Wakati wa Nyerere na Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu na hakuna aliyeuawa

..kuiba, na kuharibu mali, hakuna anayebisha.

..tatizo liko kwenye vifo. Sina uhakika kama kuficha vifo vilivyotokea kutasaidia kupata suluhisho ya yaliyotokea.

..kwa mfano, tutajuaje kama Polisi walitumia nguvu stahiki au la, ikiwa hatujui idadi ya vifo, jinsi vifo hivyo vilivyotokea, na wapi vilitokea?
Sasa umesema. Sio kutupa lawama tu.
 
Hivi inawazekanaje kukawa na ''organized crime'' nchi nzima? Yaani wezi kuanzia Mbeya, Mwanza, Dar, Dodoma etc
Kilichotakiwa ni kulinda Waandamanaji na kukamata wahalifu
Kwa mwaka mzima Polisi walipita mitaani kwa kutisha si kusoma mazingira. Serikali ilinunua magari ya deraya si kutafuta sukuhu ya tatizo.

Nyerere hakuua ! waliopigwa viboko kwa ultimatum ni pamoja na akina Warioba ambao baadaye walikuwa washauri wa Mwalimu na leo ni Wazee wenye heshima katika Taifa.

Maadamano yale ya Mwinyi kutoka Wanafunzi wa UDSM mmoja wao alikuwa James Mbatia, yupo hai hakukuuawa na ni kiongozi anayeheshimika pia

Mwaka 1964 ilikuwa ''army mutiny' washiriki wakiwa askari . Hakuna Raia aliyeshiriki .
Kilichotokea MO29 ni ''mass uprising' kwa maana yake halisi ikifanywa na Raia

Kutenganisha mambo hayo mawili ni muhimu!

JokaKuu
Samia walitaka kumletea dharau labda kwa jinsia yake hawakujua kwamba Rais ni taasisi unayemuona mbele ya mimbari huwa kiongozi wa taasisi ya urais.

Kilichotokea tarehe 29 October kitaendelea kukaa ndani ya vichwa vya hawa Gen Z, kwamba huwezi kuipelekesha serikali kwa ujinga wa maandamano. Siku ya uchaguzi polisi pekee yao walikuwa kazini muda ulivyozidi kuendelea wakaingia kazini kikosi maalum cha Ngerengere Morogoro kikashughulika na upuuzi wote.

Enzi za Nyerere na Mwinyi hatukuwa na instagram, hatukuwa na whatsapp hatukuwa na huu uwazi wa uongozaji wa nchi wanaokumbana nao marais wa kuanzia awamu ya tano.

Palikuwa na usiri ambao ulichangiwa na dunia nzima kuwa gizani kimaendeleo.
 
Hivi inawazekanaje kukawa na ''organized crime'' nchi nzima? Yaani wezi kuanzia Mbeya, Mwanza, Dar, Dodoma etc
Kilichotakiwa ni kulinda Waandamanaji na kukamata wahalifu
Kwa mwaka mzima Polisi walipita mitaani kwa kutisha si kusoma mazingira. Serikali ilinunua magari ya deraya si kutafuta sukuhu ya tatizo.

Nyerere hakuua ! waliopigwa viboko kwa ultimatum ni pamoja na akina Warioba ambao baadaye walikuwa washauri wa Mwalimu na leo ni Wazee wenye heshima katika Taifa.

Maadamano yale ya Mwinyi kutoka Wanafunzi wa UDSM mmoja wao alikuwa James Mbatia, yupo hai hakukuuawa na ni kiongozi anayeheshimika pia

Mwaka 1964 ilikuwa ''army mutiny' washiriki wakiwa askari . Hakuna Raia aliyeshiriki .
Kilichotokea MO29 ni ''mass uprising' kwa maana yake halisi ikifanywa na Raia

Kutenganisha mambo hayo mawili ni muhimu!

JokaKuu
Tarehe 29 hapakuwa na maandamano palikuwa na uasi fulani wenye kufanana na mapinduzi lengo lao haswa kuirudisha nyuma Tanzania kwa kuharibu maeneo maalum ambayo yangeurudisha nyuma uchumi wa Tanzania.

Lengo lao ni pana zaidi ya kile kinachoonekana kwa macho. Walitaka kuichoma TPA jiulize Tanzania ingepoteza pesa kiasi gani katika kuikarabati bandari ile.

