Wakati wa Nyerere na Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu na hakuna aliyeuawa

Chanzo kinafahamika! Serikali ina inteligensia kubwa kuliko wewe kizazi mbatata. Kama suala ni utekaji unadhani walioandamana wote ndugu zao walitekwa?

Huo ni wimbo mmeimbishwa kama kasuku mkajaa. Kwani waliotekwa unawajua vizuri kuliko serikali? Mbona wanaokosoa serikali ni wengi na hawakamatwi au kutekwa?

Ukishakuwa threat Kwa dola lazima ushughulikiwe ili mamilion ya watu wasiangamie Kwa sababu ya mtu mmoja.
 
..walikuwa na silaha za moto, waliuwa, walifanya uharibifu, na kuwateka nyara maafisa wa jeshi.
Walideal na jeshi na wakashughulikiwa kijeshi. Sasa hawa ndugu zetu walianza kufanya vandalism hapo polisi lazima wachukue hatua.
 
Walideal na jeshi na wakashughulikiwa kijeshi. Sasa hawa ndugu zetu walianza kufanya vandalism hapo polisi lazima wachukue hatua.

..haiyumkiniki maasi ya askari wenye silaha yazimwe kwa vifo vichache kuliko maandamano ya raia wasio na silaha. Tuache kushupaza shingo kuna tatizo kubwa ktk vyombo vyetu vya dola.
 
Kwahiyo nchi hii haina polis na mahakama ?

Shabikien tu ila hiko kikombe atakinywa kila mtu sio Zenj wala Bara mpk mkipata akil ya kuungana kukemea
 
Chanzo cha yaliyo tokea oktoba ni polisi kuanza kupiga waandamanaji
 
Aiseee!

Serikali yenu ni chafu, inahistoria ya uongo na uonevu hivyo haina moral authority ya kusema huyu tunamteka sababu anahatarisha ABC….

Kuepusha kujiamulia nani auawe au nani atekwe apotezwe, dunia ya wastarabu ilitengeneza sheria na ikaweka kitu kinaitwa mahakama, Unfortunately CCM mnaturudisha enzi za barbarism ambapo mwenyekiti wa ukoo akilala akaota kuwa Maxmello ni mtu mbaya basi kesho yake atabebwa mzobe mzobe kwenda kuuawa.

Tumerudi hatua 100 nyuma kama taifa.
 
..hata yalipotokea maasi ya Tanganyika Riffles mwaka 1964 waasi hawakuuwawa kwa wingi kama waandamanaji wakati wa Samia Suluhu.
Huko hatukuwepo na isitoshe hao walishajipambanua kuwa ni waasi. Na wale wa October 29 kama wangejipambanua hivyo huenda wasingefanywa walivyofanywa.
 
Hayo yalikuwa maandamano kweli, lakini ile ya 29/10/25 ilikuwa ni riots zilizolenga kumpindua Rais.

Nawapongeza IGP, CDF na TISS kwa kudhibiti zile vurugu ndani ya muda mfupi. Tulinunua bunduki na risasi kwa ajiili hiyo na siyo zikae ghalani kama midoli
 
..sasa kama tayari tunaujua ukweli huo kwanini serikali yetu inakwenda kuuwa wananchi wake?

..mimi nilitarajia serikali yetu itajiepusha na mauaji ili kujitofautisha na tawala zilizo dhalimu.
Kwa nini ujiepushe kuua mahayawani wanachoma miundombinu ya umma tuliyoijenga kwa kodi zetu?
 
Huko chuo cha Moshi na kwingineko, polisi hamfundishwi namna ya kudeal na waandamanaji hata wenye fujo??
FFU kazi yao pakitokea fujo na watu kuvunja mali za umma ni kupiga risasi za vichwa tena kwa kuwafata watu nyumbani???Au mnawafanya watu wajinga???
Polisi waliingia kwa lengo la kuua dhamira ilikua inaonekana kwenye matendo yenu - hatukuona kwamba mlitumia maji ya kuwasha au other means ambazo tunaamini mlimfundishwa.Kama training yenu ndo ile kuwa pakitokea fujo pigeni risasi za vichwa tena kwa kuchomoa watu majumbani, basi tuna hasara kubwa sana kama taifa.
Mali na uhai wapi na wapi??Tungesikia au kuona kuwa waandamanaji wameua wananchi kadhaa...na wanaendelea kuua..tungesema kweli, lkn waandamanaji wanaoiba mitungi ya gesi, wanaenda kwenye kituo cha mafuta, wanaacha kuchoma kisima cha mafuta, wanachoma pump, wangekua ni magaidi kama mnavyowaelezea mnafikiri walikua wanashindwa kuchoma yale mavisima ya mafuta vituoni?na kutengeneza mabomu ambapo watu wengi wangekufa????Hamuoni kuwa hao ni watu walikua wanapeleka ujumbe aggressivelly lkn pia walikua wanachukua caution..thus hawakuwa magaidi wale..You killed them in cold blood
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…