinzi wa kijima. We are very Manual and Primitive
 
Upo sahihi. Ndio maana nimesema natamani sana na huku kwetu wajengewe uwezo katika vifaa na kupunguza ulinzi wa kijima. We are very Manual and Primitive
Tatizo sio uwezo . tatizo ni bajeti Mkuu pamoja na transformation. Kufanya ulinzi kwa njia ya mfumo ni gharama kubwa sana na pia haiondoi ulinzi wa mannual - ndiyo maana Rais wa US kama nikivyosema ana walinzi phisical zaidi ya 300 (immediate details, law enforcement, military nk nk.
 
Hata Ukraine hukuti Rais wao kazungukwa kama jitu la madagascar
 
Back
Top Bottom