Walitaka kuchoma kituo cha mabasi cha Magufuli, jiulize hiyo hasara ingeumiza uchumi kiasi gani katika suala la mawasiliano.

Jiulize wepesi wa viongozi wa mataifa ya kigeni kuilaani Tanzania baada ya mauaji bila kwanza kujiridhisha na maoni yao kama yanatenda haki kwa pande zote mbili zilizokuwepo kwenye uovu ule.

Lengo linakuwa kuichafua taswira chanya iliyojengwa tangu miaka ya 60, hii ni vita inahitaji fikra pana kuweza kufahamu namna inavyopiganwa.
 
Not true! hakuna suala la uchumi. Kuna genuine complains ya Wananchi ikiwemo utekaji na kupoteza watu, matumizi mabaya ya rasilimali, viongozi kufujam kubananga demokrasia, kufunga wapinzani ili kupata ushindi.
Those are concerns za Watanzania na zinajulikana. Kwani Gwajima ni beberu?

Ushahidi gani?

Kwa ushahidi gani?

EAC, SADC, AU! Need say more? Thabo Mbeki, Ian Khama etc

Tumechafua taswira yetu wenyewe! hakuna kutafuta mchawi.
 
Uchumi huwa ni huu huu miaka yote kwanini muda huu ndio watu wainuke kudai haki, kitu gani cha ajabu kitokee 2025 kisitokee 2010?.

Rasilimali zinatumiwa kadri zinavyopangiwa matumizi yake, nchi inajengwa kila kona, sio rahisi pia kumpatia kazi kila kijana anayemaliza chuo.

Wapinzani wanafungwa kutokana na kukiuka sheria za nchi, huwezi kuleta ubishi katika suala la wazi halafu ukategemea uachiwe huru tu.

Kuhusu ushahidi kuna masuala huwezi ukayaanika hapa jukwaani lakini ndio ushahidi wenyewe. Vijana walikuwa wanaelekea kuharibu miundo mbinu nyeti ya uchumi wa Tanzania wakawahiwa kabla hawajaleta uharibifu.

Upo ushahidi wa jamaa kutoka Kenya kuletwa na Heche na wakasumbua sana kule Mara siku ya uchaguzi wenyewe, Heche aliahidi kabisa kwamba uchaguzi hautafanyika na alirekodiwa akiyasema hayo.

Walikata watu vidole, haya masuala ya kinyama hatukuyafahamu, walichoma moto mwendokasi ambao wadogo zao wakaja kusota wakikosa usafiri wa kutoka Kimara kuingia mjini kwa mwezi mzima.

Hao marais wa Botswana na South Africa walikuwa na matatizo yao binafsi, mengine yaliyotokea ndani ya Tanzania hawakuyafahamu wakaishia kuongea kidiplomasia. Mbona Rais wa Zambia na wa Burundi walikuja kwenye sherehe za kumuapisha Samia?.

Hili zengwe lote limetengenezwa kutokea huko nje kwa makusudi maalum siku zote kadri Taifa linavyokuwa linakutana na changamoto kubwa zaidi.
 
Huelewi kinachozungumzwa. Sijui umeona kichwa cha habari hii tunayoijadili na kukielewa? Kwa taarifa tu, mimi najadili hili bandiko.

Nimesema wakati wa Nyerere na Mwinyi kulikuwa na maandamano nayo yakazimwa kama yalivyozimwa yale ya MO29, ila katika maandamano hayo waandamanaji hawakuiba, hawakuharibu mali wala kuua askari.

Pamoja na yote hayo, bado yalizimwa na polisi baada ya kuonekana uwezekano wa kutokea fujo na uharibifu seuze yale yaliyofanywa kwa kushiriki katika wizi, uharibifu wa mali na mauaji ya askari.

Risasi zilikuwa ni matokeo ya uuaji wa askari, wizi na uharibifu wa mali.

..unasema UONGO.

..maandamano ya wakati wa Nyerere, na Mwinyi, hayakuzimwa kwa unyama na udhalimu kama ya Oct 29, 2025.
 
Uchumi huwa ni huu huu miaka yote kwanini muda huu ndio watu wainuke kudai haki, kitu gani cha ajabu kitokee 2025 kisitokee 2010?.
Hakuna suala la uchumi! masuala ni Haki yanazungumzwa!
Wapinzani wanafungwa kutokana na kukiuka sheria za nchi, huwezi kuleta ubishi katika suala la wazi halafu ukategemea uachiwe huru tu.
Kushtaki ni haki, kushtakiwa ni haki. Kuachiwa huru ni haki, kufungwa jela ni haki.
Tatizo ni pale haki inapotolewa kwa kuminywa. Mahakama isitumike kama chaka !
Kuhusu ushahidi kuna masuala huwezi ukayaanika hapa jukwaani lakini ndio ushahidi wenyewe. Vijana walikuwa wanaelekea kuharibu miundo mbinu nyeti ya uchumi wa Tanzania wakawahiwa kabla hawajaleta uharibifu.
OK ! tuamini tu kwasababu umesema!!!
Upo ushahidi wa jamaa kutoka Kenya kuletwa na Heche na wakasumbua sana kule Mara siku ya uchaguzi wenyewe, Heche aliahidi kabisa kwamba uchaguzi hautafanyika na alirekodiwa akiyasema hayo.
Je, Heche ameshtakiwa kwa kosa hilo?
Yule mwanajeshi wa Kenya uliyesema ameshtakiwa mahakama gani?
Walikata watu vidole, haya masuala ya kinyama hatukuyafahamu, walichoma moto mwendokasi ambao wadogo zao wakaja kusota wakikosa usafiri wa kutoka Kimara kuingia mjini kwa mwezi mzima.
Walichoma moto vituo vya kupigia kura! je ni kweli?
Hao marais wa Botswana na South Africa walikuwa na matatizo yao binafsi, mengine yaliyotokea ndani ya Tanzania hawakuyafahamu wakaishia kuongea kidiplomasia. Mbona Rais wa Zambia na wa Burundi walikuja kwenye sherehe za kumuapisha Samia?.
EAC.SADC.AU
Hili zengwe lote limetengenezwa kutokea huko nje kwa makusudi maalum siku zote kadri Taifa linavyokuwa linakutana na changamoto kubwa zaidi.
Haya ni matatizo ya ndani yashughulikiwe na sisi wenyewe. Hatuwezi kupata suluhu kama tutaficha ukweli kwa kusingizia watu. Hizi habari za mabeberu zilikuwa miaka 80.90, kwasasa hakuna anayezisikiliza!
Ironically, mtu akiongelea mabeberu anaonekana mufilisi wa hoja! archaic
 
..unasema UONGO.

..maandamano ya wakati wa Nyerere, na Mwinyi, hayakuzimwa kwa unyama na udhalimu kama ya Oct 29, 2025.
Nazungumzia kuzimwa kwa maandamano, pamoja na kwamba waandamanaji hawakuharibu mali, ila ilpoonekana kuna uwezekano wa kutokea uhalifu yalizimwa kuzuia uhalifu usitokee. Waandamanaji wakazuiwa kwa virungu walipofika Urafiki na wako walioumia.

Sasa kama wakati wa Nyerere wanaandamanaji ambao hawakufanya uharibifu wala wizi walicharazwa viboko, vipi leo ambapo waandamanaji wameua, wameiba na wamefanya uharibifu wa mali ulitarajia waachwe? Waswahili wanasema " kimbia ugwe hujaona ng'ombe".
 
Kwenye kichwa changu. Hoja kwamba waandamanaji waliuawa inatoa wapi?
Rais na Bunge walisimama kimya kwa watu waliouawa. Kuna picha mortuary za maiti zilizolundikwa
Tumezika wapendwa kwa ushahidi.
 
Ikiwa huo ndo ushahidi, huku mtaani tulizika askari waliouawa na waandamanaji.
 
..askari Polisi wangapi walikufa?

..walikufa katika mazingira gani?

..Na wamezikwa wapi kwa utaratibu gani?
 
..askari Polisi wangapi walikufa?

..walikufa katika mazingira gani?

..Na wamezikwa wapi kwa utaratibu gani?
Hao wako unosema waliuawa waliuwawa wangapi na kwa ushahidi gani wa kuaminika?
 
..kuna picha zinaonyesha miili ikiwa ktk hospitali mbalimbali.

..basi angalau tungeonyeshwa maziko ya Polisi waliouwa katika maandamano.

..mbona Polisi waliouwa na magaidi wakati wa Magufuli tuliona wakiagwa kwa heshima za kijeshi? Kulikoni hawa waliouwawa wakiwa kazini siku ya Oct 29?
 
Back
Top Bottom